mizambwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2008
- 4,422
- 1,790
HUKUMU YA KESI YA MAUAJI YA SWETU FUNDIKIRA:
Katika kesi inayoumuhusu Swetu Fundukira hakimu wakati wanasoma hukumu alikariri maneno yafuatayo:-
"Sheria iko wazi ukiondoka na mtu au ukionekana naye kwa mara ya mwisho na baadaye mtu huyo akapatikana na madhara, wewe ndiyo unawajibika kutoa maelezo ya kina kuhusu yaliyompata mtu huyo," alisema Jaji Muruke na kuongeza;
"Kisheria ukitoa maelezo ambayo hayajakidhi haja na yana utata ni faida kwa upande wa mashtaka ambao hutegemea ushahidi wa mazingira. Maelezo ya kina hayajatolewa na washtakiwa wote."Aliendelea,
"Ushahidi wa Jamhuri japokuwa ni wa mazingira, umejengwa thabiti na upande wa utetezi haukuweza kujenga matundu, ama kuuvunja mnyororo huo, kidole kinawaelekea wao."
Jaji Muruke alisisitiza kuwa katika kesi hiyo licha ya kuwa kuna ushahidi wa kimazingira, upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka bila kuacha mashaka.
"Hivyo kosa wanaloshtakiwa nalo limethibitishwa na Mahakama imewaona washtakiwa kuwa wana hatia ya kumuua Swetu Abdallah Fundikira," alisema Jaji Muruke, huku akimuuliza wakili wa Serikali kama washtakiwa wana kumbukumbu zozote za makosa ya jinai.
TUKIO LA KUTEKWA KWA DR. ULIMBOKA:
Taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari (mfano. Gazeti MWanahalisi) ni kwamba hadi muda wa mwisho aliongea kwa simu na mtu aliyetajwa kuwa ni Bw. Ramadhani Inghondu, mtumishi wa usalama wa Taifa IKULU. Ha ushahidi wa namba yake ya simu iliyotumika kupanga ahadi ya kukutana naye dakika za mwisho. Na pia mwenyewe Dr. Ulimboka akathibitisha kuwa alitekwa na huyu ndugu, na pia kabla ya kutekwa alikutana naye Leaders Club - DSM, kisha wakamteka.
MY TAKE:
Je, haya matukio mawili mbona naona kama yanafanana kutokana na hukumu iliyowapata hawa vijana wa Mwamunyange na lile la kutekwa, kuteswa kwa Dr. Ulmboka??
Naomba nisaidieni kuelewa huenda nina kasoro ya uelewa wa mambo haya kutokana na elimu yangu ndogo ya Darasa la Tatu chini ya mti kwani nilikimbia kulowana mvua kila siku kule Morogoro kwetu.
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!