Mahakama ya mafisadi: itaanza na wa kashfa ipi hasa?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Nauliza kwa Dr. John Pombe Magufuli na wanaomuunga mkono. Mimi simo kwakuwa simuungi mkono Magufuli wala Lowassa. Mahakama ya Mafisadi imekuwa sera ya Dr. Magufuli. Amekuwa akionwa kama mpambanaji wa ufisadi. Sasa nauliza, Dr. Magufuli akishinda na kufanikiwa kuunda Mahakama ya kushughulikia mafisadi, ataanza na kashfa gani?

Tunazo kashfa kama za Tangold, Meremeta, Kuuzwa kwa nyumba za Serikali, EPA, Richmond, Kuuzwa kwa wanyama waliohai, Malipo hewa ya mishahara Serikalini, Ufisadi kwenye kandarasi za barabara na madaraja, ESCROW, na nyinginezo. Tusije tukampa mbu kazi ya kutibu malaria! (Mrisho Mpoto).

Napendekeza aanze na kashfa ambazo naye anatajwatajwa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Siku akisema ukweli tena ukweli kabisa tena akisema kwa dhati kutoka moyoni kuwa ataonyesha mfano na kuagiza hiyo mahakama ianze na kashfa ya nyumba za serikali alafu ihamie kwenye upotevu wa pesa kwenye wizara ya ujenzi ambao CAG iliona nampigia kura.
 
Anaanzisha Mahakama ya nini wakati Sheria za kushughulikia Makosa Makubwa (Ufisadi) zipo? Hajui kuna Sheria ya Kupambana na Wahujumu Uchumi (Economic and Organised Crime Control Act, 1984)??
 
mnamuenea magufuli kumuuliza haya, masikini hata yeye mwenyewe hajui anamaana gani anaposema haya.
 
Nauliza kwa Dr. John Pombe Magufuli na wanaomuunga mkono. Mimi simo kwakuwa simuungi mkono Magufuli wala Lowassa. Mahakama ya Mafisadi imekuwa sera ya Dr. Magufuli. Amekuwa akionwa kama mpambanaji wa ufisadi. Sasa nauliza, Dr. Magufuli akishinda na kufanikiwa kuunda Mahakama ya kushughulikia mafisadi, ataanza na kashfa gani?

Tunazo kashfa kama za Tangold, Meremeta, Kuuzwa kwa nyumba za Serikali, EPA, Richmond, Kuuzwa kwa wanyama waliohai, Malipo hewa ya mishahara Serikalini, Ufisadi kwenye kandarasi za barabara na madaraja, ESCROW, na nyinginezo. Tusije tukampa mbu kazi ya kutibu malaria! (Mrisho Mpoto).

Napendekeza aanze na kashfa ambazo naye anatajwatajwa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Mahakama ya mafisadi itaanza na Magufuli kwa kutununulia mtumba wa meli ya abiria kati ya DSM na Bagamoyo
 
Back
Top Bottom