Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,742
Mpe maziwa ya mama na wala hayo maini ya n'gombe kwani kuongezeka kwa kilo ataongezeka baadae. Kinachotakiwa Mama anaye mnyonyesha ale chakula chenye mlo wenye afya anywe supu ya kuku wakienyeji yenye pilpili mtama kwa wingi, Atengeneza uji wa mtama wenye pilipili kali za mtama pilpili mtama atwange kuwa unga akipika uji atie huo unga pilpili mtam ndio anywe mama mnyonyeshaji. Msikimbilie kumpa vyakula mto wa miezi 9 nyie vipi hamna huruma na hicho kiumbe alichukupeni Mungu?Hujamaliza kusoma hapo juu. Nimesema wana miezi tisa.
Asante kwa ushauri mkuu.
🔸🔸VYAKULA MUHIMU KWA MAMA ANAYENYONYESHA🔸🔸
➡matunda na mboga za majani
Mama unayenyonyesha jitahidi kula matunda ya aina tofauti tofauti kwa siku. Hakikisha unakula mboga ya kutosha katika mlo wako. Hii itasaidia ongezeko la maziwa mazito.
➡nyama ,samaki
➡viazi vitamu,mihogo,magimbi,boga,wali (brown rice) oat,mahindi,maziwa nk.
➡supu. Nk
🔸🔸🔸MBEGU ZINAZOCHOCHEA MAZIWA YA MAMA🔸🔸
➡mbegu za maboga.
Tafunambegu za maboga au tumia unga wa mbegu za maboga kwenye chakula au kinywaji chako.
➡mbegu za uwatu(fenugreek seeds)
Tumia mbegu za uwatu katika kinywaji,supu. Tafuna zenyewe . Pia waweza changanya kwenye chakula kama
wali.
➡mbegu za ufuta (black sesame seeds)
Changanya mbegu za ufuta na maziwa na almond. Saga na unywe .
➡fennel seeds(mbegu za shamari)
Mbegu hizi unaweza changanya kwenye mboga mboga.,kwenye chai,chemsha pamoja na maziwa au waweza tafuna zenyewe.
➡cumin seeds(uzile)
Changanya unga wa uzile kwenye maziwa na unywe.
➡pilipili manga. Pilipili nyeusi
Changanya kwenye uji au supu Unga wa pilipili manga
➡nuts
Kama karanga,korosho,almond, tafuna mbegu izi mara kwa mara.(baadhi ya nuts zinaleta alleg kwa mtoto. Mama kua makini wakati wakati wa kutumia muts.
🔸🔸mbegu izo zinachochea muongezeko wa maziwa ya mama. Na kufanya yatoke mengi na mazito. Hivyo kumuwezesha mtoto kushiba.
Ingawa unatumia mbegu hizo mama unayenyonyesha jitahidi kula chakula bora. Usikose matunda na mboga za majani kwenye mlo wako . Pia jitahidi kunywa maji lita 2 had 3 kwa siku. Kufanya hivyo
kutafanya upate maxiwa mazito na yenye virutubisho kwa afya ya mtotowako.
Hakikisha mtoto ananyonya ziwa moja kwa dk 15 had 20 . Ndo umuhamishie ziwa lingine. Kwani mtoto anapoanza kunyonya ananyonya kwanza maji then mwisho ndo chakula chenyewe. Ukiwa unanyonyesha nusu nusu anakua anashiba maji na kuacha chakula chenyewe .Ndo mana mtoto chini ya miezi sita huruhusiwi kumpa hata maji kwani maziwa anayonyonya yanamtosheleza.
Mama unayenyonyesha jitahidi unaponyonyesha mtoto ule weusi wote uingie mdomoni ili kumuepusha mtoto asivute hewa wakati ananyonya
