Mahanga adai uchaguzi umekwisha sasa tuchape kazi!!!!!!!!!!!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahanga adai uchaguzi umekwisha sasa tuchape kazi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Feb 2, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi umekwisha, tuchape kazi - Mahanga


  na Mwandishi wetu


  [​IMG] MBUNGE wa Jimbo la Segerea, Makongoro Mahanga (CCM), amewataka wananchi na viongozi waache kutumia muda mwingi kuzungumzia masuala ya uchaguzi mkuu uliopita bali wajikite kwenye shughuli za maendeleo.
  Mahanga alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam alipokuwa akiwashukuru wananchi wa Kata ya Kiwalani kwa kumchagua kuwa mbunge pamoja na kuwachagua madiwani wa CCM katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 30 mwaka jana.
  Alisema kuwa viongozi waliochaguliwa wana wajibu mkubwa wa kutekeleza majukumu yao na ahadi walizozitoa wakati wa kampeni.
  Aliongeza kuwa pamoja na wajibu huo ni vema hivi sasa wananchi kwa kushirikiana na viongozi waliochaguliwa wakajikita katika shughuli za maendeleo badala ya kujikita kwenye malumbano ya uchaguzi.
  Alisema atahakikisha anakuwa mstari wa mbele kushirikiana na wananchi bila kujali tofauti za kiitikadi kwa kuwa kiongozi yeyote anapochaguliwa hapaswi kuwabagua wapigakura.
  “Sitabagua mtu yeyote eti kwa kuwa hakunipigia kura, maendeleo hayawezi kupatikana kwa namna hiyo, uchaguzi umekwisha tuache porojo zake, tuchape kazi,” alisema.
  Mahanga, alisema wananchi wamewaamini viongozi walioko madarakani hivi sasa hivyo ni busara kwa viongozi hao kuwatumikia ili kutovunja imani iliyoonyeshwa kwao.
  Naye Khadija Juma, mkazi wa Kiwalani, alisema kama viongozi walioko sasa hawatajikita katika kutatua kero za wananchi mwaka 2015 wasihangaike kuomba kura.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  PHP:
  [IMG]http://www.freemedia.co.tz/daima/anime/amka2.gif[/IMG] MBUNGE wa Jimbo la Segerea, Makongoro Mahanga (CCM), amewataka wananchi na viongozi waache kutumia muda mwingi kuzungumzia masuala ya uchaguzi mkuu uliopita bali wajikite kwenye shughuli za maendeleo.
  huyu ni bulicheka wa kweli.........kwa vile yeye kanufaika na dhuluma basi anataka tukaee kimya hadi damu siku itakapomwagika........................................inabidi tuendelee kuuzungumzia uchaguzi huu ili ile dhuluma tuitafutie mwarobaini........................
   
 3. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,801
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280

  Mkuu huyu jamaa si mkweli hata kidodo, hebu check hii
  Wananchi wanachanga pesa ili waweze kujenga kivuko kutoka Taa nyekundu Temeke kuja Kiwalani, wakajikusanya wakaanza utengenezaji wa kivuko huyu bwana aliposikia akajileta na watu wa makamera na kumfanyia Coverage pale kwenye kivuko na kuagiza kamati iliyopo kushirikiana na Manispaa ya ilala kuweka michoro ya Daraja la kudumu na kupelekewa yeye riport kwani ana wafadhili ambao watalijenga, cha ajabu alipelekewa taarifa zote muhimu mara tano mambo yakawa Documents zimepotea lete nyingine, tulikuwa tunafanya usafi tumemisplace, nipo busy Dodoma si mnajua mm ni mbunge mpaka kamati ile ikashindwa kumfuatilia na ikawa ndio mwisho wa kivuko kile muhimu kwa wakazi wa temeke na Kiwalani na nguvu wa wananchi kuishia pale, lakini amefanya sherehe kubwa ya watu kula pilau kata ya Kiwalani huku kukiwa na matatizo ambayo angeweza kujatatua kwa kutumia gharama hizo......FUNIKA KOMBE MWANA....................APITE
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kesi ya Mpendazoe ya kupinga ubunge wa Mahanga si ilipangwa kuanza kusikilizwa mapema mwezi huu, sasa imeishia wapi?
   
Loading...