Mahitaji Manne ya Msingi yatakayosababisha kuwa na Afrika yenye viwanda ni kuanzisha viwanda vyema k

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
540
507



Na: Simon Ngusa Jilala
8/5/2016

Mahitaji Manne ya Msingi yatakayosababisha kuwa na Afrika yenye viwanda ni kuanzisha viwanda vyenye kuendesha viwanda vyote unavyodhani vipo hapa Duniani.

Katika kubishana kwa hoja lazima ujifunze na ujifunze kufuta wakati mwingine vile vitu ulivyokuwa navyo kichwani na kuingiza vipya kabisa visubiri kama kutakuwa na hoja nyingine mbadala itayosababisha kujifunza upya tena. Mimi nimejifunza kwa rafiki yangu mmoja anaitwa Joseph Mshinga alivyonieleza kwa undani kuwa mahitaji ya msingi kabisa ili kufikia kwenye viwanda vyote lazima kwanza muanze au muwe na viwanda vya aina tatu kama nilivyovitaja hapo chini, lakini cha msingi kabisa ni kuwa na UONGOZI WENYE MAONO HAYO. Ukiangalia katika Bara letu la Afrika utagundua nchi karibu zote haziwahi kufanya au kufikiria jambo hili hapa. Kama zipo ni chache mno naamini hata 5 hazifiki kama zimeshawahi kujaribu kujenga aina ya viwanda hivi;

1. Viwanda vya kutengeneza vyuma (Iron and steel Industries),
2. Viwanda vya kemikali (Chemical Industries),
3. Viwanda vya Kiuhandisi (Engineering Industries),
4. Viongozi bora na wenye maono (Good and visionaries leaders).

Ebu angali daraja la Kigamboni lilifunguliwa juzi na kuitwa Daraja la Nyerere. Katika daraja hilo na mengine kuna vyuma, kemimali, elimu ya uhandisi na kuna maono yaliyoanzishwa nyuma kuhusu hili jambo. Lakini ukiacha kiongozi na kugharamia pesa ya ujenzi wa daraja la NYERERE, vitu vingine vitatu vyote vilitojaka nje tena kwa bei ya juu kabisa tena nje ya Bara la Afrika. Na Mataifa hayo yalifaidika maradufu katika mradi wa daraja la Nyerere kwa sababu ndio wana viwanda hivyo hapo juu.

Hata Bahresa ili atengeneze Vinywaji vyake unafikiria anatoa wapi kemikali?, nje ya Afrika, Je, unadhani viwanda vyake vimejengwa na nani? Watu kutoka nje ya Afrika, Je na vyuma vyake vinatokea nje ya Bara la Afrika. Afrika tunahitaji AKILI KUBWA ZAIDI NA ZAIDI kuanza angalau kufikiria katika jambo hili, na tusiseme ni ngumu na hatuwezi. Najua tukianza kufikiria na kuanza kutenda taratibu kizazi kijacho angalau kitasema kuna watu wenye maono walikuwepo au waliishi Tanzania. Viwanda vya Vinywaji vyote vinategemea Mataifa ya nje KUSONGA mbele acha vya aina zingine.

Ebu angalia utengenezaji wa reli, Madaraja au viwanda vyote nchini kwetu Tanzania, Afrika na hata nje ya Afrika na angalia na mahitaji hayo hapo juu unaona nini?. Unaona nini ukiongelea au ukisikia kiongozi anaongelea nchi ya viwanda?.

Je, Magufuli anapoongea kuwa anataka Tanzania ya Viwanda Watanzania tunamwelewa?.

Kuna siku vizazi vijavyo vitaamka na kujua wazi kuwa; Taifa lisipowekeza zaidi katika viwanda vifuatavyo litazidi kuwa tegemezi miaka na miaka. Na kuna siku kuna vizazi vita acha kuwaza hayo bali vita fanya kwa matendo zaidi bila UOGA sijui wa ukoloni mambo leo na vitisho vya Mabwenyenye.

1.Iron and steel industries.

Ni viwanda vinavyotakiwa kuzalisha aina zote za chuma iwe ya kutengenezea aina zote chuma kama za vyuma vya reli,injini,viwanda,karakana,magari,pikipiki,baiskeli,vyuma vya madaraja nk. Kwa kifupi viwanda hivi vinapaswa kuhudumia mahitaji yote ya chuma na ni viwanda muhimu sana kwa kuwa viwanda vingine vyote haviwezi kuanzishwa bila chuma.

2.Chemical industries.

Hivi ni viwanda vinavyotumika kutengeneza na kuzalisha kemikali mbalimbali ikiwemo ya viwanda vya madawa ya binadamu, viwanda vya madawa ya mifugo, kiwanda cha madawa ya mimea katika kilimo, Viwanda mbolea. Viwanda vya kutengeneza kemikali za kutumika viwandani iwe kwenye viwanda vya mbalimbali vya kiuhandisi,viwanda vya viatu,viwanda vya simu,viwanda vya magari nk. Viwanda karibu vyote vinahitaji kemikali ili vizalishe bidhaa.

3.Viwanda vya kiuhandisi.

Engineering industries. Hapa utakutana na electronic infistries kama simu,saa,radio,tv, viwanda vya auto, kama kutengeneza magari,pikipiki,injini mbalimbali zinazotumiaka kwa mfano za magari,mashine,viwanda,meli nk.

Chunguzeni tangu tupate Uhuru nchi nyingi za Afrika; Viwanda karibu niseme vyote tulivyoanzisha sisi vyote vinategemea viwanda vya hapo iron and steel, chemichal na Engineering.

4. Viongozi bora na wenye maono ya mbali zaidi.

Tunahitaji viongozi ma jasiri Afrika ambao watatengenza njia ambazo vizazi vijavyo na si vya leo kuja kufaidika na urithi wa leo. Tunahitaji viongozi wenye maono ya mbali zaidi ili waanze kuwaza haya. Lakini pia wajue kuwa kuna mambo Afrika ilifanya kwa shinikizo kama kusaini mikataba ya misaada yenye masharti lukuki kama Structural Adjustment Policy (1980's). Tunahitaji wajue kuwa tuko Dunia gani na tunaelekea wapi.
 
Back
Top Bottom