kambagasa
JF-Expert Member
- Aug 18, 2014
- 2,271
- 1,810
Katika hali inayoonyesha kutotakiwa tena na wananchi katika jimbo la Msalala, mbunge anayemaliza muda wake Mh. Ezekiel Maige leo amenusurika kichapo toka kwa wananchi wa Kakola maeneo ya Mgodini mara tu alipotaka kuanza kuhutubia.
Maige aliyeambatana na wanamziki kama gia ya kuvutia watu alifika Kakola na kuruhusu wanamziki wa kizazi kipya kutumbuiza, watu walipokusanyika ndipo akapanda jukwaani kuhutubia na zomea zomea ikaanza ghafla.
Kichekesho ni wanachama wa chama cha CCM wakaanza kukimbia na kutawanyika ovyo huko wanakokimbilia nao wakaanza kufukuzwa na wanamabadiliko. Polisi wakaogezwa kutoka kituo cha polisi Bugarama ndipo Maige akakimbilia kwenye gari lake na kutokomea huku gari la polisi likiwa nyuma yake.
Kumbukeni Kakola ndipo ulipo mgodi mkubwa wa dhahabu Bulyanhulu ila hakuna maji wala barabara ya lami.