Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Serikali ya CCM imetenga Shs Bilioni 2.5 za kitanzania kwaajili ya Mahakama ya mafisadi, Tujiulize; ili iweje?
Je: Mahakama zetu zinashindwa kutoa hukumu hizo? Mfumo wetu wa kimahakama ni dhaifu kiasi gani,hata nchi ifikie huko? Au kwasababu ni ahadi iliyoahidiwa majukwaani wakati wa kampeni ili kujipatia kura, basi itekelezwe hata kama haina tija? Sidhani kama maneno yote ya jukwaani wakati wa kampeni yanapaswa kufanyiwa kazi, kwani wakati mwingine wagombea huchoka au huishiwa hoja, hivyo hutafuta cha kuongea, hasa wagombea wanaoongea sana, yaani wenye maneno mengi.
Mbali na kuwachenga wananchi kwa matumizi ya lugha, yaani mlisema mtajenga mahakama ya mafisadi, na sasa mnasema mtaunda kitengo (division) cha rushwa na ufisadi kwenye mahakama kuu... huu ni usanii mtakatifu usio hojika kwa akili ya kawaida, lakini usanii huu uliwanufaisha ninyi kwenye kampeni, hauna manufaa kwa taifa.
Basi, tuamini kuwa Ufisadi utaendelea kuwepo nchini na mafisadi wataendelea kuibuka serikalini na kufisadi fedha na mali za umma, maana yake hakuna namna ya kuudhibiti ufisadi na badala yake litakuwa ni janga endelevu, maana kama ipo dhamira ya dhati ya kuziba mianya ya ufujaji wa fedha za
umma, ufisadi utatokea wapi? mtaziba mianya, halafu mafisadi watakuwa wanazichota fedha za umma, mtakuwa mmeziba kweli? au bado tuamini kila kitu nchi hii kinachozungumzwa na viongozi ni kiini macho?
Mfano; Kuna mafisadi kumi nchini, mpaka sasa Serikali iwe imepigwa ganzi, ikose uwezo wa kuwafikisha mahakamani kuwashitaki, basi hata hiyo mahakama mnayoiita ya mafisadi hamtaweza kuwafikisha huko pia...
Kwanini msiboreshe na kuziimarisha Taasisi simamizi na kuzipa makali (kuzipa meno) ziwe na uwezo sio tu wa kuwabaini wabadhirifu wa mali ya umma, mafisadi na wala rushwa, bali ziwe na uwezo wa kuwafikisha mahakamani na ushahidi mkononi, taasisi hizi zikawa ndiyo mshitaki, na mafisadi, walarushwa, wabadhirifu nk. wakawa washitakiwa?
Mnavyotenga pesa hizo, maana yake ni kwaajili ya magari, vifaa vya maofisini, na gharama nyingine nyingi, kwanini fedha hiyo isielekezwe kwenye uchunguzi wa kina na upelelezi wa hali ya juu ili kukusanya ushahidi wa kweli na wakutosha, usio na shaka hata kidogo, juu ya wabadhirifu wa mali ya Umma, mafisadi, wala-rushwa, nk. hata kama waliwahi kuwa viongozi wa juu kabisa wa nchi, mfano marais, na kisha kuwapeleka mahakamani?
Mnaunda mahakama hiyo, itakuwa na gharama lukuki ambazo ni mzigo kwa wananchi, mfano hao mnaowaita mafiisadi, kama hamkuwekeza zaidi katika kujikusanyia ushahidi wa kutosha, mkiwapeleka huko, watashinda kesi, gharama zitakuwa upande wa serikali (fedha ya umma), ilhali mnajua kuwa taasisi simamizi ndizo zenye matatizo makubwa ya kuboreshwa, mfano TAKUKURU, CAG, na TUME YA MAADILI YA UMMA, taasisi hizi zikiimarishwa na kuongezewa ufanisi, tutaweza kukomesha kabisa mattizo haya ambayo yamekuwa ni donda ndugu nchini....
Watanzania, wasitegemee kuiona Tanzania mpya isiyo na Rushwa na Ufisadi, badala yake watarajie kuwaona mafisadi wakiibuka, wakipelekwa mahakamani kama kawaida, watashinda kesi na wengine watahukumiwa kufagia mahospitali, na nchi itaendelea kuwa na mifumo mibovu, uchumi mbovu, na viongozi wabovu.