Mahindi ya Njaa Igunga yameipa CCM ushindi wa kura 2400 zaidi ya CHADEMA

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
27,667
30,115
Wakuu,

Nimesikitishwa sana na kitendo cha serikali yetu kuisaidia CCM kuipa ushindi kwa kugawa mahindi ya chakula igunga kwa kisingizio eti inasadia watu, wote tunajua njaa ni adui wa haki na hata mimi ningekuwa igunga ningemuheshimu sana mtu anayenipa uhai - mtu anayenipa uhakika wa kuiona kesho.

Lakini cha kujiuliza je kwa nini mahindi yagawiwe igunga tu? tena wakati wa kampeni?. Mimi ni mwenyeji wa Tabora, ndugu zangu Tabora kuna njaa sana karibia wilaya zote je kwa nini igunga pekee ndiyo ipate chakula?

Hizi njama za wazi wazi za serikali kuisaidia CCM kwenye chaguzi na ninaungana na wananchi wenzangu kupinga hatua hii ambayo inadhoofisha demokrasia nchini.

Kutumia njaa kuwashawishi wapiga kura ni rushwa na dhambi kwa mwenyezi mungu, sikatai kugawa msosi lakini wakati wa kampeni? ndiyo maana tunasema hii Tume ya uchaguzi si tume ya taifa ila ni tume ya kuhakikisha CCM inashinda chaguzi.

Mpira gani usio na Refa? Mpira gani usio na sheria, taratibu na udhibiti? uonevu huu utaisha lini ndugu zangu? sisi sote ni watanzania tunahitaji haki, je utapataje haki kama vitui hivi vinaendelea nje nje tena bila kificho, woga wala aibu?
 

THINKINGBEING

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
2,778
1,303
Mahindi ya njaa pia yameipa ccm ushindi wa udiwani monduli kata ya engutoto.
Huu utaratibu wa kugawa chakula maeneo yenye chaguzi ni wakuangaliwa upya.
 

mama kubwa

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,090
7,820
waendelee kuwagawia mahindi maana ubaya wa njaa bora tumbo lizoee kukosa au kupata kidogo lakini huu mwezi walizoea kujichana vikiisha itakuwa balaa mpaka tena 2015.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom