Mahojiano ya Maxence Melo, Clouds+

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,874
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo akihojiwa Clouds+ katika kipindi cha sebuleni

======

Katika mahojiano haya amejibu nadharia zilizopo.

Moja ya nadharia iliotolewa ufafanuzi ni kudhani kuwa Jamiiforums ipo 'against' serikali, nadharia hii, haina usahihi kwa kuwa hata kesi iliyotolewa hukumu Aprili 8, 2020 ilikuwa ni taasisi binafsi Oilcom na sio serikali

Pia kuhusu jamiiforums kutumia kesi ili kujipatia umaarufu swala ambalo limejibiwa kuwa, Jamiiforums inatoa uhuru wa raia(watumiaji) wa jamiiforums kutoa mawazo yao, na hata kesi iliyotolewa hukumu msingi wake upo katika serikali kutaka taarifa za mteja ambaye kwa wajibu wake kama mtanzania alikerwa na yaliyokuwa yanaendelea bandarini na akayafanyia 'whistle blowing' ndani ya jamiiforums

Mtu anapotoa kero ya jambo haimaanishi kuwa anatafuta umaarufu bali anatimiza wajibu kama raia mwema


 
Na nyinyi wananzengo tuache kuzingua humu, tunamchonganisha na mamlaka maana hapa kapigwa fine sina uhakika kama kuna member humu katoa hata buku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nanyinyi wananzengo tuache kuzingua humu,tunamchonganisha na mamlaka maana hapa kapigwa fine sina uhakika kama kuna member humu katoa hata buku.

Mkurugenzi hakutaka kutembeza bakuli, hata hivyo kama ulishawahi kufuga.... mbuzi wako wakila shamba kwa jirani utalipa wewe na sio mbuzi.
 
Muuliza maswali wa kwanza Melo amekujibu vizuri sana swali la kuikosoa Serikali
hahahhh alikuwa anataka kuonyesha kusifu na kuabudu.
 
Back
Top Bottom