๐——๐—ž๐—ง. ๐— ๐—ช๐—œ๐—š๐—จ๐—Ÿ๐—จ: ๐— ๐—”๐—–๐—›๐—œ๐— ๐—•๐—ข ๐—ฌ๐—”๐—ฆ๐—œ๐—ž๐—”๐—ง๐—œ๐—ฆ๐—›๐—˜ ๐— ๐—”๐—ฆ๐—ข๐— ๐—ข

๐——๐—ž๐—ง. ๐— ๐—ช๐—œ๐—š๐—จ๐—Ÿ๐—จ: ๐— ๐—”๐—–๐—›๐—œ๐— ๐—•๐—ข ๐—ฌ๐—”๐—ฆ๐—œ๐—ž๐—”๐—ง๐—œ๐—ฆ๐—›๐—˜ ๐— ๐—”๐—ฆ๐—ข๐— ๐—ข

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
681
Reaction score
444
๐——๐—ž๐—ง. ๐— ๐—ช๐—œ๐—š๐—จ๐—Ÿ๐—จ: ๐— ๐—”๐—–๐—›๐—œ๐— ๐—•๐—ข ๐—ฌ๐—”๐—ฆ๐—œ๐—ž๐—”๐—ง๐—œ๐—ฆ๐—›๐—˜ ๐— ๐—”๐—ฆ๐—ข๐— ๐—ข

โ–ช ๐—”๐˜€๐—ถ๐—บ๐˜‚๐—น๐—ถ๐—ฎ ๐—บ๐—ฐ๐—ต๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐—บ๐˜„๐—ฎ๐—น๐—ถ๐—บ๐˜‚ ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐—ฒ ๐—ธ๐˜‚๐—บ๐—ฟ๐˜‚๐—ฑ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐˜€๐—ต๐˜‚๐—น๐—ฒ๐—ป๐—ถ
โ–ช ๐—”๐—ฎ๐—ด๐—ถ๐˜‡๐—ฎ ๐˜‚๐˜€๐—ฎ๐—ป๐—ถ๐—ณ๐˜‚ ๐˜„๐—ฎ ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ ๐˜‡๐—ฎ ๐—ธ๐—ถ๐—ฝ๐—ฎ๐˜‚๐—บ๐—ฏ๐—ฒ๐—น๐—ฒ ๐—ฆ๐—ต๐—ถ๐—ป๐˜†๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ฎ ๐˜‚๐—ธ๐—ฎ๐—บ๐—ถ๐—น๐—ถ๐˜€๐—ต๐˜„๐—ฒ

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanahitimisha masomo na kuwasihi wanafunzi wasikatishe masomo kwa sababu ya uchimbaji madini.

โ€œTusiache kuwapeleka shule watoto kwa sababu ya aina ya shughuli tunayofanya leo,โ€ amesema, akisisitiza kuwa elimu itawawezesha kuendelea kujipatia kipato hata baada ya machimbo kuisha.

Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo (Jumatano, Novemba 11, 2026), akizungumza na wananchi katika viwanja vya Segese, Jimbo la Msalala, wilayani Kahama, ambako amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Shinyanga.

Wito huo umefuatia maelezo ya Mbunge wa Msalala, Mabula Johnson Magangila, kuwa baadhi ya wanafunzi wanakatisha masomo na kwenda machimboni, wakiwemo wanaofaulu kwa daraja la kwanza na kuchaguliwa kuendelea na masomo.

Akisimulia maisha yake ya utotoni, Waziri Mkuu amesema alipenda kuchunga mifugo na alikuwa mgumu kupelekwa shule. Hata hivyo, mwalimu wake aliendelea kumshawishi baba yake amrudishe shuleni.

โ€œTuletee yule kijana alikuwa na akili mno. Tuletee aende shule,โ€ amesema, akinukuu maneno ya mwalimu wake.

Amesema elimu itawawezesha vijana kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo biashara ya madini ndani na nje ya nchi.

Aidha, amesema Serikali imepokea ombi la kuanzishwa kwa kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam itakayotoa mafunzo ya madini Msalala na italifanyia kazi.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu amemwelekeza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Ntuli Mwaikokesye, kukamilisha usanifu na maandalizi mengine ya kitaalamu ya barabara za kipaumbele zilizotajwa Msalala, Ushetu na Kishapu, ili ziwe tayari Serikali itakapoanza kutekeleza miradi mipya.

Ametoa maelekezo hayo baada ya Magangila kuomba ujenzi wa barabara itakayorahisisha safari za wananchi kwenda Isaka, ambako kuna bandari kavu na reli ya kisasa (SGR).

Waziri Mkuu amesema kipaumbele ni ujenzi wa barabara zinazofungua maeneo ya uzalishaji.

Kwa mujibu wa Magangila, ujenzi wa barabara ya Kahamaโ€“Kakola umeanza kupunguza gharama za usafiri. Nauli kutoka Kahama hadi Segese imeshuka kutoka shilingi 5,000 hadi 3,000, huku ile ya Kahama hadi Kakola ikishuka kutoka shilingi 7,000 hadi 5,000.
 

Attachments

  • IMG-20261111-WA0238.jpg
    IMG-20261111-WA0238.jpg
    274.9 KB · Views: 1
  • IMG-20261111-WA0235.jpg
    IMG-20261111-WA0235.jpg
    298.1 KB · Views: 1
  • IMG-20261111-WA0228.jpg
    IMG-20261111-WA0228.jpg
    102 KB · Views: 1
  • IMG-20261111-WA0237.jpg
    IMG-20261111-WA0237.jpg
    325 KB · Views: 1
  • IMG-20261111-WA0233.jpg
    IMG-20261111-WA0233.jpg
    265.3 KB · Views: 1
  • IMG-20261111-WA0236.jpg
    IMG-20261111-WA0236.jpg
    314.7 KB · Views: 1
  • IMG-20261111-WA0241.jpg
    IMG-20261111-WA0241.jpg
    350.1 KB · Views: 1
  • IMG-20261111-WA0234.jpg
    IMG-20261111-WA0234.jpg
    290.9 KB · Views: 1
  • IMG-20261111-WA0239.jpg
    IMG-20261111-WA0239.jpg
    372.7 KB · Views: 1
  • IMG-20261111-WA0230.jpg
    IMG-20261111-WA0230.jpg
    198.8 KB · Views: 1
  • IMG-20261111-WA0242.jpg
    IMG-20261111-WA0242.jpg
    398.9 KB · Views: 1
  • IMG-20261111-WA0231.jpg
    IMG-20261111-WA0231.jpg
    207.2 KB · Views: 1
  • IMG-20261111-WA0229.jpg
    IMG-20261111-WA0229.jpg
    169.4 KB · Views: 1
  • IMG-20261111-WA0232.jpg
    IMG-20261111-WA0232.jpg
    255.3 KB · Views: 1
  • IMG-20261111-WA0240.jpg
    IMG-20261111-WA0240.jpg
    335.5 KB · Views: 1
Back
Top Bottom