Maisha baada ya kumzika mwanangu

Maisha baada ya kumzika mwanangu

Grealish10

Senior Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
104
Reaction score
295
Habari ndugu zangu,

Asante kwa wote mliolia nami katika kifo cha binti yangu mpendwa aliefariki kwa uzembe wa watu wa afya, faraja yenu ilikuwa tiba sana sijaamini JamiiForums kuna watu wana roho nzuri hivi na wanaumia kwa matatizo ya watu.

Maisha baada ya maziko yamekuwa magumu sana muda wote nalia nimeshindwa kurejea kawaida, kwa sasa natamani kufa tu maana naona giza kuna njia yoyote ya kusaidia kuondoka hali niliyonayo?

Naishi peke yangu mama yake tulikuwa hatukai pamoja ila yeye baada ya msiba amehama mkoa kabisa.

Pia soma - Kifo cha mwanangu kipenzi kimetokana na uzembe
 
Pole sana mkuu, jipe moyo hayo ni mapito yataisha tu
 
Thats nature binadam lazma afariki bila kujali umri wake, hilo ni jambo tuu ambalo lingetokea na kukuumiza tuu hata baada ya miaka mingi mbele..

Kufa ni wajibu na lazima tujiandae tuu kuwa wapendwa wetu iko siku tutawakosa.

Mimi nilifiwa mfululizo mwaka jana lakini nikakumbuka tuu kuwa binadamu sisi ni wapitaji tuu.

Usiwaze kujiua sababu utakuwa umetengeneza tatizo kubwa zaidi kuliko unavyodhani.

Jikaze jaribu kutoka nje mbali na mazingira kumbukishi ya mwanao.

Safiri kidogo km uwezo upo.

Jichanganye na ndugu jamaa au marafiki..

Piga mastori sana cheki muvi.

Basi muda ukifika utapona tuu uwe sawa
 
Hutomuelewa mleta mada kama huna mtoto yaani mtoto purukushani zake huanza pale akitembea. Ndani ya nyumba huwa inachangamka sana akiwepo mtoto leo kaondoka milele. Nyumba huwa inapwaya sanaa mpaka unaichukia hakika mfiwa pole sana.

Kwioooo
 
thats nature binadam lazma afariki bila kujali umri wake,
hilo ni jambo tuu ambalo lingetokea na kukuumiza tuu hata baada ya miaka mingi mbele..
kufa niwajibu na lazma tujiandae tuu kuwa wapendwa wetu iko siku tutawakosa.
mimi nilifiwa mfululizo mwaka jana lakini nikakumbuka tuu kuwa binadam sisi ni wapitaji tuu.
usiwaze kujiua sababu utakuwa umetengeneza tatizo kubwa zaidi kuliko unavyodhani.
jikaze jaribu kutoka nje mbali na mazingira kumbukishi ya mwanao.
safiri kidogo km uwezo upo.
jichanganye na ndugu jamaa au marafiki..
piga mastori sana cheki muvi.
basi muda ukifika utapona tuu uwe sawa

Maneno mengine ni ya kufarijiana tu ila kuzika mtoto kusikie tu.

Hakuna huzuni kubwa kama kwa baba kumzika mwanae.
 
Pole sana broo Ni jambo la kuomba Mungu sana akupe ujasili na uvumilivu kwa kweli ni ngumu sana kuweza kusahau kifo cha mtoto. mimi tu nikitaka kujiweka kwenye hali yako machozi yananitoka its a very hard situation kufiwa na mtoto kwa kweli..
 
Poole sana ndugu. Mshirikishe Mungu kwenye mapito yako.
 
Kaka kujitoa uhai sio suluhu. Muachie Mungu muweza wa yote. Kesho yako ni kubwa yenye baraka. Utapata watoto wengine kwahio kumpoteza huyo mmoja usione ni mwisho wa maisha...
 
Hutomuelewa mleta mada kama huna mtoto yaani mtoto purukushani zake huanza pale akitembea. Ndani ya nyumba huwa inachangamka sana akiwepo mtoto leo kaondoka milele. Nyumba huwa inapwaya sanaa mpaka unaichukia hakika mfiwa pole sana.

Kwioooo
Ni kweli mkuu yani naamka nalala kama gogo mimi
 
acha kufa akiugua tuu moja haikai wala mbili..
Kweli kabisa mkuu! Hii ilinikuta mwezi January, kijana wangu alianza kuhisi maumivu makali sana ya mgongo mpaka kukaa alikuwa hawezi. Akilala nako kuja kuamka ni shida! Yaani ikawa kukaa kwake mpaka aweke mto nyuma ya mgongo.

Sasa anatakiwa kurudi shule kwa hali hiyo anasomaje masomo yake ya sayansi. Nilikuwa kila nikiingia namkuta anlivyokaa natoa machozi kama mwehu! Kwa kweli aliniliza sana! Namshukuru Mungu alisimama na sisi katika maombi sasa hivi mzima wa afya!
 
Take heart mkuu. You will one day make a very wonderful reunion. Usijifungie ndani always jichanganye na marafiki ili kukuondolea ukiwa
 
Habari ndugu zangu,

Asante kwa wote mliolia nami katika kifo cha binti yangu mpendwa aliefariki kwa uzembe wa watu wa afya, faraja yenu ilikuwa tiba sana sijaamini JamiiForums kuna watu wana roho nzuri hivi na wanaumia kwa matatizo ya watu.

Maisha baada ya maziko yamekuwa magumu sana muda wote nalia nimeshindwa kurejea kawaida, kwa sasa natamani kufa tu maana naona giza kuna njia yoyote ya kusaidia kuondoka hali niliyonayo?

Naishi peke yangu mama yake tulikuwa hatukai pamoja ila yeye baada ya msiba amehama mkoa kabisa.
Mzee kanisa la Yesu linakuita nenda kanisani kama uko dar eagt city center kwa pastor katunzi ni sehem sahihi sana kusali....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom