Konzo Ikweta
JF-Expert Member
- Oct 3, 2013
- 766
- 1,532
Siku hizi watu wanaenda kwenye ibada ili wafanikiwe kwenye maisha yao hapa Duniani,
Wahubiri nao wamesha liona hilo,ukihubiri mafanikio ya hapa Duniani ndio unapata waumini wengi na sadaka zinaongezeka,
Ni issue ya Demand and Supply tu,
Maisha yamebadilika,dini zimekua kama biashara za watu.
Matajiri wengi huwa wako sharp kutambua utapeli
Wengine pia hufuata muujiza. Kumbuka wapenda miujiza wengi ni wale wenye vipato duni.
Mfano:
Tajiri kwa kuwa anajimudu kiuchumi, akipata hata homa tu anakimbilia hospitalini kufanya checkup na hata akipatwa na gonjwa zito, anakuwa na pesa za kwenda kutibiwa popote duniani mfano India n.k.
Masikini akipatwa hata na homa, cha kwanza anajua karogwa, atapita kwa waganga wa kienyeji, na baada ya kushindikana kwa ugonjwa wake, anakimbilia kwa watoa muujiza ya uponyaji.
Hapo ndipo atanunuzwa madongo, maji n.k
Kwenye Biblia Kuna mstari unasema hivi, "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"Unashauri nini Mkuu?
Wapo wanaoenda tu kusali sio kuomba utajiri maana utajiri tayari wanao upo tuMatajiri wengi huwa wako sharp kutambua utapeli