Makau Js
Member
- May 25, 2017
- 93
- 233
Single Mother Part One.
TBTG-Mtandao wa , www.singlemotherguide.com unaonyesha ya kuwa duniani kuna akina mama wanao lea watoto bila baba zao Milion 9,781,000 ambayo ni sawa na 83.0% na kuna idadi ya akina baba Milion 2,033,000 ambao wanalea watoto bila mama zao ambao ni sawa na 17 %.
Tanzania , kizazi hiki kina ongezeko kubwa sana la mabinti wengi kupata watoto na kulea bila baba wa mtoto,kuna sababu nyingi ambazo zinasababisha ulezi wa mama kulea mtoto pasipo baba mtoto .
Ukosefu wa uaminifu,uvumilivu ,uadilifu na uhaba wa pesa ni moja ya sababu kubwa ambazo zimejeruhi ndoa nyingi na mauhusiano mengi sana ,nchini Tanzania na dunia kwa ujumla.
Kama wewe ni binti uliyezaa kabla ya ndoa na unahitaji kupata mwenza/mume ambaye si baba watoto wako ni vyema ukaanza kumuomba Mwenyezi -Mungu akupe hekima na busara ili uweze tambua mwanaume mwenye mapenzi ya dhati atakayekupenda wewe pamoja na mwanao bila kubagua na kuweka mizani ya mapenzi na upendo kwako wewe na mwanao bila upendeleo.
Usipofanya maamuzi sahihi utatengeneza ndoa ambayo ,mwanaume atakupenda na kukutamani wewe na kutomjali mtoto wako,ukaingia kwenye ndoa ambayo itakupa furaha wewe na kumpa mtoto simanzi kwa kutopewa mapenzi bora na kuwekewa ukuta wa upendo wa baba mpya .
Binti mwenye mtoto ambaye unahitaji kuolewa jifunze kuvaa vazi la uaminifu, uadilifu nidhamu na heshima njema kwa jamii inayokuzunguka na kuwa na haiba bora .
Tengeneza sifa njema ili kufunika tatizo la kwanza na hakikisha unakuwa mkweli na mwenye dhamira ya dhati ,huku ukiwa umefuta mambo ya kale na kuingia ukurasa mpya ukiwa msafi wa mwili na tabia.
A single mother needs a heart of steel, even if it is full of love and care. So yes, you are one who are strong, not just one who is struggling.[HASHTAG]#SingleMother[/HASHTAG].
Itaendelea ..................