maisha bila marafiki

Mbona sikuelewi unawezaje kuishi bila rafiki ina maana huna watu wanaokuzunguka au wewe umekamilika kila kitu?
hebu naomba nifafanulie zaidi.
 
Nina marafiki wengi ila sina best friend.
Bf/gf/wife/husb si sahihi kusema ndio best friend wako maana huyo ni zaidi ya best.
Siwezi kuishi bila marafiki maana 70% ya furaha yangu inatoka kwa marafiki.
Ahsante the boss kwa thread lenye akili.
 
rafiki wa kusaidiana kwenye shida na raha niwachache sana au hawapo kabisa, mie rafiki yangu ni mume wangu, watoto wangu na mama yangu basi.

maisha yakiwa mazuri wengi watajitokeza kama vile ni marafiki, maisha yakibadilika unaweza usimwone hata mmoja.
 
Asanteni wadau kwa mawazo yenu,nimepata mengi nakujifunza kua wingi si hoja bali ubora,hivyo ni bora kua na marafiki wachache wa ukweli kuliko wengi wazushi.pamoja tunajenga taifa.
 
Tafiti nyingi zinzonyesha kua mtu aliye mpweke hua hana furaha na mra nyingi hupata msongo wa mawazo maana hana mtu wakumweleza matatizo yake na furaha zake.ila mtu aliwa na marafiki wengi wakumfariji wakati wa matatizo na wa kushirikiana nao wakati wa furaha mtu huyu huishi maisha marefu.nawasihi wana jf kuwa na marafiki na kuepuka upweke.

nibora kuwa na marafiki wachache wenye akili kuliko wengi wenye kukutia karaha. Hili nalo ulikumbuke maana adui zako ni rafiki zako.
 
Kweli rafiki ni muhimu ila kwa kweli kupata real rafiki siku hizi ni ndoto. Imekuwa unafiki mwingi. Mtu anajifanya rafiki yako kumbe kuna kitu anataka kwako. Mtu anajifanya rafiki yako ili umsaidie issue fulani ila kiukweli sio rafiki. Ule urafiki wa kweli umepoteza maana na ndio maana wengi wana hiari kusema wana washkaji wanaofahamiana ila sio best friend tena. Dhana ya best friend unayemwamini na kumkubali ambaye atakuwa na wewe kwenye shida na raha imepoteza maana. Unafiki na kujipendekeza ndio umejaa siku hizi.
 
Nina marafiki weng ila sijapata the best coz i dont trust any1 even my own dat why sina bestf even my wife
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom