"Mahojiano yetu ni ya Divisheni 5" By Edo Kumwembe

"Mahojiano yetu ni ya Divisheni 5" By Edo Kumwembe

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,934
Na edo kumwembe

BADO Napata wakati mgumu. Nafungua magazeti ya Ulaya nayasoma huku natabasamu. Halafu
baadaye nafungua magazeti ya nyumbani huku nakunja sura. Na hasa linapokuja suala la mahojiano. Unasoma kwa makini kauli ya mtu unayemuheshimu.

Ukimaliza unakunja sura. Unatamani kupata namba yake ya simu umepigie na kumuuliza kama kweli ni
yeye ndiye aliyeongea au wamemnukuu vibaya. Unakosa namba yake. Lakini siku zinapita mwenyewe hakanushi. Unajua kweli aliongea. Kiurahisi tu hivi karibuni nilisoma sehemu Mwenyekiti wa Yanga akizungumzia kuhusu Frank Domayo kwenda Yanga.

Nilitamani kuamini kuwa alikaririwa vibaya. Alisema Kuna akina Domayo wengi Kariakoo wanapatikana. Mwache aende tu baadaye atarudi mwenyewe Yanga. Hapo hapo unajiuliza kama nafasi hiyo angekuwa anaikalia Ed Woodward wa Manchester United au Florentino Perez wa Real Madrid angeweza kusema Domayo ni mmoja kati ya viungo bora nchini.

Ni pigo kwetu na ni faida kwa Azam, lakini tutakuwa makini kutafuta mbadala wake. Tunamtakia kila la
kheri huko aendako kwa sababu ameitumikia vema klabu yetu kwa miaka mitatu iliyopita. Nakumbuka Juni mwaka juzi wakati wa mapumziko wa mechi ya Ivory Coast na Tanzania uwanja wa Felix Houphouet-boigny nilimfuata Yaya Toure ambaye hakucheza mechi hiyo kumuuliza kuhusu kiwango cha Taifa Stars.

Alinijibu kwa upole Timu yenu ni nzuri na mnapiga pasi za haraka. Tatizo dogo nililoliona ni kuwa wachezaji wenu hawana nguvu sana. mna wachezaji wowote wanaocheza Ulaya? Najaribu kuvuta picha kama Yaya Toure angekuwa Mtanzania, halafu timu yake ya Tanzania ni kama Ivory Coast. Naweza kujibu ambacho angesema. Lazima angesema Hamna wachezaji nyinyi.

Bado hamna uwezo kabisa. Kwanza hamjawahi kushiriki kombe la dunia. Unamfuata kocha wa timu kubwa kabisa. Unamuuliza unaionaje Yanga na pambano lenu dhidi yao wiki ijayo. Kocha anajibu Yanga ni kama mti wa uani. Nikirudi nyumbani napopoa tu nakula. Yaani Yanga ni kama mapambo ya Jeneza tu. Anayesema hivi ni kocha wa kulipwa ambaye maisha yake yanategemea soka. Lakini kama Yanga
ingekuwa inacheza na Manchester United, Sir Alex Ferguson angejibu kwa umakini mkubwa
huku akiwaangalia waandishi usoni.

Tunaiheshimu Yanga kwa kiasi kikubwa. Navutiwa na viungo wao na itabidi tuongeze umakini katika eneo hilo ikiwemo kumdhibiti zaidi Haruna Niyonzima. Huyu ni Ferguson ambaye ametwaa mataji ya mawili ya Ulaya. Ametwaa mataji kibao ya Ligi Kuu ya England. Anaheshimika duniani kote. Lakini hapotezi heshima kwa timu yoyote anayocheza nayo.

Amiss Tambwe amefunga mabao 19 msimu ulioisha. Ni mmoja kati ya washambuliaji hatari kwa kuziona nyavu ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati. Lakini niliwahi kumsikia kocha mmoja akiulizwa vipi kuhusuTambwe katika pambano lao linalofuata.

Alijibu kwa haraka haraka Bwana Kitenge, Tambwe ni mviziaji tu, lakini nakwambia njoo uwanja wa Taifa kesho uone shughuli atakayokumbana nayo.

Kama kungekuwa na shule kichwani kwake, au upeo mzuri wa kawaida angeweza kujibu Tambwe ni mmoja kati ya wafungaji tishio nchini na wote tunafahamu hilo. Ni mfungaji wa mfano sana na katika timu yetu
tunamuheshimu sana.

Lakini nadhani tumejiandaa kupambana vizuri na Simba kwa ujumla na sio Tambwe peke yake. Tutajitahidi
kupata pointi tatu kesho. Hakuna unachoweza kufanya zaidi ya kucheka tu. Tatizo ni shule au upeo wa kawaida?

Rafiki yangu Gaudence Mwaikimba zamani alikuwa anamtungua kip Juma Kaseja mara nyingi wakutanapo. Hata alipohamia Azam hadithi iliendelea kuwa hiyo hiyo. Lakini siku moja na yeye akapata bahati ya kuhojiwa kuhusu hilo.

Nikasoma katika gazeti. Kaseja hanisumbui kabisa. Yaani nitamfunga ninavyotaka popote pale tukikutana.
Hapo hapo unakumbuka mahojiano ya Wayne Rooney wakati alipoulizwa ni kwa nini amekuwa akiifunga Arsenal mara kwa mara tangu akiwa Everton mpaka Manchester United.

Alijibu kwa umakini huku akijikuna nywele zake. Nadhani ni bahati tu. Mara nyingi inatokea tu kuwa Napata nafasi nzuri na kufunga. Lakini leo nataka kuipongeza timu yetu yote. Tumecheza kwa umakini mkubwa katika mechi hii dhidi ya Arsenal na tumepata pointi tatu muhimu.

Hawa ndio wenzetu. Wachezaji kama akina Wayne Rooney hawajaenda shule sana. alikuwa na muda gani wa kusoma wakati alisaini mkataba wake wa kucheza soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 15? Tangu hapo ni soka na yeye, yeye na soka.

Nilipokuwa msemaji wa Coastal Union, kitu cha kwanza nilikuwa napenda kuiheshimu timu pinzani. Utashindaje mechi bila ya kujua ubora au udhaifu wa timu pinzani? Unaziponda Simba, Yanga na Azam zenye Domayo, Kipre Tchetche, Tambwe, Niyonzima na wengineo, unamdanganya nani zaidi ya kuwadanganya wachezaji wako?
 
Napata taabu na hawa waandishi wetu.

Napata hisia kwamba hawawezi kujisikia wamebobea bila ya kusifu timu za nje na kuziponda za hapa kwetu, hasa Simba na Yanga. Kauli ni hisia ya mtu kutoka moyoni mwake. Huwezi kulazimisha mtu aongee maoni yako wewe eti tu kwa sababu unajidanganya kwamba wewe ni mwandishi bingwa. Hata huko Ulaya kwenyewe kuna wabwabwajaji kama au hata kuliko Manji na Mwaikimba.

Nani hamjui Mourinho? Balotelli? Hata Ferguson amgshawahi kuadhibiwa kwa kuwalaumu waamuzi baada ya kushindwa kwa timu yake. Simeone aliingia uwanjani kwenye mechi muhimu ya fainali ya mabingwa wa Ulaya. Tumesikia mwandishi gani mahiri wa michezo akimsulubu kwa lawama? Sijui mwandishi huyu angesem
 
Napata taabu na hawa waandishi wetu. Napata hisia kwamba hawawezi kujisikia wamebobea bila ya kusifu timu za nje na kuziponda za hapa kwetu, hasa Simba na Yanga. Kauli ni hisia ya mtu kutoka moyoni mwake. Huwezi kulazimisha mtu aongee maoni yako wewe eti tu kwa sababu unajidanganya kwamba wewe ni mwandishi bingwa. Hata huko Ulaya kwenyewe kuna wabwabwajaji kama au hata kuliko Manji na Mwaikimba. Nani hamjui Mourinho? Balotelli? Hata Ferguson amgshawahi kuadhibiwa kwa kuwalaumu waamuzi baada ya kushindwa kwa timu yake. Simeone aliingia uwanjani kwenye mechi muhimu ya fainali ya mabingwa wa Ulaya. Tumesikia mwandishi gani mahiri wa michezo akimsulubu kwa lawama? Sijui mwandishi huyu angesemaje laiti jambo lile lingefanywa na Minziro kwenye mechi ya Lgi Uwanja wa Taifa. Ubaya hauna kwao, ndivyo wazee wetu walivyotuambia. Ni vyema wanaojidhani wana haki ya kulaumu wenzao bila ya wao kulaumiwa wakaamini hivyo. Njia mojawapo ya waandishi mabingwa kulaani wanachohisi kuwa ni kasoro ama aibu ni kutoliripoti kwenye vyombo vyao.
 
Napata taabu na hawa waandishi wetu. Napata hisia kwamba hawawezi kujisikia wamebobea bila ya kusifu timu za nje na kuziponda za hapa kwetu, hasa Simba na Yanga.

Kauli ni hisia ya mtu kutoka moyoni mwake. Huwezi kulazimisha mtu aongee maoni yako wewe eti tu kwa sababu unajidanganya kwamba wewe ni mwandishi bingwa. Hata huko Ulaya kwenyewe kuna wabwabwajaji kama au hata kuliko Manji na Mwaikimba. Nani hamjui Mourinho? Balotelli?

Hata Ferguson amgshawahi kuadhibiwa kwa kuwalaumu waamuzi baada ya kushindwa kwa timu yake. Simeone aliingia uwanjani kwenye mechi muhimu ya fainali ya mabingwa wa Ulaya. Tumesikia mwandishi gani mahiri wa michezo akimsulubu kwa lawama? Sijui mwandishi huyu angesemaje laiti jambo lile lingefanywa na Minziro kwenye mechi ya Lgi Uwanja wa Taifa. Ubaya hauna kwao, ndivyo wazee wetu walivyotuambia.

Ni vyema wanaojidhani wana haki ya kulaumu wenzao bila ya wao kulaumiwa wakaamini hivyo. Njia mojawapo ya waandishi mabingwa kulaani wanachohisi kuwa ni kasoro ama aibu ni kutoliripoti kwenye vyombo vyao.
 
Napata taabu na hawa waandishi wetu. Napata hisia kwamba hawawezi kujisikia wamebobea bila ya kusifu timu za nje na kuziponda za hapa kwetu, hasa Simba na Yanga. Kauli ni hisia ya mtu kutoka moyoni mwake. Huwezi kulazimisha mtu aongee maoni yako wewe eti tu kwa sababu unajidanganya kwamba wewe ni mwandishi bingwa. Hata huko Ulaya kwenyewe kuna wabwabwajaji kama au hata kuliko Manji na Mwaikimba. Nani hamjui Mourinho? Balotelli? Hata Ferguson amgshawahi kuadhibiwa kwa kuwalaumu waamuzi baada ya kushindwa kwa timu yake. Simeone aliingia uwanjani kwenye mechi muhimu ya fainali ya mabingwa wa Ulaya. Tumesikia mwandishi gani mahiri wa michezo akimsulubu kwa lawama? Sijui mwandishi huyu angesem

Hapa ndipo tunapokwama Waafrika, hatuwezi kufikiri kwa namna yetu bila kuwa na rejea kutoka kwa hao mabwana wakubwa.

Kuhusu alichokiandika Edo, kwanza ifahamike kuwa wazungu ni watu wanafiki kuliko wote duniani, kama wao wanasifiana sisi hatuna haja ya kusifiana pia. Makocha na wachezaji wetu wana namna yao ya kujieleza na jinsi wanavyoona Soka, zaidi ya hayo lugha wanayotumia nayo ina mikogo yake ambayo haifanani na ya lugha ingine yoyote.
 
Hapa ndipo tunapokwama Waafrika, hatuwezi kufikiri kwa namna yetu bila kuwa na rejea kutoka kwa hao mabwana wakubwa.

Kuhusu alichokiandika Edo, kwanza ifahamike kuwa wazungu ni watu wanafiki kuliko wote duniani, kama wao wanasifiana sisi hatuna haja ya kusifiana pia. Makocha na wachezaji wetu wana namna yao ya kujieleza na jinsi wanavyoona Soka, zaidi ya hayo lugha wanayotumia nayo ina mikogo yake ambayo haifanani na ya lugha ingine yoyote.
Acheni ujinga nyinyi, ivi Yahya Ture ni mzungu? Alichokisema Edo ni chakweli ambacho ainabudi watanzania tujifunze. Maana kwenye kubwabwaja hata wanasiasa nao wamo kwenye kundí hili.
 
kuna kitu Eddo anasahau...hao akina rooney ni pros na akina mwaikimba amateurs....akina rooney hawana shule ya darasa na chuo cha kawaida ila wana shule ya mpira...wanafundishwa nini cha kuongea,wapi na muda gani akina mwaikimba hawana shule yoyote ile....ukiwasikiliza wachezaji wa ulaya wakihojiwa wengi wana mtiririko sawa kwa ulaya ukimponda mpinzani ni sawa na kumpa motivation hivyo utajipa mwenyewe wakati mgumu and vice versa...its more psycological na wanajua hilo.
 
Mimi nashangaa badala ya kujadili maudhui mnaanza kumshambulia EDDO, mimi nadhani EDDO amezungumzia ufahamu wa viongozi wetu makocha na wachezaji ni kweli ukisikiliza interview zao zinatia kichefuchefu badala ya kuzungumza kwa uweledi analeta mzaha mifano ni mingi tu angalia jinsi afisa habari wa mtibwa tobias kifaru anavyojikita kutaka kuzungumzia mambo ya ufundi uwanjani utadhani yeye ni sehemu ya benchi la ufundi na si yeye tu ni karibu wote kabisa wanafanya hivyo.

Pia waandishi wetu nao hovyo kabisa unakuta anafanya interview na mwenyekiti au katibu wa club anamuuliza maswali ya kiufundi badala ya kumtafuta kocha bado tuna udhaifu mkubwa sana kwenye hili.
 
Edo amesema ukweli mtupu,hatuna tabia ya kuheshimu timu/wachezaji pinzani ni kubwabwaja tu ni misifa isiyo kweli,pia waandishi wetu hawajui kuuliza maswali ya msingi....wajifunze.
 
Hapa ndipo tunapokwama Waafrika, hatuwezi kufikiri kwa namna yetu bila kuwa na rejea kutoka kwa hao mabwana wakubwa.

Kuhusu alichokiandika Edo, kwanza ifahamike kuwa wazungu ni watu wanafiki kuliko wote duniani, kama wao wanasifiana sisi hatuna haja ya kusifiana pia. Makocha na wachezaji wetu wana namna yao ya kujieleza na jinsi wanavyoona Soka, zaidi ya hayo lugha wanayotumia nayo ina mikogo yake ambayo haifanani na ya lugha ingine yoyote.

Iliked your comment because in a way it complements my earlier views to the letter. Kama waandishi wana haki ya kujieleza kw kutumia lugha na mikogo yao, haki hiyohiyo ndiyo ambayo kina Manji na Julio wanayo. Wanapoitumia isiwe nongwa! Au kwa sababu wao sio Wazungu?
 
Hiyo divisheni 5 umetupendelea sana inaweza discussions zetu hapa nyingi ni level ya -1000. Kuanzia jinsi tunavyoandika grammar za Kiswahili hadi tunavyojibu maswali. Unaweza kusema mtu hajamaliza hata darasa la tano. Sio viongozi wetu tu haya mambo yapo hapa JF pia. Inasikitisha jinsi tunavyoendekeza na kuhusudu ujinga(stupidity) kila kitu ni bora liende. Waandishi wetu wa habari nao ndo usiseme uandishi upo kijiweni sana, sijui walimu wa Kiswahili mashuleni wanafanya kazi gani. Ni aibu sana.
 
Dah, kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake. Hivi bado kuna mtu anaweza kuwa na guts za kupinga alichokiandika Edo?
Yaani kuheshimu mpinzani wako ni kitu kibaya?

Hakuna kocha yeyote professional anayeponda na kuikosea timu pinzani. Hata huyo Mourinho sio mwehu wa kiwango hico hebu fuatilieni vizuri comment zake kuhusiana na game. Hawezi kusema Liverpool ''ni sawa na mwembe wa uani''. Never kabisa, huu ni ujinga na tuukatae kwa pamoja
 
Unamuhoji Ngassa anakwambia tuombee dua tushnde! Hizo dua tunaomba kila siku na mbona tunafungwa tu?
 
mwanahabari ukiuliza maswali ya hovyo hovyo basi utajibiwa hovyo hivyo hivyo. jana baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Tanzania na Malawi mwandishi wa Azam tv alikwenda kumuhoji nahodha wa Malawi, swali alilouliza ni "how was the match? alipojibiwa akakosa kingine cha kuhoji akaishia kusema thank you
 
mmoja kati ya watu nnaowakubali hapa tanzania na ninamshukuru kwa kunipatia signature
 
mi sidhan kama kuwaza kwa namna wazungu wanavyowaza ndiyo sahihi..unasahu pia wakati mwingine jose mourhino huwa anatamka maneno ya kuudh au kebehi na watu wengine anampenda kwa hilo tu. hiyo yote ni sanaa ya lugha,ni tambo na maneno ya kumkatisha tamaa mpinzani wako au kumwathiri kisaikolojia. Muhamad ali mmoja ya mabondia wa kuheshimiwa dunian alishawa kumwita mpinzan wake nyani, alishawahi kumwambia mpinzani wake kuwa anapiga ngumi hafifu kuliko hata za mwanamke...hizo ni tambo katika michezo ambazo pia ni chachandu au kileta hamu katka mpira. si kwamba wazungu au waishio ulaya hawafanyi hivyo. nao hufanya sana tu. tatizo la ninyi badhi ya waandishi na waswahili mnadhani kwa kuiponda tanzania na watu wake mnaonensha namna gani mlivyo mahiri. huo ni ulimbukeni. wazungu ni binadamu kama sisi ...hatuna tofauti hata kidogo katika suala la hisia n.k mbona kuna makocha au husema wazi hata hapa tanzania kuwa mchezaji flan ni pengo? mbona Mbeya City walikataa mechezaji wao asiende team nyingine kwa kuwa ni tegemeo? si wangesema aende tu wapo wengi?tuache kila kitu kuwaza kwa mlengo wa kimagharib au nchi nyingine tukidhan kwa kuponda kila kitu cha kitanzania ndo tunaonesha umahiri wetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom