Mahakama ya Kisutu yamhukumu raia wa Vietnam miaka 20 Jela au faini ya Millioni 100

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,504
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh. 100 milioni Bui Hoa, Raia wa Vietnam baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kukutwa na kucha na meno ya simba.

Hukumu hiyo imetolewa na Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu baada ya mshitakiwa huyo kukiri kukutwa na nyara hizo za serikali kinyume cha sheria.

Awali, Helleni Moshi, Wakili wa Serikali Mwandamizi alisema mshitakiwa huyo alikutwa na nyara hizo tarehe 8 Januari mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jinini Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa siku hiyo, Hoa alikutwa na kucha tano za simba na meno manne yote yakiwa na thamani ya Dola za Marekani 4900 (takribani Sh. 10,647,700 za Tanzania), mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.
 
Hao wachina wafungwe tu, na nawaomba Mahakimu wasiwe wanatoa option ya faini ama kifungo iwe kifungo tu.
Nilikwisha andika mara nyingi kuwa ktk nchi yetu, kila kosa la ajabu ajabu ni wachina. Nchi wameigeuza shamba la bibi, lakini vyombo vya usalama pia viwasake na wanaowasaidia na kuwapa kiburi. Kama wale wa Morogoro wa kukata mawe walivyokuwa wakijibu!
Wachina wazuri ni wale waliotujengea reli ya TAZATA tu. Lkn wengine kwa asili mia kubwa ni matapeli tu!
NAWACHUKIA sana.
 
Hakimu Simba ameona watateketea kama tembo....nashauri akina tembo waige mfano huo wa kutoa adhabu kali ili kujilinda dhidi ya wahalifu wa aina hiyo
 
Hakika tunahitaji hukumu kali za namna hii ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama za huyu Muevietnamu.
Hakimu amekuwa kama Rambo maana hawa kwenye movie huwa hawaishi kuja hata uwauwe vipi kama siafu.
 
Back
Top Bottom