Maigizo ya ICC na Afrika

kabagile

Member
Jan 15, 2016
64
11
Nimejiuliza saana ingawa sikushuhudia huo uharifu uliotokea Kenya kipindi hicho cha uchaguzi na Bw Rutto nawenzake kutuhumiwa kama wahusika/vinara wa vurugu hizo. Le
 
Umejiuliza nini? Hukushuhidia huo uharibifi... sasa kuna maigizo gani?
 
Nimejiuliza saana ingawa sikushuhudia huo uharifu uliotokea Kenya kipindi hicho cha uchaguzi na Bw Rutto nawenzake kutuhumiwa kama wahusika/vinara wa vurugu hizo. Le
Aisee? Huenda ulikua mtoto mdogo, maana 2007 hadi sasa ni karibu miaka 8-9, ni Muda mrefu umepita

Ila kwa ufupi tu watu 1700 walipoteza maisha kwenye vurugu ambazo zilianza kama vurugu za kisiasa na mauaji yalipoendelea zikageuka kuwa vurugu za kikabila kati ya vijana wa kikikuyu wakifadhiliwa na wanasiasa kutoka ukikuyuni wakiongozwa na uhuru kenyata aliekua akifadhili kundi la mungiki dhidi ya muungano wa makabila ya wajaluo wa nyanza na wakalenjini kutoka rift Valley wakifadhiliwa na William ruto kutoka Chama cha raila odinga cha odm kabla ya kuvurugana na ruto kuanzisha Chama chake baada ya vurugu kuisha

Kwa muktadha huo hapo juu, ruto na kenyata walishiriki kufadhili vurugu hizo Ingawa walikua vyama tofauti, ruto alikwenda kwenye media za kwao rift Valley na kuhubiri na kuhamasisha fujo kwa uwazi kabisa Bila woga, viongozi wa magenge hayo ya wauaji walijitokeza hadharani baadae na kuwataja wanasiasa waliokua wakiwafadhli akiwemo ruto na uhuru kenyata na wengine wengi

Sio kwamba akina odinga hawakushiriki bali ni Bahati yao tu jumba bovu halikuwaangukia

Kenyata alipoingia madarakani alihakikisha anawashughulikia mashahidi wote wa kesi yake, kwa kutumia vyombo vya upelelezi waliweza kuwabaini mashahidi karibu wote na tukaanza kusikia vifo vya mashahidi kwa kasi ya ajabu, hivyo mwishoni fatoe bensouda akashindwa kujenga strong case dhidi ya kenyata, sababu mashahidi wengi walipotea ktk mazingira ya kutatanisha na wengine wengi kujitoa kwa vitisho vya serikali ya Kenya, maana ktk Hali ya kawaida huwezi kwenda kutoa ushahidi dhidi ya rais wako

Mnaopinga icc mpinge kwa sababu zingine zozote zile lakini sio suala la kenya, mashahidi wengi wa kesi hiyo walijiandikisha Muda mrefu nyuma kabla hata kenyata hajaonyesha nia ya urais ndio maana hawakua na woga, lakini uhuru alipotwaa madaraka mashahidi wengi walijitoa kwa hofu, wengine kupotea na maiti zao kuokotwa baadae
 
vinara vurugu zile ni raila na kibaki, ruto na uhuru walifanywa mbuz wa kafara tu, baada ya
maridhiano ilikuwa ni lazima kuhadaa umma kwa kushitaki wanasiasa wakuu na wakawaida ndo kila upande ukatoa mtu. kibaki ilimtoa uhuru na raila akamtoa ruto afu wao kibaki na raila wakaunda serikali ya mseto
 
sisi raia wa kawaida tunaunga mkono tu mambo mengi bila hata kujua faida yake nini. viongozi wengi wa kisiasa wanaipinga mahakama hii hasa kwa kuwa wanajua kwamba wanatawala vibaya. Kiufupi hatufikirii kiundani faida za ICC kwetu sisi akina yakhe
 
ICC inatumika na nchi maarufu kwa jina eti 'firstworld' kututawala kwa njia ya ukoloni mamboleo.Walipokubali Mh. Emilio Mwai wa Kibaki na Mh. Raila Amolo Odinga,kutuliza misimamo yao mikali. Wengine nao walikuwa kwenye mikakati ya kujaribu kutuchagulia sisi wakenya rais wetu atakayetawala serikali kipindi cha serikali ya muungano kikiisha.Si ajab kuwa rais wetu wa sasa na makamu wake wamejipata wakijitetea ICC!Si ajab pia kuwa 'puppet' wa nchi hizo za magharibi aliyepigiwa hesabu hizo zote Mh. Raila Amolo Odinga alikataliwa na wakenya!Mungu aendelee kuongoza na kuibariki nchi yake ya Kenya,AMINA!
 
vinara vurugu zile ni raila na kibaki, ruto na uhuru walifanywa mbuz wa kafara tu, baada ya
maridhiano ilikuwa ni lazima kuhadaa umma kwa kushitaki wanasiasa wakuu na wakawaida ndo kila upande ukatoa mtu. kibaki ilimtoa uhuru na raila akamtoa ruto afu wao kibaki na raila wakaunda serikali ya mseto

Duh! Kaka kwa Watanzania wote humu, wewe ndiye umeonekana kuelewa issue ya hapa kwetu Kenya na sokomoko la ICC kwa undani. Umeiweka jinsi ilivyo bila kuchakachua, ndio ukweli huo japo wengi huwa tunahangaika kuuficha, ila utafichuka siku moja.

Inafaa ieleweke wazi kwamba Ruto na Uhuru hawakua wagombezi kwenye huo uchaguzi, na machafuko yaliisha pale kibaki na Raila walikubali kugawana madaraka baada ya kuburuzana kwa damu. ICC ningewakubali kama wangefanya kweli na kuwatuhumu hao wawili, lakini walichokifanya ni kuja huku na kucheza siasa. Wakakubali kupokea "ushahidi" na "mashahidi" walio andaliwa kwa hali ya kimafia kabisa.
 
Back
Top Bottom