Mahojiano JF: Mhe. Kagasheki azungumzia Matatizo ya Utendaji wa Balozi za Tanzania nchi za nje - #3

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
SWALI: Je, Balozi zetu nje zina Tija? Je! Matatizo ya utendaji kazi kwao ni nini?




(Katika maandishi kutokana na video hii)

Mabalozi ni jambo ambalo hatuwezi tukaliepuka, zipo na zitaendelea kuwepo ndo uwakilishi wa hizi nchi huko nje, ni kama vile unavyoona wabunge wanaowakilisha wananchi, lakini sasa ni nchi kupanga, wanataka waweke hizi balozi wapi na ni wapi wanaona patakuwa na manufaa zaidi kwao.

Zipo nchi nyingi tu ambazo wameamua kwamba labda tuweke ubalozi hapa na tusiweke, na wanatoa sababu na sababu nyingine ziko valid, balozi za Tanzania me niseme nyingi unakuta kwamba zina sababu na sababu ni nzuri, sababu za kimaendeleo , sababu za kuendeleza mahusiano kati ya taifa na taifa nk.

Lakini niseme tu kwamba kwa muda kwakweli sasa, hizi balozi zimekuwa kidogo ni tabu upande wa finance, upande wa kusurport staff kule, waweze kufanya kazi zao vizuri,unajua diplomasi unakutana na wenzako,wa nchi hii, nchi ile, lakini sasa kukutana si kukutana tu, mnakutana over coffee, mnakunywa kahawa, mnakutana over tea, mnakutana over lunch, kukutana kwenye reception, lakini sasa haiwezi nyie mnakwenda kwenye reception za wenzenu tu, unaalikwa lunch ni wewe, mnaalikwa chai ni wewe, wewe hutoi, yaani you don't receplocade, yaani huna, sasa of course ukipiga kelele huku, huku unajua na hali zenyewe. Kwa hiyo, hiyo hali kwa kweli ipo na wakati mwingine inawafanya wawakilishi wetu wanakuwa wanyonge hawawezi wakashiriki kama ambavyo wangeweza kushiriki kwa sababu wana limitation ya kuweza kuwawezesha katika kufanya kazi.

Lakini diplomasi ni muhimu inasaidia katika mambo mengi na ndio maana kwa mfano ile philosospy nzima ya tulivyosema tumemaliza liberation ya Afrika politically na kuona kwamba nchi nyingi sasa zimekuwa huru, sasa foreign policy ya Tanzania ifocus katika nini. Naturaly ilikuwa katika economic diplomacy, diplomacy ya kiuchumi ambayo itaweza sisi kutusaidia katika maendeleo yetu na kututoa hapa point A ya matatizo ya umasikini na tukaenda point B ambayo tunaweza kufanya.

Sasa wether hayo yanafanyika au hayafanyiki, nafikiri sasa hayo sasa evaluation watafanya wahusika huko, lakini hizi ofisi na fuction hizi ni muhimu, sasa kama zinafanyika kama inavyohitajika, kama tunapata the maximum benefit out of them kama inavyotarajiwa nafikiria hayo tena hayo ni maswala ambayo wanaweza wakayajua wengine tena.

Unajua swala hili ni gumu kidogo, kuna mabalozi wanajitahidi for the purposes ya kuona kwamba wanaweza kuleta vitu vya kuisaidia nchi hii, lakini sasa hawawezi wakafanya wenyewe, inabidi either kwa mfano, wafanye na wizara ya fedha, wafanye na wizara ya viwanda na biashara, wafanye na wizara ambayo inashughuikia maswala ya uwekezaji etc,ect.

Kwahiyo unakuta ni shughuli ambayo ina involve players wengi, coordination hiyo ya hao players hapa internally is a nightmare, ni tatizo hata ufuatiliaji unakuwa ni tatizo.

Of course me nilikuwa balozini, mnaweza mkaandika mabarua, yasijibiwe, balozi wanaweza wakaja hapa, unamkuta anatoa wizara hii anakwenda wizara hii anakwenda wizara hii anafuatilia, akishandoka ndo ameondoka na hilo limeondoka.

Kwa hiyo matatizo ni makubwa zaidi, mbali na uforeign, mbali na mabalozi lakini pia system,there is the systematic problem ambayo unaona kabisa maswala ya kuweza kufanya coordination iliyokuwa ni nzuri ya kuweza kufuatilia na kusema kwamba sisi tunafocus katika kupata,to get the maximum out of our diplomacy jinsi tunavyokwenda tuweze kupata yaani maximum tunaweza kupata,unaona kweli,

Hata Rais mwenyewe amekuwa anaisema, you could see,he speaks very well rais unaona kabisa hata emphasis yake lakini unamuona he is a loner ,he is a lone ranger you know,ukitizama yeye kashaongea,yeye kashasema anatakata tuende wapi amekwisha even point out.

Lakini sasa who picks some peaces picks from there raisi kweli kaongea,ametoa muongozo, ametoa direction nani sasa anayefuata kusema kwamba haya ya rais sasa tuyaweke sasa katika vitendo kwasababu yanainvolve kama nilivyosema wachezaji wengi, inainvolve wizara nyingi,inainvolve wanani sasa unawacordinate namna gani tofauti na nchi nyingine me I have seen diplomacy ya wahindi,nimeona diplomacy ya Algeria za hawa unaona kabisa kabisa ni diplomacy ya kupata kwa taifa lakini,sio kupata kama individuals kama watu binafsi lakini kupata kama taifa,kwahiyo hiyo unayosema bado sisi tutakua na kazi na shughuli ya kufanya ili tuweze kupata the maximum benefit kutoka katika diplomacy yetu hii.


*Zingatia hii ni swali la nne (4) katika orodha ya maswali yaliyojibiwa. Kwa taarifa zaidi tembelea
- https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...rview-ya-jamiiforums-na-khamis-kagasheki.html
 
Last edited by a moderator:
Mbona hakuna mtiririko? kila swali video yake.huwezi elewa mnachotaka tujue.weka video nzima tutazame,hii ya vipande vipande inaboa
 
Mkuu,

Ulalamishi katika kila jambo hasa kama hujalielewa vema, haipendezi.

Kwa hiyo wewe mtiririko ni kuweka video yote hapa? Haya ni mahojiano ya masaa sita (6). Inahusisha maswali 70+. Endapo una shida na video yote kwa pamoja tuma maombi hayo support@jamiiforums.com na utapewa utaratibu.

Kwa taarifa zaidi kwanini mahojiano ya video yamepangwa kama ilivyo sasa tembelea - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...rview-ya-jamiiforums-na-khamis-kagasheki.html

Mbona hakuna mtiririko? kila swali video yake.huwezi elewa mnachotaka tujue.weka video nzima tutazame,hii ya vipande vipande inaboa
 
Very well spoken Kagasheki.

Kuna wakati mabalozi wetu hadi wanatia huruma jinsi wakianza kujitetea kwa nini efforts zao hazizai matunda yanayostahili.Yani Tanzania ikija initiative kutoka nje watu wanawaza wao kama wao watafaidika vipi?kama hana chake basi atamuonea aibu balozi, akiondoka na hilo jambo ndio limeondoka.

Nimegundua over the years, mabalozi wanaopata mafanikio ni wale waliokuwa na pull huku nyumbani, mfano, aliwahi kuwa waziri au mtendaji mkuu wa sehemu nyeti, hivyo anauwezo wa kuweka uzito wa jina lake nyuma ya initiative. Lakini wale mabalozi wanaoteuliwa based on merit of their diplomatic abilities huwa frustrated nyumbani.

Ingetakiwa kuwa katika baraza letu la mawaziri kuwe na at least asilimia 30 ya watu wenye significant foreign experience. This would help a lot in moving the country forward, for there is no replacement for proper exposure at the highest level of government. Hizi ziara za mafunzo za wiki moja 2 hazihesabiki, kwani wengi huja na kuondoka wakiwa kwenye bubble flani hivi.
 
Mkuu,

Ulalamishi katika kila jambo hasa kama hujalielewa vema, haipendezi.

Kwa hiyo wewe mtiririko ni kuweka video yote hapa? Haya ni mahojiano ya masaa sita (6). Inahusisha maswali 70+. Endapo una shida na video yote kwa pamoja tuma maombi hayo support@jamiiforums.com na utapewa utaratibu.

Kwa taarifa zaidi kwanini mahojiano ya video yamepangwa kama ilivyo sasa tembelea - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...rview-ya-jamiiforums-na-khamis-kagasheki.html


Kuna watu msipoteze nao muda, binadamu hawaridhiki, mngeweka video ya masaa 6 hapa kuna wangelalamika ndefu sana.

Pleasing everyone is the surest way to not achieving anything. The quality of the videos is fantastic. I have an idea regarding this initiative. You may already have such in the works, but shouldn't hurt airing it out.
We need JF TV.
You may partner and sell your content with one of the local broadcasting houses, or TV topbox companies, to have JF TV there.

Then curated and up to date content that if quality focused and based on superior research and top notch questions and interviews may be compressed for public consumption.

Kwa hiyo, kama mkiwa na StarTV kipindi kitaitwa Kutoka Mitandaoni/JF(just rhetorical name). Na mada zitajikita kwenye ku-air mambo mazito yanayojadiliwa JF na majibu un-interupted kwa general audience.

My only pledge is, please stick to value adding politicians not empty noise makers, with no substance and shady credibility. In a few years, Getting interviewed by JF will be an honor politicians vie for.and only the very best of them should get the chance
 
Nafungua huku nafungua kweli but I see nothing,anyway kwa kuwa mmeridhika kwamba walengwa wenu wamefikiwa ni sawa,sie wengine tutasubiri magazeti yakianza kuandika make tunaweza shauri na kuongea mengi tukaishia kulimwa ban
 
tatizo nikiwakosoa mtanifungia, ngoja nikae kimya......

Nafungua huku nafungua kweli but I see nothing,anyway kwa kuwa mmeridhika kwamba walengwa wenu wamefikiwa ni sawa,sie wengine tutasubiri magazeti yakianza kuandika make tunaweza shauri na kuongea mengi tukaishia kulimwa ban

Mpaka wamefungua jukwaa la malalamiko na ushauri na kuna watu wanaongoza kushinda kule sijawahi kuona wamepigwa ban, wanashaurika bana, mwageni mawazo yenu. Mimi nawaomba namba ya kwenye title iendane na swali lililomo ndani, kama kuna zilizokuwa combined sawa lakini likija jengine liandikwe namba sahihi kuliko kuruka.
 
Back
Top Bottom