Mahakama yazuia kuuawa kwa wafungwa Arkansas, Marekani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,407
Mahakama ya Juu katika jimbo la Arkansas nchini Marekani imetoa agizo la kuzuia kuuawa kwa wafungwa wawili kati ya wanane ambao wamepangiwa kuuawa kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Mawakili wa wafungwa hao, ambao walipatikana na makosa ya mauaji, wameibua maswali kuhusu hali ya kiakili ya wafungwa hao.

Serikali ya Arkansas imesema itakata rufaa uepesi kupinga uamuzi huo.

Katika uamuzi mwingine, mahakama hiyo pia iliondoa agizo la muda la kuzuia kuuawa kwa wafungwa hao wanane.

Jimbo la Arkansas linataka kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya wafungwa hao haraka iwezekanavyo kwa sababu shehena yake ya dawa za kutumiwa kuua wafungwa inakaribia kufikisha muda wake wa mwisho kutumika.

Dawa hiyo aina ya Midazolam itafikisha muda wake wa mwisho wa kutumika mwishoni mwa mwezi Aprili.

Mahakama ilikuwa imetoa agizo la muda Jumamosi kwamba wafungwa hao hawangeuawa kwa sababu shindano hiyo ya sumu ingewasababishia dhiki.

Watetezi wa haki wamepinga kutumiwa kwa dawa hiyo.

Wanaume hawa walifanya nini?

_95385737_716326b8-a211-4f50-a449-21f2ed9cd924.jpg

Bruce Ward - Alimnyonga kijana mhudumu wa duka Rebecca Doss

Don Davis - Alimuua ane Daniel alipokuwa akitekeleza wizi

Stacey Johnson - Alimuua Carol Heath, ambaye alichapwa na kunyongwa kisha kukatwa shingo

Ledell Lee - Alimuua Debra Reese kwa kumpiga kwa kipande cha chuma

Jack Jones - Alimbaka na kumuua Mary Phillips

Marcel Williams - Alimbaka na kumuua Stacey Erickson, baada ya kumteka kutoka kwenye duka moja

Kenneth Williams - Alimuua mkulima Cecil Boren wakitoroka gerezani ambapo Williams alikuwa amefungwa kwa kumuua Dominique Hurd

Mbona suitafahamu?

Sawa na majimbo mengine mengi Marekani, jimbo la Arkansas limetatizika kupata dawa za kutumiwa kuwaua wafungwa.

Mara ya mwisho wafungwa kuuawa jimboni humo ilikuwa mwaka 2005.

Maswali kuhusu Midazolam yalianza kuulizwa baada ya wafungwa katika majimbo matatu Marekani kuchukua muda mrefu kuliko kawaida walipokuwa wakiuawa mwaka 2014.

Chanzo: BBC
 
Hakuna kuremba; yeyote anayeua kwa kukusudia, stahiki yake ni kifo tu! Mbona wao walipokuwa wanauwa binadamu wenzao hawakuwa na huruma? Nimesoma sababu za kukatiwa kwao adhabu ya kifo; duh! Wanyongwe haraka sana maana walikosa chembe ya utu.
 
Wamarekani wa ajabu sana wao wanapiga vita wengine wasitekeleze hii adhabu ya kifo kumbe wao wanafanya sana au kisichotakiwa ni kunyonga kwa kamba kwa sindano ni ruhusa?
 
Back
Top Bottom