Munkari suala la mahari inaenda wapi ni suala pana sana kujadili, maana inategemea imani ya dini mtu aliyonayo au na pengine na tamaduni za kabila husika. Kwenye tamaduni nyingi, mahari huchukuliwa kama "token of appreciation" inayotolewa toka kwa kuoaji kwenda kwa mzazi wa binti kumshukuru kwa kumzalia na kumtunzia huyo binti. Mahari hiyo pia hugawiwa kwa ndugu wa karibu kama babu, bibi, wajomba, mashangazi nk kulingana na mila na tamaduni za eneo husika.
Tukirudi kwenye imani, kama alivyosema
Rock City, kwa waislam mahari huenda kwa binti anayeolewa. Ukisome Quran [4:4] kuna andiko linasema "
You shall give the women their due dowries, equitably. If they willingly forfeit anything, then you may accept it; it is rightfully yours."
Lakini kwa upande wa Wawakristo, Maandiko yanasema mahari huenda kwa wazazi wa binti na ilitafsiriwa kama "payment made by a man as a gift to the family of a woman he desired to be his wife". Ukisoma Genesis 29, andiko linasema "Jacob loved Rachel and offered to work seven years for her father, Laban, in exchange for her hand in marriage". Na huu ulikuwa ni mfano wa mahari zilizotolewa zamani ktk imani na tamaduni tofauti.
Hitimisho kwa mtazamo wangu
Hivyo, ndugu suala la mahari inakwenda wapi inategemea imani ya dini yako na kama si mtu wa imani sana basi tamaduni za kabila lako husika. Ni ngumu kuelezea moja kwa moja wapi mahari iende kwa sababu ya tofauti za kiimani na kitamaduni.