Mahindi ya kuchoma ni bora kuliko pop corn

hiram

JF-Expert Member
Aug 1, 2013
266
393
wanajamvi mnaonaje watanzania tukaanzisha utamaduni wa kuingia kwenye kumbi za sinema kama pale Quality Centre na mahindi ya kuchoma badala ya pop corn. unajua mahindi ya kuchoma ni fresh kutoka shamba kuliko mahindi ya pop corn yamekaaa weee ndo yanakuja kukaangwa, awepo mchoma mahindi pale nje unanunua hindi lako unatafuna punje moja moja huku unacheki movie kama tunavyootaga moto kule kwa bibi na kusimuliana hadithi. Hizi tamaduni za kizungu ni za kibwege sana, kuna siku nimenunua pop corn za sukari zikanishinda kula. mi nasema wazungu waje waingie movie na mahindi wapate cha kusimulia
download (1).jpg
download.jpg
 
Tatizo, ni kwamba wabongo wengi wanajifanya wa kishua ila huku wakitafuna popcorn kitanzania tanzania sana na.kulimaliza kopo zima kabla ya dakika 5 za movie au mpira kuanza.

Ila wazo hilo, ni bomba sana ili kuendeleza asili na vitu vyetu japo kidogo tu!
 
unajua mahindi ya kuchoma ni fresh kutoka shamba kuliko mahindi ya pop corn yamekaaa weee ndo yanakuja kukaangwa


Labda uchome mwenyewe, ila kama ni wale wachoma mahindi kitaa wanajikuna sana halafu bila kunawa mikono wanageuza muhindi
 
Tatizo, ni kwamba wabongo wengi wanajifanya wa kishua ila huku wakitafuna popcorn kitanzania tanzania sana na.kulimaliza kopo zima kabla ya dakika 5 za movie au mpira kuanza.

Ila wazo hilo ni bomba sana!
Kiutamaduni wa sinema, popcorn nddo snack iloenea kutumika kwa event hiyo!!! Sijui kwanini ila hatujachelewa kuanzisha utamaduni wetu!!! Ila tuangalie na utengenezaji wa hayo mahindi pia...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom