Mahusiano,Mapenzi na Ndoa na Bibi yangu wa Kitangile

Mahusiano,Mapenzi na Ndoa na Bibi yangu wa Kitangile

Sodoku Myebusi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2016
Posts
1,320
Reaction score
3,009
Juzi usiku iitokea nikiwa nmezama kwenye kina kirefu sana cha mawazo nikamkumbuka Bibi yangu Ndembule miaka ile nmeenda mkoani kutoa taarifa nmepata mchumba.

Nakumbuka alikuwa amekaa kivulini kwenye mkeka akisuka mkeka mwingine.pamoja na kuwa na miaka zaidi ya 90 bibi yangu hakupenda kukaa hivi hivi. Bado alitaka afanye kazi. Nakumbuka alikuwa anagombana sana na akina mama wanampatia mfanyakazi lakini bibi bado anataka aamke asubuhi sana afanye kazi za usafi n.k na lengo la akina mama ni kuwa awe analala achelewe kuamka na asifanye kazi. Bibi alikuwa anagoma kabisa.

Siku hiyo alikaa chini ya mti amenyoosha miguu yake anasuka mkeka. Nilikuwa nmetoka kupata breakfast ndani ya chai ya maziwa na viazi.nmeshiba sana. Nikamfuata nikakaa mkekani.nikamwambia "bibi nmepata mchumba nataka mwaka huu kuoa" bibi aliendelea kuwa ameinama akisuka mkeka wake.nikahis pengine hajasikia nikamwambia tena kwa sauti ya juu kidogo. Akameza fundo la mate akanyoosha mkono wake akachukua maji yaliyokuwa yanakaa pembeni kwenye jagi akanywa.nikahisi sasa amemeza maeno nliyomwambia.

Akasema kwa upole" haya baba nmekusikia, pole sana" nikashtuka kidogo kwa nini pole badala ya hongera.

Akaanza kuongea akiwa ameinama anasuka mkeka wake. "Baba siku hizi mnapooa tunajua mnaenda kuish pamoja kama vile mume na mume badala ya mume na mke.mnataka haki sawa, mnashindana ndani ya nyumba, wote mnataka wote vichwa. Bibi akaendelea kuelezea mambo ya kwenye ndoa za kisasa. Hazina uvumilivu wanawake wengi wamekuwa hawana upendo, wanaume wamekuwa wababaishaji.

Ndoa zimekuwa hazina upendo,uvumilivu na busara kutumika.si kwa watoto tu hata wazaz wamekuwa na mchango hasi kwa ndoa za watoto wao" bibi aliongea mengi sana. Akaanza kunitia moyo pia kuwa nisimwaibishe.

Ilitokea tu nikamkumbuka na ni miaka kadhaa imepita toka anambia maneno hayo. Alifariki mwaka jana lakin maneno yake yanaishi. Mtizamo wake katika mahusiano, mapenz na ndoa ulikuwa ni wenye kukatishwa tamaa hasa kwa kizaz chetu hiki. Babu yangu alifariki miaka ya 80s mwishoni.kipind hicho alikuwa na wake watatu ambao wote walimweshimu na kumpenda sana. Sisi tumekumbwa na nini na ndoa zetu?
 
kwani siku hizi kuna ndoa mkuu?..mi naona kuna harusi..kwenda kuishi pamoja..kuzaa watoto..kulea...basi
watu hawafuati misingi ya ndoa now
 
Dah wakuu x
Sasa kama hakuna ndoa nami nataka niingie huko. Mbona mwanikatisha tamaa xna
Usikate Tamaa bado wazuri wenye kuheshimu na kujua maana ya ndoa nini,chamsingi mtangulize sana mwenyezi mungu kwenye kila jambo lako....
 
Back
Top Bottom