INANIPA FARAJA KUCHUKIWA NA KUSEMWA VIBAYA NA WAOVU( wezi na watumiaji vibaya wa rasilimali na dhamana za uongozi walizopewa). HII INANIFANYA NISONGE MBELE KUWATETEA WANYONGE NA MASIKINI WA NCHI YANGU DHIDI YA UNYANG'AU WA MAFISADI HAWA!
Huwa inauma na mafunzo kusema vibaya na wazalendo na wanyonge wenzangu, na imekuwa ni mafundisho mazuri kwangu. Lakini nikisemwa na mafisadi, wezi, watumiaji vibaya wa rasilimali za nchi, tena kwa kuumia tu kisa mirija yao imekatwa, kwangu ni faraja kubwa kwani inaonyesha vita dhidi ya matumizi ya rasilimali za nchi yetu inaenda vizuri na imekamata pazuri!
SITAKATA TAMAA, NITASONGA MBELE MPAKA TONE LA MWISHO LA DAMU YANGU. NCHI KWANZA VYAMA BAADAE!