Maisha bora ni yapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha bora ni yapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtumiabusara, Oct 11, 2010.

 1. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  NDUGU WANA JAMVI, NIMEKUTANA NA ARTICLE HII KATIKA MAIL ZINAZOZUNGUKA MTAANI

  Subject: Maisha Bora ni yapi?

  Viongozi wa juu wanalipwa mishahara mizuri sana na hapo hapo hawalipii zile huduma muhimu ama kutokana na huduma hizo kulipiwa na serikali au wapo katika taratibu ambazo zinawasaidia kupata huduma hizo bure. Kwa mfano; Waziri, Katibu mkuu, mkurugenzi, commissioner n.k hawa wanapata mishahara mikubwa sana. Lakini pia serikali inawapatia usafiri, nyumba na pia wamo katika utaratibu wa mifuko ya afya na hivyo wanatibiwa katika hosptali nzuri za hapa nchi na hata nje bila wao wenyewe kulipia. Viongozi hawa wananunuliwa mpaka samani za ndani na fungu kubwa sana la pesa ambazo zinatengwa kila mwaka kwa ajili ya kubadilisha smani za majumbani mwa.

  Sasa tuchuku mfano mwingine, wa "Manganga bin Kuchoka" ambaye yeye ni tarishi katika Wizara ya kwa mfano Jinsia na watoto. Kwa hiyo nyongeza unayoizungumzia analipwa 160,000. Hiyo 160,000 anunue chakula, apange nyumba na alipe kodi, ajigharamie matibabu, usafiri na asomeshe watoto. Anhangaika kwa kila kitu. Na mahitaji yake yote ni lazima atoe pesa zake mfukoni. Anakaa kama ni hapa Dar labda Mbagala. Unajua ananunua maji kila siku kiasi gani? kwa taarifa yako mtu mwenye familia ya watu sita kwa kujibana sana, anatumia si chini ya 5,000 kwa kununua maji tu. Kwa mwezi ni 150,000.

  Anakaa katika mazingira magumu sana, nyumba imechoka haina hata wavu wa mbu. Hivyo anaumwa malaria yeye na watoto wake kila mara, unajua kutibu malaria ni kiasi gani? mifereji ya maji machafu inapita karibu na nyumba yake. Hivyo anaumwa tumbo kila mara. Most likely watoto wake watasoma katika shule za "Msondo Ngoma" au yebu yebu ambazo hazina vitabu wala walimu wala madawati. Katika mazingira haya watoto hawa hawawezi kupata elimu bora, hawawezi kushindana katika ulimwengu huu wa utandawazi, wanaweza waka drop katika masomo yao, wakaanza kuuza karanga na watoto wa kike wakaanza kufa uhuni na matokeo yake ni kupata ujauzito au UKIMWI. Hivyo umaskini unaendelea na huo ni mzunguko wa umaskini.

  Licha ya kulipwa maslahi mabovu hakuna mipango ambayo inamlenga mtu huyu wa chini ili aweze kupata unafuu. Badala yake ile mifumo na mipango ya kutoa unafuu inawalenga wale wale ambao wanapata mishahara na allowances nono. Ngoja nikupe figures:  • 59% ya pesa za budget yote zilikwenda katika kulipa allowances kwa watumishi wa ngazi za juu kama wakurugenzi na wengineo. Nusu ya pesa hizi iwapo zitapelekwa katika mishahara inawezekana kabisa serikali kuweza kulipa mishahara hiyo.
  • 2006/2007 113 Billion zilitumika katika allowances.
  • Mbunge baada ya kuwa bungeni kwa miaka 5 analipwa 45 million kama kiinuo mgongo wakatika mfnyakazi wa kawaida "Manganga Bin Kuchoka" analipwa 4 million baada ya kufanya kazi miaka 40.
  • Waziri akifungua semana au workshop analipwa 1.2 million
  • Naibu Waziri analipwa 900,000
  • Katibu Mkuuu analipwa 600,000


  Kwa nini nimekupa hizi figures? Nikukufahamisha kuwa usidanganyike kuwa eti serikali haina uwezo. Si kweli uwezo upo. Kinachokosekana ni ubinadamu wa kuwafiiria wengine, ujasiri wa kufanya maamuzi magumu, ubunifu na mipango mizuri.

  Hiyo ni moja lakini nebda kasome ripoti ya CAG uone ubadhirifu na ufujaji wa fedha katika taasisi na wizara serikali. Mabilioni ya pesa yanapotoe. Kwa mfano tuna tatizo kubwa sana la "ghost workers". Iwapo tutaziba mianya ya "ghost workers" tunaweza ku save pesa nyingi sana ambazo tunaweza kuzitumia kuboresha maslahi ya watumishi wa serikali.

  Ayoub na wanabidii, tunapoteza mapesa mengi sana. Believe me. Ukisoma Daily News la jana utaona CAG katika ripiti yake anasema kuwa hakuweza kuona mkataba wowote kati ya serikali na TRL juu pesa ambazo serikali iliikopesha TRL kwa ajilii ya top up ya mishahara ya wafanyakazi. Hiyo ni moja tu. Lakini angalia pesa tunazopoteza katika magogo, samaki, madini n.k n.k.

  Mfano, tumeuza nyumba za serikali, halafu tunateua mawaziri chungu nzima, tumeteua majaji chungu nzima (kumbuka tunateua majaji bila ya kujenga vyumba vya mahakama). Hawa wote wanahitaji nyumba za kukaa. Nyumba tumekwishauza. Tunawaweka hotelini na kulipa pesa chungu nzima. Baadhi ya wakubwa wengine wanapangishiwa nyumba na zinalipiwa hadi dola za kimarekani 8,000. Yaani hata nchi tajiri hazifanyi ujinga huu. Halafu unasema hatuna uwezo!!!?

  Kwa hiyo uwezo upo kinachokosekana ni fikra za kimpainduzi kuleta mabadiliko ya namna tunavyoendesha mambo yetu. Nina hakika kwa mfano mtu akifanya utafiti anaweza kugundua a lot of waste. Kwa mfano huu uamuzi wa kuhamia Dodoma unatugharimu kiasi gani kwa wiki, kwa mwezi, kwa mwaka na kwa miaka mitano. Tunahitaji bold minds.


  Nakumbuka juzi niliona na kusikia kwenye baadhi ya vyombo vya habari
  kuwa kua ujumbe wa Watu wa Ujerumani wanaitembelea Tanzania na
  Mjerumani mmoja akasema hivi: SIELEWI NI KWA NINI NCHI HII YA TANZANIA
  NI MASKINI ILHALI INA UTAJIRI WA KUPINDUKIA!!!!!!!!!!!
  Yaani mjerumani wa watu haelewi,anajaribu kufikiria kuna tatizo gani
  mpaka hali iwe hivi. Ujumbe huohuo wa WAJERUMANI ukatembelea Reli ya
  Kati inayotoka Dar kwenda Mwanza na Kigoma hawakuelewa ni KWANINI RELI
  HIYO INA HALI MBAYA NA IMEACHWA BILA MATENGENZO KWA MUDA MREFU. Reli
  ya Kati mtakumbuka impaka hivi majuzi ilikuwa inaendeshwa na matepeli
  wa Kihindi wanaojiita RITES!

  Natamani ningelikuwa karibu na hao wajerumani ningeliwaambia kuwa
  MATATIZO YOTE HAYA YA TANZANIA KUWA MASIKINI HUKU IMEZUNGUKWA NA
  UTAJIRI LUKUKI NA UCHAKAVU WA RELI YA KATI YANASABABISHWA NA SERIKALI
  YA CCM ILIYOKO MADARAKANI.

  Kwa hiyo dawa ni kuwang'oa CCM madarakani kwenye Uchuguzi wa mwaka huu
  ili nchi hii iweze kuondoka kwenye lindi la umaskini.
  Kuna ndugu zetu wa pale Botswana. Botswana wana uchumi wa kupigiwa
  mfano katika Afrika wao wanafukuzana na SA kwa karibu. Botswana wana
  madini aina moja tu Almasi na kitu kingine kinachoinua uchumi wao ni
  Ng'ombe,wanauza nyama ya ng'ombe nje ya nchi!!!!. Uchumi wao ni
  super.Kwanini wamefanikiwa? Ni kwasababu ya Utawala bora wenye sera
  safi za serikali iliyoko madarakani.

  Hapa Tanzania tuna Almasi za Mwadui,Dhahabu imetapakaa ukanda wote wa
  Kanda ya Ziwa,tuna Tanzanite(Madini ambayo yanapatikana Tanzania peke
  yake hapa Duniani)nayo yamejaa tele huko Kanda ya Kaskazini Arusha na
  maeneo yake ya jirani. Gesi nayo ipo Songosongo na Ukanda wote wa
  Kusini. Uranium nayo imeonekana sehemu za Dodoma na maeneo ya jirani.
  Hapa sijazungumzia Mbuga za Wanyama na raslimali zingine. Bado
  sijazungumza kuhusu mifugo tuliyo nayo ikiwemo Ng'ombe,Mbuzi,Kondoo
  n.k

  Kwanini tuendelee kuwa masikini?? Shime Watanzania wenzangu mwaka huu
  tusema basi kama msemo wa enzi za Mwalimu wa Tumeonewa kiasi cha
  kutosha,tumenyonywa kiasi cha kutosha,tumenyanyaswa kiasi cha
  kutosha,unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe,tunyonywe na tunyanyaswe
  na sasa tunasema CCM BASI IMETOSHA

  Tusiseme kuwa hatuna uwezo. Tunatakiwa tubadilishe fikra. Tuseme inawezekana kubadili uongozi na kuchagua Kiongozi mwenye uchungu na Taifa hili. Tusidanyike

  Asante
  Mungu Ibariki Tanzania
   
 2. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,806
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Maisha bora ni ya JK na wanaomzunguka na ndio maana alisemaga ktk kampeni zake awali! lakini siyo ya Mdanganyika!
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Labda haya.....

  [​IMG]
   
Loading...