Maimamu waliohamasisha fujo wamechukuliwa hatua gani?

Top Cat

Member
Aug 31, 2009
97
23
Misikitini
Katika Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni, Imamu wa msikiti huo, Alhaji Wallid Alhad, alipigwa na baadhi ya waumini pale alipowataka kutofanya maandamano kwa maelezo kwamba hayakuwa na tija.

"Wekeni hasira zenu chini na mkitoka humu msiweke vikundi kwani Sheikh Ponda kakamatwa na yuko chini ya dola na jana (juzi), alifikishwa mahakamani ambako haki itatendeka," alisema Alhaji Walid. Alisema Sheikh Ponda yupo katika hali nzuri mikononi mwa Serikali na haki itatendeka.
Kutokana na kauli hiyo, waumini walimgeukia na kuanza kumwandama, hivyo kuzusha vurugu ndani ya msikiti huo... "Haiwezekani... huyo anatumika kuzuia maandamano, ametumwa na watu wasio utakia mema Uislamu acha tumpige," ilisikika sauti ya mmoja wa waumini.

Hata hivyo, waumini hao waligawanyika na baadhi yao walimkingia kifua na walifanikiwa kumtoa nje na kumwondoa kwa nguvu katika eneo la msikiti huo kwa gari.

Katika Msikiti wa Mtambani, Kinondoni kabla ya swala ya Ijumaa, Imamu wa msikiti huo alisikika akiwahamasisha waumini wake kutoogopa polisi na kwamba anayepaswa kuogopwa ni Allah. Baada ya swala hiyo, wakati wanajiandaa kufanya maandamano hayo, Polisi waliwadhibiti walipofika eneo la Kinondoni kwa Manyanya kwa kuwatawanya kwa baruti.

Katika Msikiti wa Idrissa, Kariakoo, Imam wa Msikiti huo baada ya swala ya Ijumaa alianza kuwahamasisha waumini wake kufanya maandamano kwenda Ikulu kwa kutumia Barabara ya Msimbazi karibu na Kituo cha Polisi Msimbazi.
Walipofika karibu na kituo hocho, walizuiwa na askari na kuanza kurusha mawe ambayo yalijibiwa kwa mabomu wa machozi. Hali hiyo ilidumu kwa takriban dakika 15.
Iliwalazimu polisi kuongeza nguvu kwani mbali na magari matano yaliyokuwa na polisi wa kutuliza ghasia, waliwasili wengine wapatao 16 wakiwa kwenye pikipiki nane.

Baada ya swala ya jioni kundi kubwa la waumini lilirejea tena barabarani na polisi waliamua kutumia maji ya kuwasha na kuwakamata baadhi ya watu waliokuwa katika kundi hilo.
 
wamehamasisha vurugu, wamesikika na mahazeti yameandika. hatua gani zimechukuliwa na kova?
asante Mwamunyange kutuokoa hiyo jana!
 
Hata hivo nimegundua kuwa sisi waislam waoga mbwembwe nyingi hatuna lolote mimi nilikuwa kariakoo jana mtu unamsalimia Asalam alaikhum anajibu Milele Amina. Nikasema ama kweli kipigo ni noma hata maustaz waoga kiasi hiki duu? Haya bana tuache ushabiki wa kufuata kila kisemwacho kama mabehewa ya treni.
 
Back
Top Bottom