Mi nionavyo mafisadi wamejitoa mhanga kulifundisha somo la uzalendo kwa wasio nacho. Ila tu wanalivutia pumzi hilo somo, muda si muda watu wataungana ili kuwashughulikia hawa viongozi wa siasa wanaotumikia mafisadi badala ya wananchi walowachagua.
Tanzania siyo kisiwa, na upepo unaovuma duniani dhidhi ya hawa mamumiani, hatuwezi kuukwepa sisi kwa nchi, na wananchi bahati nzuri wamekwisha jua ni nani mwanga wao. Hatabaki salama, baada ya hapo Tz yenye wazalendo ambao hawako radhi kubadilishana neti za mbu kwa mapande ya dhahabu watazaliwa na kuishi kati yetu.
Its a matter of time!
Kutegemea elimu ya darasani, ambako mwalimu amekopwa mshahara wake pamoja na marupurupu yake, na mshahara wenyewe ni wa ku-beep mahitaji yake yakiwemo yale ya msing -chakula na maradhi; tusitegemee sana huko. Turuhusu hali iliyopo ichukuwe mkondo wake tu, ndo mwisho wa ubabaishaji