Mahanga atabiri kifo cha CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahanga atabiri kifo cha CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, May 2, 2011.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mbunge wa Segerea (CCM), jijini Dar es Salaam Dk. Makongoro Mahanga, amesema bado CCM haijajivua gamba na ameitahadharisha kuwa isipojisafisha na tope la rushwa na ufisadi kama ilivyoagizwa na Halmasahuri Kuu (NEC) itapigwa mweleka kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

  Amesema kupungua kwa kura za urais mwaka jana ni kielelezo kuwa chama kinaweza kuanguka hivyo jitihada za makusudi zinahitajika kwa ajili ya kukinusuru.

  Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho tawi la Ugombolwa kata ya Segerea, ambayo inaongozwa na diwani wa Chadema.

  “Hii si dalili nzuri hata kidogo na wala tusijidanganye kuwa CCM itatawala milele na tukalala, makundi bado yako tuyavunje maana haya yakiendelea tujue mwaka 2015 tutapigwa mweleka,” alisema Dk. Mahanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira.

  Alisema mwaka 2005 chama hicho kilipata ushindi wa kimbunga wa asilimia zaidi ya 80 kwa nafasi ya urais, lakini kushuka hadi asilimia 61 mwaka jana ni dalili ya hatari kubwa mbele ya safari.

  “Tujiulize, mwaka 2005 tulipata asilimia zaidi ya 80, mwaka 2010 asilimia 61, je mwaka 2015 tukishuka na kupata asilimia 40 kutakuwa na chama hapo jamani, kwa hiyo tusibweteke na kuona hii asilimia 20 iliyopongua uchaguzi wa mwaka jana kuwa ni ndogo,” alisema Dk. Mahanga.

  “Ndugu zangu tufanye kazi la sivyo mambo yatazidi kuharibika huko tuendako, mnakumbuka uchaguzi wa mwaka jana hapa palikuwa hapatoshi, mimi mwenyewe nimeshinda kwa hatihati, katika asilimia za ushindi wa nafasi ya ubunge, jimbo letu la Segerea liko nafasi ya tatu kutoka chini, maana nilimshinda mpinzani wangu kwa kura 4,000, tu inamaana hawa wapinzani wangeungana nisingekuwa mbunge leo,” alisema.

  Dk. Mahanga alisema kuna wanachama wa chama hicho wamekuwa na chuki zisizo na kikomo ingawa mchakato wa uchaguzi ulishamalizika na ndio wanakihujumu chama.

  “Makundi wakati wa kura za maoni ndani ya chama ruksa, maana kila mtu anakuwa na wapambe wake, lakini nilipopitishwa na NEC mlipaswa kumaliza makundi, cha kushangaza humu humu CCM kuna watu walikuwa wamenuna na inaonekana walikuwa wanashabikia upinzani, na wakasababisha uchaguzi kuwa mgumu sana” alisema.

  Alisema hatua ya sekretarieti kuu kujiuzulu na kuwekwa mpya si kujivua gamba kwani huo ni mwanzo wa kuelekea kujivua gamba na isitafsiriwe kuwa mambo sasa yameshanyooka.

  Alisema kujivua gamba ni pale ambapo viongozi watajirekebisha na kuhakikisha chama hakipati tena tuhuma za ufisadi.

  "Kuondoka kwa Makamba (Yusuf) na ujio wa Katibu Mkuu mpya Mukama (Wilson) si kwamba ndo tumeshajivua gamba, hapana huo ni mwanzo wa safari tunapaswa kujirekebisha kuokoa chama chetu," alisema.

  Kadhalika, Dk. Mahanga alisema kujivua gamba kwa chama hicho si kufukuzana ndani ya chama kama wanavyodhani baadhi ya watu bali ni kujirudi na kujirekebisha kwa wanachama wote wa chama hicho.

  Alisema dhana pana na ya ukweli ya kujivua gamba ni wanaCCM wote kujiuliza, kujirudi na kujirekebisha na kuwa na mtazamo chanya wa kukijenga upya chama hicho.

  Alisema tatizo lingine ambalo lilikiathiri chama hicho mwaka jana na ambalo lilizungumzwa kwa kirefu kwenye mkutano wa NEC Dodoma ni rushwa na ufisadi.

  Alisema NEC iliazimia kuwa sasa ni wakati mwafaka wa chama kujisafisha kutoka kwenye tope la rushwa na ufisadi.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #2
  May 2, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Makongoro hakushinda bali alitangazwa mshindi. Unapomgusa Lowasa unagusa moyo wa Makongoro Mahanga kwani anaamini kuwa akiwa Rais yeye mambo yake yatanyooka zaidi. Hana jipya ni magamba yaleyele tu
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  mwizi wa kura huyo
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mahanga anamaanishaaa niniiiii???????
   
 5. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mahanga is another guy among currupted figures!!!!!
   
 6. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,852
  Likes Received: 2,780
  Trophy Points: 280
  Hivi si tuliambiwa na MP tukiwaona mafisadi tuwapigie mayowe? Huyu naye ni wa kupigia yowe mwizi wa kura mkubwa huyo! Eti anatudanganya alishinda kwa hatihati na kwa kura chache wakati alishindwa!!

  Hebu aoene aibu!!
   
 7. d

  daniel.nickson Member

  #7
  May 2, 2011
  Joined: Apr 30, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa wale wanaoishi segerea, au wilaya ya ilala au mkoa wa dar au unaishi nje ya mkoa mkoa huu lakini walikua wanafuatilia kwa karibu uchaguzi wa mwaka jana watakubaliana nami kwamba segerea ni moja ya majimbo mengi ambayo upinzani ulishinda lakini mgombea wa ccm akatangazwa mshindi, mengine kwa uchache ni kama babati vijijini(nccr), same mashariki (chadema), karagwe (chadema), shinyanga mjini(chadema), tandahimba(cuf) na mengine mengi.
   
 8. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hali yao ni mbaya , ndio maana kila mmoja na lwake mara huyu katabiri chama kufa, mara huyu kasema chama kinajivua magamba, mara huyu gamba likitoka sumu huongezeka, mara yule nyoka akijivua gamba huongezeka ukubwa sasa kipi ni sahihi?

  Na kusema kuwa Kikwete alishinda kwa asilimia 61 sio sahihi ndio maana mpaka leo tume wameshindwa kuweka matokeo kwenye website yao...
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Makongoro Mahanga ni mbunge wa NEC kwenye jimbo la segerea, namchukia huyu mpumbavu kuliko mwanasiasa yeyote, huyu baada matokeo kuonesha ameanguka akaamuwa kusubortage matokeo kwenye zile kata ambazo CHADEMA ilifanya vizuri mpaka akasababisha hata kwenye kata yangu ambako diwani wa CHADEMA alishinda na diwani wa CCM alishakubali kushindwa kwa mdomo basi matokeo yakapinduliwa na matangazo ya washindi yakaamishiwa Anatouglu baada ya siku 3, eti Dar es salaam hii matokeo ya Zanzaibar nzima yametangazwa lakini eti kata yetu matokeo siku 3 hawataki kutangaza mpaka wakapinduwa matokea eti diwani wa ccm kashinda kwa tofauti ya kura 16! ili linaniuma sana, na nitamchangia Pesa za kuendesha kesi Mpendazoe mpaka tumuondoe huyu jambazi kwenye jimbo letu, mpumbavu malaya mkubwa huyu.
   
 10. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mi naamini kuwa mtu huitaji kabisa kuwa Filip Kajura au Hussein Yahya kukitambua kifo cha ccm! Ccm kwa sasa ni sawa na mgonjwa aliyerudisha nyumbani kutoka hosp baada ya ushauri kutoka kwa Dr bingwa. Unaambiwa mumrudishe mgonjwa nyumbani mkajaribu tena na dawa za mababu.
   
 11. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #11
  May 2, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Makkkkokorooo kuuuuumaaaaaaaa!
   
 12. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  makongoro bora tu useme wazi kuwa hukushinda bali mfumo umekurudisha. Waeleze watu wako ukweli uujuao nafsini mwako ukweli ambao kila mtu anaujua. sitarajii utafika next election brother, take it from watu wa jimbo lako, hufiki asilani
   
 13. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #13
  May 2, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Tayari Mahanga Makongoro keshapata gongo distilled in Kitunda,Don wake katoswa sasa haoni wa kumkingia kifua ,ajiulize yeye alipata kura ngapi naye ajivua gamba kwani alikwiba kura za wana Ukonga
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  May 2, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye RED jimbo ni segerea na hiyo kitunda ipo jimbo la ukonga. kuwa makini unapopost kuondowa usumbufu.
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MAMBO NDANI YA CCM HIVI SASA NI HATIRI NA WALA SI SALAMA:
  WENZETU HIVI SASA MBELE HAKUENDEKI NA NYUMA HAKURUDIKI KATIKA MKAKATI WA 'OPERESHENI VUA GAMBA' KUKOMESHA UFISADI NDANI MWAKE

  Haaa!!! haaa!!!! haaaaaa, CCM bana!!!

  Willisoni hiyo ripoti ya kuokotwa mitaani wala haikua Scientific Research, itupe mbali sana kwa kuwa itakisambaratisha CCM kwa haraka zaidi kuliko wengine tunavyotarajia leo hii.

  CCM imara zaidi ya KANU ya Kenya ndani ya kambi ya upinzani ni muhimu sana kwa utawala murua kwa CHADEMA na wananchi kwa ujumla tangu hapo 2015.

  Masikini CCM, mlivyoingia kiulaini ndani ya huu mtego ya OPERESHENI VUA GAMBA!!! Katika hili mnalooo; nyuma hakurudiki na wala mbele hakuendeki katika vita vyenu dhidi ya UFISADI nchini.

  Nasema CCM mnaloooo mwaka huu sijui sasa wananchi tutaelezwa kiswahili gani baada ya siku 90 za kujivua gamba???????????

 16. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  sasa nani gamba kama sio yeye kwa kuwachakachua segerea? kwa yuko kambi gani , ya sitta au mwakyembe kama sio hiyo ya RACHEL ?
  naona yale ya MENGI yametimia aliposema kwa tanzania ya leo MWIZI ANAOBA KISHA YEYE NDIO ANAMPIGIA YOHE ALIYEMUIBIA!!!!!!
  hawa na ccm yao watatuuza, wasije kuchoma tu ofisi zetu za magogoni kama alivyofanya chinga kupoteza ushahidi
   
 17. M

  Marytina JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  anza wewe MAHANGA kujivua gamba la ufisadi na elimu
   
 18. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Joseph Mwendapole

  Mbunge wa Segerea (CCM), jijini Dar es Salaam Dk. Makongoro Mahanga, amesema bado CCM haijajivua gamba na ameitahadharisha kuwa isipojisafisha na tope la rushwa na ufisadi kama ilivyoagizwa na Halmasahuri Kuu (NEC) itapigwa mweleka kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

  Amesema kupungua kwa kura za urais mwaka jana ni kielelezo kuwa chama kinaweza kuanguka hivyo jitihada za makusudi zinahitajika kwa ajili ya kukinusuru.
  Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho tawi la Ugombolwa kata ya Segerea, ambayo inaongozwa na diwani wa Chadema.

  “Hii si dalili nzuri hata kidogo na wala tusijidanganye kuwa CCM itatawala milele na tukalala, makundi bado yako tuyavunje maana haya yakiendelea tujue mwaka 2015 tutapigwa mweleka,” alisema Dk. Mahanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira.

  Alisema mwaka 2005 chama hicho kilipata ushindi wa kimbunga wa asilimia zaidi ya 80 kwa nafasi ya urais, lakini kushuka hadi asilimia 61 mwaka jana ni dalili ya hatari kubwa mbele ya safari.

  “Tujiulize, mwaka 2005 tulipata asilimia zaidi ya 80, mwaka 2010 asilimia 61, je mwaka 2015 tukishuka na kupata asilimia 40 kutakuwa na chama hapo jamani, kwa hiyo tusibweteke na kuona hii asilimia 20 iliyopongua uchaguzi wa mwaka jana kuwa ni ndogo,” alisema Dk. Mahanga.

  “Ndugu zangu tufanye kazi la sivyo mambo yatazidi kuharibika huko tuendako, mnakumbuka uchaguzi wa mwaka jana hapa palikuwa hapatoshi, mimi mwenyewe nimeshinda kwa hatihati, katika asilimia za ushindi wa nafasi ya ubunge, jimbo letu la Segerea liko nafasi ya tatu kutoka chini, maana nilimshinda mpinzani wangu kwa kura 4,000, tu inamaana hawa wapinzani wangeungana nisingekuwa mbunge leo,” alisema.

  Dk. Mahanga alisema kuna wanachama wa chama hicho wamekuwa na chuki zisizo na kikomo ingawa mchakato wa uchaguzi ulishamalizika na ndio wanakihujumu chama.

  “Makundi wakati wa kura za maoni ndani ya chama ruksa, maana kila mtu anakuwa na wapambe wake, lakini nilipopitishwa na NEC mlipaswa kumaliza makundi, cha kushangaza humu humu CCM kuna watu walikuwa wamenuna na inaonekana walikuwa wanashabikia upinzani, na wakasababisha uchaguzi kuwa mgumu sana” alisema.

  Alisema hatua ya sekretarieti kuu kujiuzulu na kuwekwa mpya si kujivua gamba kwani huo ni mwanzo wa kuelekea kujivua gamba na isitafsiriwe kuwa mambo sasa yameshanyooka.

  Alisema kujivua gamba ni pale ambapo viongozi watajirekebisha na kuhakikisha chama hakipati tena tuhuma za ufisadi.

  “Kuondoka kwa Makamba (Yusuf) na ujio wa Katibu Mkuu mpya Mukama (Wilson) si kwamba ndo tumeshajivua gamba, hapana huo ni mwanzo wa safari tunapaswa kujirekebisha kuokoa chama chetu,” alisema.

  Kadhalika, Dk. Mahanga alisema kujivua gamba kwa chama hicho si kufukuzana ndani ya chama kama wanavyodhani baadhi ya watu bali ni kujirudi na kujirekebisha kwa wanachama wote wa chama hicho.

  Alisema dhana pana na ya ukweli ya kujivua gamba ni wanaCCM wote kujiuliza, kujirudi na kujirekebisha na kuwa na mtazamo chanya wa kukijenga upya chama hicho.

  Alisema tatizo lingine ambalo lilikiathiri chama hicho mwaka jana na ambalo lilizungumzwa kwa kirefu kwenye mkutano wa NEC Dodoma ni rushwa na ufisadi.
  Alisema NEC iliazimia kuwa sasa ni wakati mwafaka wa chama kujisafisha kutoka kwenye tope la rushwa na ufisadi.

  CHANZO: NIPASHE
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kifo hicho kilichotabiriwa CCM, Mahanga mwenyewe kujitoa mhangaaaaaaaaaa au???
   
 20. D

  DENYO JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko ccm -magamba kuwatosa magamba wenzao
  nape, chiligati, na mkulu siku ile walitoka kwa mbwembwe sasa wananywea wenyewe hivi hawakujua kwamba mapacha watatu ndio walioshikiria ccm na ndio wanoendesha serikali ya kimtandao? Tofauti na chadema na slaa hakuna mtu mwingine mwenye ubavu wa kumtosa chenge anajua madudu mengi ten years as ag. Tofauti na chadema na slaa dr wa ukweli hakuna mwingine anaweza kumtosa mzee wmenye mvi amekamata kila kona ya ccm watavua wapi waache wapi? Amekamata hadi spika -kila konaaaaaaa ni mjanja huyu isipokuwa kwa chadema tu na dr slaa ndio maana alisema ccm iangalie sana arusha, tofauti na chadema na dr slaa nani anaweza kumnyoshea roast ni gwiji la magamba anajua kila kila kona akiguswa tu anafungulia -nape ajifunze sasa ataanza kuchukua chake mapema na kuanza kuwapamba. Kifo cha ccm hicho mbele pachungu nyuma pachungu waende wapi??????? Let them dissolve the party.
   
Loading...