Mahakama zetu zinafuata hii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama zetu zinafuata hii?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MAKOSHNELI, Oct 25, 2011.

 1. MAKOSHNELI

  MAKOSHNELI JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 474
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 80
  [h=1]AMRI KUMI ZA SHERIA ZILIVYOORODHESHWA NA[/h]ALIYEKUWA JAJI MKUU WA TANGANYIKA MWAKA [1928]
  1. Usijari,hata kidogo kukwepa uwajibikaji kwenye hukumu zako. 2. Usimtie hatiani mtu ambaye amejulikana ana tabia mbaya mpaka pale umeridhika kwamba ametenda kosa analoshitakiwa. 3. Usisite kumuachia huru mtu ambaye hakuna ushaidi mbele yako wa kumtia hatiani, hata kama unajaua ametenda kosa, wewe sisitiza upate ushaidi.
  1. Usisite kumtia hatiani mtu na kumuadhibu ipasavyo, kama kuna ushaidi kuonyesha kwamba ametenda lile kosa hata kama ni mkubwa….
  5. Usiende nje ya ushaidi unaopewa Mahakamani, kwa lugha nyepesi, usisikilize mambo ya mtaani.
  6. Usitoe hukumu huku jicho lako liko kwa wakubwa wako wa kikazi, yaani kwa hofu ya hukumu yako kupinduliwa, Au huku ukihofia magazeti,au kitu chochote kile- Wewe zingatia sheria na ushaidi.
  7. Usiizungumzie kesi kabla haijamalizika mbele yako, na usiruhusu mtu aizungumzie mbele yako.Vile vile ni vema kutokuizungumzia kesi hata baada ya kumalizika, hadi wakati imekuwa historia – Jaji au Hakimu anapata heshima kubwa sana toka kwa jamii ikiwa mtulivu, asiyeropoka juu wadhifa wake, na anayeendesha kazi zake kwa utulivu na hekima. 8. Usisite kuomba ushauri toka kwa wale majaji na mahakimu waliokutangulia kikazi, na waliopata uzoefu wa muda mrefu kazini. 9. Hata siku moja usikasirike Mahakamani, na vile vile usiwe na jaziba hata kama umechokozwa kiasi gani, Usisahau kwamba wewe pale penye ukumbi wa Mahakama ni bosi (nikitumia neno linalotumiaka sana siku hizi kwa kiongozi wa juu kabisa), kutokaririshwa na kutobabaishwa ni silaha kali sana kwa washitakiwa na mashaidi wakorofi Mahakamani. 10. Usiwe na haraka isiyo na maana, Chukua muda wako na toa hukumu safi na ya haki, Usipende kuonekana kwamba wewe ni mchapakazi zaidi kuliko wengine,Unaandika haraka haraka sana, lakini hukumu zako ni mbovu na hazina haki ndani yake,Utaheshimu zaidi watu watajua kwamba wewe siyo mlipuaji wa kazi zako Mahakamani……..[na JajiJoseph Masanche].
   
 2. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mahakama zetu yanaongozwa na viongozi wa kisiasa hata katika kutoa hukumu,katika mihimili mitatu Bunge Mahakama na Serikali, huu wa Mahakama unachezewa sana na viongozi walioko madarakana.
   
Loading...