Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,502
- 9,282
Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetoa hati kumwita Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu kuendelea kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.
Mbowe na wenzake wanatakiwa kuwa mahakamani hapo leo baada ya kesi yao kusimama kwa siku nne kutokana na Jaji Elinaza Luvanda kujitoa kuisikiliza. Jaji huyo alijitoa Jumatatu baada ya washtakiwa kutokuwa na imani naye kwamba hawaamini kama atawatendea haki baada ya kutupilia mbali mapingamizi waliyoweka.
Mahakama sasa imemteua Jaji Mustapha Siyani kusikiliza kesi hiyo. Kwa mujibu wa hati ya wito, kesi itaendelea leo mahakamani hapo
Mwananchi