hivi kwanini siku hizi watu uanza mahusiano ktk umri mdogo ata kutenda tendo la ndoa.?tofauti na enzi za mababu zetu?
Sababu hasa ni urahisi wa kupatikana nyenzo za kujenga uhusiano na utendaji wa ngono.
Watoto wa siku hizi wana nafasi nzuri ya kujua nini ngono kwani wana nyenzo nyingi za kuwafundisha kiasi hata tunadai kuwa elimu hiyo ifunzwe shuleni.
Watoto wa siku hizi wanafunzwa mapema kujitayarisha kwa mahusiano na matendo ya ngono kwa njia tofauti ikiwa pamoja na mavazi na mapambo.
Watoto wa siku hizi wanafundishwa kuwa ili uwe maarufu basi uwe tofauti na maadili yanayoitwa yaliyopitwa na wakati.
Watoto wa siku hizi wanaachiwa faragha ya kutosha kwa jinsia mbili kumaliza maumbile kwani hakuna linalofuata panapo faragha kati ya mwanamke na mwanamume zaidi ya kufuatia tendo la ndowa.