Maige afichua siri nzito maliasili

Anasema kuna wakubwa kuliko yeye Waziri wa wizara nani hao?Kama wapo ni remote control wa wizara?Alijua lini kuwa yeye ni Paper Tiger tu? Hatua gani alichukua?Je kwanini hakufikiria kujiuzulu kabla ya kutakiwa afanye hivyo na Bunge ?Je kujitetea katika vyombo vya habari kunatamfanya arudie uwaziri wa Mali asili wakati tiyari JK ameishaapisha waziri mwingine ? Mbunge Maige wewe gangana na kazi yako ya kuwakilisha jimbo lako.
 
Yaah. Nakubaliana naye lakini isije ikawa ni kwa nia mbaya kuyaelezea yote haya bungeni. Ayafanye yote haya kwa nia ya kurekebisha palipo pabovu ili raslimali za Taifa hili ziyanufaishe makundi yote ya jamii

Mwaka huu watamalizana sana.
Yetu macho na masikio.
 
Maige ni MSANII SANA.If he was active? angekuja na list of shame ya wizara hiyo na kuomba aungwe mkono kuwafikisha maakamani.Hiyo wizara ina ubadhirifu na ufisadi toka enzi ya Zakia Megji.Huyu Kagasheki anapaswa kwanza kuanika wale wote waliokula hiyo wizara na wafikishwe maakamani.
Serekali hii bwana watu hula na wakishutuhiwa hupumzisha na kukabidhi mlaji mwingine KIJIKO.
 
Kama naibu waziri na waziri kamili Je anajua ktk kipindi cha uongozi wao DEGE LA FALME ZA KIARABU TENA LA JESHI lilitua TANZANIA na kuchukua mali zetu, Je anajua kua ndani ya mbuga kuna eneo kubwa linalomilikiwa na familia moja ya kifalme tena wamejenga mpaka ikulu yao ndogo analifahamu hilo? Je anajua wazungu na waarabu waliopewa hayo maeneo wamewahamisha wamasai tena kwa kuwachomea nyumba zao? Nini kifanyike kwako mtuhumiwa MAIGE ni kuyaweka wazi haya masuala ni nani aliehidhinisha kutoloshwa kwa wanyama wetu wakiwa hai? Nani aliegawa eneo la kufuru kwa familia ya kifalme ya uarabuni? na mengineyo hupaswi kujifananisha na YESU kwani yeye alitetea haki na hakuogopa dola iliyokuepo sasa wewe hiyo haki unaiteteaje kwa kuficha ukweli?
 
Kama aliyafanya hayo Mazuri hapo Wizarani kwanini hakuyatangaza kwa kuita Waandishi wa Habari na kuyajadili? Nani angejua aliyoyafanya? Angalia ya Nyumba yake hata kama alipata Mkopo kihalali ilibandikwa Magazetini na Rais aliona walakini au alikuwa anawaogopa hao Vigogo?

Na hao Vigogo ni akina nani kwanini asiwataje kwa Majina? na wao wakubali au kukanusha? kwanini kuwaficha na ametupwa Uwaziri? Kama Anasema kweli mbele ya dini yake, ni bora kuwataja hao Vigogo itusaidie sisi wananchi. Tujue Mali za nchi yetu nani anazidokoa na kuzipeleka Nje kwa Manufaa ya hao walafi wachache?

Tumechoka na kuambiwa vitu kimafumbo na kuficha ficha; Kama wewe ni Mkweli sema yote
 
Kila utumishi una mwanzo na mwisho, Maige tambua kuwa muda ulifika nawe upumzike ama kwa shari ama kwa heri. Yote tisa, siasa na utumishi si vita ni njia tu tunapita ili tufanikishe safari ya kuishi hapa duniani kwa heri na fanaka kama alivyotupangia mola. Yalaiti, ingekuwa tunapenda kila kitu kiwe kama tutakavyo basi nawe usingefikwa na haya. Ni mamalaka na wadhifa vina kuja na kuyeyuka kama theluji.
Kaa, tafakari, jisahihishe kama uliteleza sehemu fulani. Ongeza moyo wa ujasiri na bidii ya kufanikisha nia yako ya utumishi uliotukuka kwa watanzania kwa kufuata misingi bora ya haki, usawa na uwajibikaji. Hakika utafanikiwa, SIASA si baba yako na nina hakika akili alizokujalia mola hazikukuelekeza tu uwe mwanasiasa ili utimize jukumu la kuishi hapa duniani alilokupangia mola wako.
Ndoto za ufalme ni dhana ya wanyonyaji nami nina imani we si mmoja wao...........
Wakatabahu,
 
hata maamuzi yake ya kununua nyumba ya $ 700,000 kwa familia yake nayo anasemaje? Bado ni majungu? Mwizi tu kama wezi wengine, hana namna, hakusign document za kuruhusu tembo wetu waibiwe? Mfa maji .... Kama ana malori mawili yanayomuingizia $ 20,000 per months, wenge la nini?


kutemwa uwaziri: Maige afichua siri *mwanasheria ajipanga kuchukua hatua *kuanika uozo wa maliasili bungeni



na salim nyomolelo

aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii, bw. Ezekiel maige, amefichua siri nzito zilizochangia kung'olewa katika wizara mojawapo ikiwa ni kugusa maslahi vigogo wenye nguvu kubwa na ushawishi wa hali ya juu.

Bw. Maige ilifichua siri hiyo jana kupitia ujumbe wake alioutoa kwenye mtandao wa kijamii.

Aliongeza kuwa maamuzi aliyokuwa akiyatoa wakati akiwa waziri wa wizara hiyo alijua fika kuwa hayawafurahishi vigogo hao.

"kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu... Ni ngumu kukabiliala na wabaya. Wapo waliojipanga ukiwavamia hovyo hovyo unaondoka wewe," alisema bw. Maige na kuongeza; "ndivyo ilivyotokea."

alisema maamuzi yake aliyokuwa akisimamia ndiyo yamemfanya yamfike yaliyotokea. Alisema akiwa wizarani alisimamia sheria na kuwapa vitalu watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza.

"ni waziri gani aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina kamrani na wenzake? Watu wametumia records (kumbukumbu) za matukio ya mwaka 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya maige ya 2011," alisema bw. Maige na kuongeza;"yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi.

Niliwaomba wenzangu wamwogope mungu...bado nasisisitiza hivyo."alihoji kuwa; "ni waziri gani aliyefunga biashara ya wanyamahai, ni waziri gani aliyeonesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Lakini mimi sikusita kuchukua hatua."

alisema anawahakikishia wazalendo kuwa wamepoteza mpambanaji aliyejitolea kupambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini ndani na nje ya nchi.

Bw. Maige alisema alitumia kila aina ya uwezo wake kuzawadia taifa lake utumishi uliotukuka.

Alisisitiza kuwa maamuzi hayo magumu yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa. "nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda," alisema bw. Maige akinukuu maneno aliyowahi kuyatamka bungeni na kuongeza;"watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini muda haukuruhusu, ila nitarudi bungeni na nitasema."

kuhusu sakata la nyumba alisema suala hilo amelifafanua na kutoa vielelezo. "kila mbunge aliyetaka alikopeshwa sh. Milioni 290, wengine wameanzisha biashara na wengine wamenununua magari na wengine majumba," alisema.

Alisema mwenye mashaka aende kwa msajili wa hati wizara ya ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au crdb tawi la azikiwe na dodoma alikokopa au amtafute muuzaji.

Alisema maeneo yote hayo atapata rekodi ya bei. "wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei tofauti na niliyonunulia...mwanasheria wangu anashughulikia suala hilo," alisema bw. Maige.

Kwa upande wa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (cag), bw. Maige alisema haikumgusa, kwani ilikuwa inaishia juni 2010, wakati yeye alipewa dhamana ya kuongoza wizara hiyo novemba 2010.

Kuhusu biashara ya wanyamahai, bw. Maige alisema hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wa uongozi wake mwaka 2011 na kuwa matukio ya utoroshaji yalipobainika, walifungua mashitaka kwa watuhumiwa na kufunga biashara hiyo.

Aliahidi kuwawakilisha wananchi wa jimbo lake la msalala kwa mujibu wa katiba na ahadi zake kwao atazitekeleza hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo. Bw. Maige kabla ya kuteuliwa kuwa waziri kamili wa wizara hiyo mwaka 2010, alikuwa naibu waziri akiwa chini ya bi. Shamsa mwangunga.
 
KUTEMWA UWAZIRI: Maige afichua siri *Mwanasheria ajipanga kuchukua hatua *Kuanika uozo wa Maliasili bungeni



Na Salim Nyomolelo

ALIYEKUWA Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige, amefichua siri nzito zilizochangia kung'olewa katika wizara mojawapo ikiwa ni kugusa maslahi vigogo wenye nguvu kubwa na ushawishi wa hali ya juu.

Bw. Maige ilifichua siri hiyo jana kupitia ujumbe wake alioutoa kwenye mtandao wa kijamii.

Aliongeza kuwa maamuzi aliyokuwa akiyatoa wakati akiwa waziri wa wizara hiyo alijua fika kuwa hayawafurahishi vigogo hao.

"Kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu... ni ngumu kukabiliala na wabaya. Wapo waliojipanga ukiwavamia hovyo hovyo unaondoka wewe," alisema Bw. Maige na kuongeza; "Ndivyo ilivyotokea."

Alisema maamuzi yake aliyokuwa akisimamia ndiyo yamemfanya yamfike yaliyotokea. Alisema akiwa wizarani alisimamia sheria na kuwapa vitalu Watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza.

"Ni Waziri gani aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu wametumia records (kumbukumbu) za matukio ya mwaka 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya Maige ya 2011," alisema Bw. Maige na kuongeza;"Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi.

Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu...bado nasisisitiza hivyo."Alihoji kuwa; "NI waziri gani aliyefunga biashara ya wanyamahai, ni waziri gani aliyeonesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Lakini mimi sikusita kuchukua hatua."

Alisema anawahakikishia wazalendo kuwa wamepoteza mpambanaji aliyejitolea kupambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini ndani na nje ya nchi.

Bw. Maige alisema alitumia kila aina ya uwezo wake kuzawadia taifa lake utumishi uliotukuka.

Alisisitiza kuwa maamuzi hayo magumu yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa. "Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda," alisema Bw. Maige akinukuu maneno aliyowahi kuyatamka Bungeni na kuongeza;"Watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini muda haukuruhusu, ila nitarudi bungeni na nitasema."

Kuhusu sakata la nyumba alisema suala hilo amelifafanua na kutoa vielelezo. "Kila mbunge aliyetaka alikopeshwa sh. milioni 290, wengine wameanzisha biashara na wengine wamenununua magari na wengine majumba," alisema.

Alisema mwenye mashaka aende kwa Msajili wa Hati Wizara ya Ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au CRDB tawi la Azikiwe na Dodoma alikokopa au amtafute muuzaji.

Alisema maeneo yote hayo atapata rekodi ya bei. "Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei tofauti na niliyonunulia...mwanasheria wangu anashughulikia suala hilo," alisema Bw. Maige.

Kwa upande wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Maige alisema haikumgusa, kwani ilikuwa inaishia Juni 2010, wakati yeye alipewa dhamana ya kuongoza wizara hiyo Novemba 2010.

Kuhusu biashara ya wanyamahai, Bw. Maige alisema hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wa uongozi wake mwaka 2011 na kuwa matukio ya utoroshaji yalipobainika, walifungua mashitaka kwa watuhumiwa na kufunga biashara hiyo.

Aliahidi kuwawakilisha wananchi wa Jimbo lake la Msalala kwa mujibu wa katiba na ahadi zake kwao atazitekeleza hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo. Bw. Maige kabla ya kuteuliwa kuwa waziri kamili wa wizara hiyo mwaka 2010, alikuwa naibu waziri akiwa chini ya Bi. Shamsa Mwangunga.

Kaka nilipenda sana ujumbe wa Maige kwa kuwa inaonesha ni jinsi gani watu wema wanaonekana maadui huku waovu wakifanywa washindi. tunamuombea tu heri na ajitahidi sana kusimamia kweli ili awe Huru kweli. Hujuma iliyompata inaonesha udhalimu wa chama chake na jinsi wanavyoangamiza taifa letu. naye aone kilele za wapinzani siyo za uongo bali ni hali halisi inayofanya na ccm. naamini moyoni atakuwa anatamani kuona yale ya moyoni yakiwafikia wananchi kuhusu uozo unaofanya na serikali aliyokuwa miongoni mwa viongozi. Mungu ni mwema na ndo aliyekufanya upate hiyo nafasi ya kushuhudia mambo hayo na hayo yakawe ukombozi wa watu wake. Ni mpango wa Mungu ulokupa nafasi hiyo na akataka ukainjilishe watu wake wanaoangamia kwa kukosa macho na maarifa na kuchagua viongozi wanaoangamiza kizazi cha sasa na kijacho. Usiwe na moyo mgumu, wewe ni sawa na Yonna aliyetumwa Linawi akataka kutotoroka, kini Mungu mwenye nguvu alisababisha dhuduba liyomfanya Yona atoswe baharini kuokoa maisha ya abiria wengine. Hivyo Linawi yako ni Tanzania inayozama kwa umaskini, matumizi mabaya ya rasilimali, wizi,ufisadi,uonevu,uongozi ulojaa kila aina ya dhuluma na mambo mengi ya kufedhehesha, kawaambie wananchi wafunguke na uwape ujumbe Mungu anaotaka watu wake wakolewe na rasilimali zako. Utakuwa mkuu wa wakuu baadaye.Mungu akubariki na akutie nguvu na ujasiri ili ukatende aliyokutuma kuwaambia watanzania wote kuwa serikali ya ccm ni janga na ni kansa ya maisha ya sasa na ya baadae.
 
Back
Top Bottom