Mahujaji wa DRC wazuiliwa kwenda Makka kuhiji sababu ya Ebola

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
ebola_QT1_14331.jpg

NCHI ya Saudi Arabia imegoma kutoa hati ya kusafiria ‘Viza’ kwa mahujaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ikihofia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imesema uamuzi huo umefikiwa baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza kwamba nchi ya DRC ina mlipuko wa Ebola.
Wizara hiyo imesema hatua hiyo ya kuzuia watu kutoka DRC kuhiji Makka ni kulinda usalama wa mahujaji kutoka katika mataifa mengine.

Imamu Djuma Twaha, Kiongozi wa Waislamu nchini DRC amesema watu 410 nchini humo walipanga kwenda kuhiji mjini Makka mwezi huu.
 
ebola_QT1_14331.jpg

NCHI ya Saudi Arabia imegoma kutoa hati ya kusafiria ‘Viza’ kwa mahujaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ikihofia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Wizara hiyo imesema hatua hiyo ya kuzuia watu kutoka DRC kuhiji Makka ni kulinda usalama wa mahujaji kutoka katika mataifa mengine.

Imamu Djuma Twaha, Kiongozi wa Waislamu nchini DRC amesema watu 410 nchini humo walipanga kwenda kuhiji mjini Makka mwezi huu.
SAHIYH KABISA HAPO NI UAMUZI SAHIHI NA NI WA BUSARA
NI KTK KUJALI MAISHA YA MAMILIONI YA WATU.
TUNGESHAURI PIA HUKU TZ ICHUKUE TAHADHARI KWA WANAOTOKEA CONGO KWA KUFANYIA KAZI REPORT YA W.H.O
 
Back
Top Bottom