Mahakama ya Mafisadi ndio itatekeleza maazimio ya Bunge kuhusu kashfa ya Escrow?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Hivi Mahakama ya Mafisadi ndio itakuwa na jukumu la kupitia upya maazimio ya Bunge kuhusu kashifa ya Escrow na kisha kuyatekeleza?

Maswali mengine:

Hivi Mahakama ya Mafisadi ndio itachunguza na kuchukua hatua kuhusu tuhuma za ununuzi wa kivuko kibovu?

Hivi Mahakama ya Mafisadi ndio itaibua upya sakata la Richmond baada ya Bunge kuagiza kufungwa kwa mjadala huo?

Hivi Mahakama ya Mafisadi ndio itaanzisha uchunguzi, kukamata walioua mashirika ya umma na kisha kuwafungulia mashitaka?

Hivi Mahakama ya Mafisadi ndio itachunguza sakata la mgodi wa Kiwira?

Hivi Mahakama ya Mafisadi ndio itazuia mafisadi kupewa adhabu za kifungo cha nje?

Hivi Mahakama ya Mafisadi itakuwa ni kwa ajili ya ma-CEO tu wa mashirika na Taasisi za umma na si wanasiasa mafisadi?

Yataka uvumivu na kuwa na moyo wa chuma kufuatilia siasa za nchii hii.
 
Itakuwa inashughulikia wale mafisadi papa wanaoandika maneno ya uchochezi na kumkosoa huko fb, Instagram, JF, WhatsApp.
 
Kila wanaloliombea Chadema linashindwa vibaya, inaonyesha jinsi gani shetani yupo upande wa bavicha mwaka huu.
 
Unaongelea kuanzisha mahakama ya mafisadi wakati unashindwa hata kutaja hadharani baadhi ya kashifa kubwa na kujisifu kuadhibu vidagaa!!
 
Tutajie kashifa kubwa iliyotokea enzi ya Magufuli.

Ukiweka pembeni Richmond
 
Sahau...

Kiwira?
Richmond?
Lugumi
Escrow

Hii mahakama ikiyagusa haya majipu nitatembea uchi mchana kweupe
 
Hivi Mahakama ya Mafisadi ndio itakuwa na jukumu la kupitia upya maazimio ya Bunge kuhusu kashifa ya Escrow na kisha kuyatekeleza?

Maswali mengine:

Hivi Mahakama ya Mafisadi ndio itachunguza na kuchukua hatua kuhusu tuhuma za ununuzi wa kivuko kibovu?

Hivi Mahakama ya Mafisadi ndio itaibua upya sakata la Richmond baada ya Bunge kuagiza kufungwa kwa mjadala huo?

Hivi Mahakama ya Mafisadi ndio itaanzisha uchunguzi, kukamata walioua mashirika ya umma na kisha kuwafungulia mashitaka?

Hivi Mahakama ya Mafisadi ndio itachunguza sakata la mgodi wa Kiwira?

Hivi Mahakama ya Mafisadi ndio itazuia mafisadi kupewa adhabu za kifungo cha nje?

Hivi Mahakama ya Mafisadi itakuwa ni kwa ajili ya ma-CEO tu wa mashirika na Taasisi za umma na si wanasiasa mafisadi?

Yataka uvumivu na kuwa na moyo wa chuma kufuatilia siasa za nchii hii.

Tararira
 
Ungeminywa Uhuru wa kutoa habari ,ungekuwa hapa unatoa uharo wako?
Post ya Ben kuhusu elimu ya mh.unaona inavyofanyiwa?Kwanini kila ikiletwa pamoja na kuwa na details nyingi inaunganishwa na post isiyo na chochote cha maana zaidi tu ya tuhuma za juujuu zisizo na maelezo ya kutosha?
 
Hebu lete detail za elimu ya hapa na pale ya Mbowe kwanza kama wewe ni jasiri kweli
 
Back
Top Bottom