Mahiza atetea sekondari za kata

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Serikali imesema haijashtushwa na matokeo mabaya ya shule za sekondari za kata na imewashangaa watu wanaozibeza shule hizo.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza, wakati wa uzinduzi wa harambee ya kuchangia elimu Wilaya ya Kisarawe, iliyoandaliwa na Fashion for Education Benefit.
Alisema serikali inaona changamoto ya shule hizo kuwa ni mafanikio makubwa kwake.
“Wakati tunaanza mpango wa kujenga shule zile tulijua kabisa ni vigumu kukamilisha kila kitu, maabara, nyumba za walimu na walimu wa kutosha, hivyo yanayosemwa juu ya shule hizo ni changamoto ya kusonga mbele,” alisema.
Alisema serikali imeweka mkakati wa kuziimarisha shule hizo ili zipate maabara, nyumba za walimu, vitabu vya kutosha, nyumba za walimu na walimu bora. Alisema wanaozibeza shule hizo hawajui watendalo kwani miaka michache ijayo angalau kila kata nchini itakuwa na wahitimu wa kidato cha nne.
“Hivi nyinyi mlitaka tuendelee na utaratibu wa kujenga shule moja moja tungefika hapa tulipofika angalau kwa sasa, hamuoni kwamba shule hizi zitawasaidia watu wengi wa kipato cha chini kwenda shule, tufanye wewe ndo ungekuwa Rais halafu asilimia 75 ya watoto wanaopaswa kwenda sekondari hawaendi ungejisikiaje? Tunaomba mtuunge mkono maana mpango huu ni ukombozi kwa watanzania jamani,” alisema.
Aliongeza kuwa shule hizo ndizo zitasaidia kwa kiwango kikubwa kuondoa tatizo la mimba za utotoni kwa kuwa wasichana wengi watakuwa shule. Alisema pia zitaondoa tatizo la wanaume kuoa vibinti vidogo kwani wazazi walio wengi watamudu kuwapeleka shule.
“Hata muendelee kuzipa majina ya aina gani, shule hizi zipo na zitaendelea kuwepo na ndizo mkombozi wenu kama hamfahamu,” alisema.
Jumla ya Shilingi bilioni 10 zinatarajiwa kupatikana katika harambee hiyo ya kuzichangia shule za sekondari za kata.
 
hii inasikitisha sana.....wote tunakubali kuwa lengo la shule hizi ni jema, lakini kweli kwa kiwango hiki cha kufeli kweli na matamshi ya namna hiyo, wapi na wapi!!!!linalojadiliwa hapa ni kuwa shule hizo zimekuwa kama makambi ya kuwakusanya watoto wasizagae mtaani badala ya lengo halisi la kuwapa elimu bora. sasa unategemea nini kwa nchi ambayo kiwango cha kufeli ni asilimia 70? yaani div 4 na 0 ni asilimia 70... what a joke... watoto hawa sasa wataishia mtaani tu wakiwa wamekosa kabisa hata elimu ya kujitegemea kwa badala ya muda huo wa miaka minne kukaa nyumbani at least kujifunza kupika, kufua,na mambo mengine ya kimisingi ambayo wote tunayafahamu wao walikuwa darasani wakipoteza muda.

tunahitaji kubadilika kifikra!!.
 
mahiza ni matunda ya siasa za kubebana za serikali ya AWAMU YA NNE.
mahiza daima anatoa kauli zenye kuonyesha kuwa yeye ni WAZIRI DHAIFU sana, aliwahi kunukuliwa akiwaambia walimu wa TANZANIA kuwa wanalipwa mishahara MIKUBWA, na kama kuna kwalimu anadhani mshahara huo ni mdogo aacha kazi naende kwenye sekta ambazo wao wanadhani zinalipa, kisha akawashauri wale walioko vyuoni kuacha kusomea kazi hiyo kama wanadhani mshahara wa walimu ni mdogo, mshahara aliokua akijivunia ni kati ya Tsh 197000 hadi 320000, bila allowance yoyote.
kweli kwa mazingira ya walimu yalivyo magumu zikudhani kama waziri wenye dhamana kwenye elimu angeweza kutoa kauli yenye utata kama hiyo, kauli ya kuvunja moyo.
kwa maelezo hayo nilimtarajia mahiza kuzisifu shule za kata, na kwake ni mafanikio kuwa vijana wetu wamefika KIDATO CHA NNNE , bila kujali wameelimika ama laah.
mimi naamini kama mfumo wa kugawana madaraka ya juu kitaifa utaendelea kuwa hivi, maisha ya watu wetu yatakua shakani, alaaniwe aliemteua kushika wadhifa mkuubwa hivyo kitaifa.
 
Back
Top Bottom