Noma sana, nakumbuka miaka flani nikamsindikiza msela wangu kutoa mahari, moja la hitaji la wakwe ilikuwa wapelekewe mbuzi. Basi tukanunua mbuzi then jamaa akamuweka kwenye buti ya gari. Safari mpaka kwa wakwe hapo tumepaki tumesahau kama mbuzi yupo mule. Wakwe wanatiki vitu haya kreti la bia, mbuzi dooh. Wakaenda mchukua mbuzi akazima mbele ya watu nikasikia mbibi kwa mbali anasema laaanaaa hii. Ndio maana siku hizi mahari ni cash tu.