Mahitaji ya umeme yameongezeka

Mahitaji ya umeme yameongezeka

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
MAHITAJI YA UMEME YAMEONGEZEKA

Mahitaji ya juu ya umeme katika Gridi ya Taifa nchini yameendelea kuongezeka na kufikia Megawatt (MW) 1,921.44 zilizofikiwa tarehe 09 Aprili, 2025 saa 3:00 usiku ikilinganishwa na MW 1,590.10 zilizofikiwa tarehe 26 Machi, 2024 saa 3:00 usiku sawa na ongezeko la asilimia 20.84.

Ongezeko la mahutaji linatokana na jitihada za Serikali hususan kukuza uchumi wa nchi yetu kunakoambatana na mahitaji ya umeme, kuimarisha huduma za kijamii ambazo uendeshaji wake unahitaji umeme na kukua kwa sekta za viwanda na usafirishaji (treni ya SGR).

Aidha kumekuwa na ongezeko la matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuimarika kwa uunganishaji wa umeme kwa wananchi mijini na vijijini

Huo ni Utekelezaji wa bajeti ya serikali 2024/25 kwa Wizara ya Nishati eneo la Mahitaji ya Umeme.
 
View attachment 3321699
Na yanazidi kuongezeka
 
Umeme ni mdogo sana. Haufiki 220v unaishia 185-200v kitu ambacho kinatisababishia hasara. Kuna nchi hawaitaji stabilizer kwasababu umeme wao upo stable 98% ila kwetu ni changamoto sana. Hilo ongezeko linatokana na watu wengi kununua vifaa vya kustablize umeme na ups as backup kwahiyo hapo hakuna juhudi za serikali wala nini.
 
Back
Top Bottom