Kwa msabato, mkazo wa kwanza ni kuwa kama waberoya. Waberoya walikuwa watu waliokuwa wakichunguza kile walichofundishwa kama kinaendana na Biblia kweli, au ni mawazo ya mtu tu. Na ukiona msabato kafanya ujinga (kama wale wa kutaka kwenda Israeli kuhubiri bila viza Wala passport) basi ujue akili alimkabidhi mhubiri.
Kuwajua waberoya soma aya zifuatazo.
Matendo ya Mitume 17:10-11
[10]Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi.
[11]Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.
Sasa wewe endelea kuhubiriwa na ukubaliane na mhubiri bila kuhunguza kama anachohubiri kinaendana na neno la Mungu tuone unaishia wapi kwenye mambo ya Imani.