DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imetoa kibali cha kufungua kesi ya msingi kwa walalamikaji Vyonheaven Exaud Urima na Andrew Fadhili Bomani katika shauri la kiraia Na. 8286/2025 waliofungua dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)
Katika shauri hilo walalamikaji wanapinga uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa wa kuchelewesha kushughulikia ombi la usajili wa chama kipya cha siasa cha Independent People's Party (IPP)
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dkt. Anna Henga, akizungumzia maamuzi hayo ya Mahakama amesema kituo anachokiongoza ndicho kinachowasaidia walalamikaji kuwapatia msaada wa kisheria Mahakamani, hivyo utolewaji wa kibali hicho ni hatua muhimu ya kitaratibu inayothibitisha wajibu wa mhimili wa Mahakama katika kusimamia matumizi ya madaraka ya kiutawala na kulinda haki za Kikatiba na haki za kiutawala.