Maige na ukisaajabu ya Musa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maige na ukisaajabu ya Musa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by petrol, May 28, 2012.

 1. p

  petrol JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Soma habari hii kutoka Tanzania Daima ndiyo utagundua Watanzania bado tungali na safari ndefu kufikia azma ya maisha bora kwa kila mmoja wetu.[TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]

  Wazee 380 waapa kuhama na Maige  na Ahmed Makongo, Kahama

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  ZAIDI ya wazee 380 wa kata za Segese, Shilela na Mega katika Jimbo la Msalala wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, wamesema wapo tayari kuhamia chama chochote atakachokwenda mbunge wao Ezekiel Maige.
  Kauli ya wazee hao imekuja wiki chache baada ya mbunge huyo aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kuondolewa kwenye wadhifa huo na Rais Jakaya Kikwete baada ya kuandamwa na tuhuma kwenye wizara yake zilizoanzia bungeni.
  Tamko la wazee hao lilitolewa juzi kwenye kikao cha pamoja na mbunge huyo kilichofanyika usiku katika Kijiji cha Segese kwa ajili ya kumpa pole baada ya kuondolewa kwenye uwaziri.
  Bila kujali itikadi za vyama vyao, walisema iwapo Maige atakihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) alichopo sasa, wapo tayari kuondoka naye.
  “Sisi tupo tayari kumfuata kokote aendako kwa sababu tunamfahamu uadilifu wake na ni mchapakazi mzuri na mwana maendeleo, kwa hili sisi wazee tunasema tutahama na wewe kwenda popote,” lilisema tamko la wazee hao lilitolewa kwa maandishi.
  Mzee aliyefahamika kwa jina la Lugiko, alisema Maige ni mwakilishi wao tangu mwaka 2005 hivyo wanajua faida yake hususan kwenye elimu, afya na miundombinu ya barabara hasa zile korofi.
  Kwa upande wake, Maige aliwatuliza wazee hao na kusema kuwa yupo pamoja nao katika kipindi hiki cha mpito, na kuwaomba wasibabaike wala kusikiliza maneno ya watu aliodai wanamchafua.
  Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamisi Mgeja aliyesema ipo haja ya uongozi wa chama hicho wilayani hapa kutembea kila kata ili kukutana na wananchi na kuwatuliza kutokana na mbunge wao kuondolewa kwenye uwaziri.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Naomba ee Mwenyezi Mungu uwasamehe makosa wazee hawa kama ulivyonisamehe mimi, maana ni vilaza hawajui wasemalo. AMEEEN!
   
 3. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Hakuna tena ada za vitalu sasa sijui atatoa wapi milioni mia tano za kupeleka jimboni
   
 4. MANI

  MANI Platinum Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Hapo sasa!
   
 5. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama wazee ni halali yao kusema hivyo kwasababu akili yao nayo ni ya kizee pia na huku ukiichanganya na pombe za kienyeji basi utaproduce matapishi.
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Aliwahi kusema amemwaga misaada ya karibu Mil. 500, sasa unafikiri hao wazee wataelewa. Na hakuna kuhamia Chadema, ni sumu hiyo hata kwa maziwa ya mbwa haitoki!!!
   
 7. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,277
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  wazee wanatumika vibaya jamani.mtu anaandaa pilau na lubisi then anawaita wazee.wakishakula na kunywa,utasikia sisi tunakuunga mkono asilimia mia.mhh!
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,375
  Likes Received: 19,640
  Trophy Points: 280
  keshawachomea nyama hao watasema nini tena?
   
 9. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Wazee hao wanadhihirisha ubinafsi wa wanaccm, wamepewa mahela yaliyochotwa na Maige maliasili, wameridhika na kuona uwaziri wake ni haki yake ya kikatiba, kwamba hauwezi kuny'ang'anywa. Kuvuliwa uwaziri ndio uhame chama, kwani kama yeye ndio mtetezi wao wa kweli, si ataendelea kuwatetea akiwa mbunge wa jimbo lake kupitia CCM chama mnachokiamini? Acheni kuweweseka magamba.
   
Loading...