Kwa hiyo ndo kusema manesi wanaongoza kwa uzinzi?
Labda alishawahi kufanya yeye, na ndivyo hivyo vyumba vinavyotumika anaongea kwa kua yeye ni mzoefu....
Si kweli sio wote wako hivyo.
Aiseee. .
Sasa wanafanya na nani? Wanaitisha hawara zao hosp?
Na Vipi madaktari? Au ndo wana-pair na manesi?
Wana jf, katika professional za watu na mahusiano nimekutana na kikao cha watu wakijadili hiyo mada. Wanasema kuwa wanawake wanaofanya kazi ya uuguzi(manesi) ni rahisi sana kutoka nje ya ndoa zao kulingana na nature ya kazi yao. Kuna mama mmoja naye ni nesi kwenye hospitali mojawapo ya mkoa hapa Tanzania alikuwa anawaambia wanakikao hao kuwa katika ile hospitali manesi wote wa kike walioko pale wanafanya kile kitendo kwenye vile vyumba vilivyomo wodini kwa ajili ya kupumzikia. Eti mara nyingi hufanya hvyo usiku. Kwa kweli nilivyosikia hvyo ikabidi niwaletee wadau humu tuijadili kama haya mambo yanatokea kweli au huyu mama alikuwa anawasingizia.
Kuna point moja alisema, kwa wale wenye mahawara, akishafika kazini kwenye zile night zao huongea na mlinzi amruhusu hawara yake kwa kumpatia kitu kidogo mlizi. Wapo pia wanaofanya hvyo na madaktari humo humo kwenye vyumba vyao kwa kufanya mpango na manesi wenzao walipo zamu nao.
Aiseeeee.
Sasa hapo ni uchungu wa kulupia gesti au ni mkakati wa kuokoa muda?
Mkuu hii mada yako tunaweza kuiunganisha na ile mada ya kufanya kazi za shift usiku (Night) ambazo kimsingi, haziwahusu manesi tu, ila wafanyakazi walio wengi ambao wana ratiba za namna hiyo. Tulishajadili kuwa night shift nyingi huwatega watu, na hata kuwafanya baadhi ya wafanyakazi huzitumia nafasi hizo kufanya mambo ya uzinzi.
Ningependa kuichambua mada yako kwa mapana, lakini nahisi naweza kuwabore baadhi ya watu; ila niungane na wewe kwa kusema kuwa manesi wanatupiwa lawama zaidi kwa hayo matendo pia kutokana na nature ya kazi ya kuhudumia (kuwashika, kuwachoma sindano, kuwavalisha pampas walio mahututi, kutoa dawa, wound dressing hata zilizo sehemu nyeti) wagonjwa wa jinsi zote na hivyo huenda kisaikolojia kuwafanya washiriki kwenye mahusiano bila woga sana.
Lakini si manesi tu, pia wapo madaktari, walimu wa shule za msingi (sijui hawa kama nature ya kazi inahusika vipi?), masekretari (sijui wanalazimishwa na mabosi?), wanajeshi (sijui wanabanwa na amri za kijeshi), nk ambao pia wamelalamikiwa na kuhisiwa na jamii kwa kutoka nje ya ndoa kwa kiwango kikubwa zaidi.
Hivyo kwa sehemu, hoja hii inaweza kuwa na ukweli, ila tabia za individual employees zina sehemu kubwa zaidi ya kutokuwa waaminifu kuliko nature ya kazi wanazofanya.
Aiseeeee.
Sasa hapo ni uchungu wa kulupia gesti au ni mkakati wa kuokoa muda?
Wewe ni nesi?
Enheeeee!!