Mahakama ya Kisutu imegoma kumfutia dhamana Tundu Lissu baada ya Jamhuri kuomba afutiwe

Bila kusahau hakimu simba ndo aliemfunga yule mtoto wa miaka 14 kifungo cha maisha
 
Watu wa humu vigeu geu aki. Juzi hakimu huyu huyu alitoa hukumu ya life imprisonment mkamtukana leo kaibania serikali mnammwagia sifa. I hope siku moja mtamjua kuwa ni the most humble and thoughtful magistrate I've ever seen in my career. Ila ma state attorney Mungu anawaona khaah.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hakinui siyo malaika; ni binadamu wa kawaida tu kama sisi. Atasifiwa wapofanya vizuri na kukosolewa anapoonekana kupotoka. Najua mahakimu wao hilo wanalitambua vizuri.
 
Mtapata tabu sana

Na apo ndio Dunia itaprove Serikali ndio iliyomshambulia.

Mmeshindwa Swala la Korosho mtaweza mziki wa Lissu?

Size yenu ni Vitambulisho vya machinga sio Lissu mjipange kweli kweli...

Lasivyo mtawekewa vikwazo na shilingi itafika elf10 kwa dollar......

Over.

Sent using Jamii Forums mobile app
hivi kuna mtu asiyejua hili ?
 
Wazulu niliwaweka kwenye list ya watu wenye roho mbaya ukanda huu wa SADC ila kwa hili linaloendelea kuhusu Lissu bila shaka yeyote Watanzania ndio wakatili na wauaji hao Wazulu wanasubiri mbali...mtu kaondoka ajitambui leo mnapeleka dokezo la kutaka kumkamata kisa kuwafurahisha wanaowatuma uzuri karma ipo hapa hapa Duniani...
 
Ni wapi imeandikwa ukiwa mgonjwa huruhusiwi kufanya siasa au majukumu yako?Mbona spika ndugai alipokuwa India,alihamishia ofisi yake huko india katika hoteli ya nyota 5 pamoja na wahudumu wake wa ofisi?Nakumbuka katika kipindi hicho akiwa kwenye matibabu india,ndipo alipotekeleza maamuzi ya kiofisi kwa kujibu barua aliyoandikiwa na Lipumba kuwa CUF imewafukuza wabunge kadhaa wa viti maalumu,Spika akiwa kitandani(hoteli ya nyota 5) akamjibu na hapo hapo akamwandikia barua msajili kuwa nafasi za viti maalum CUF ziko wazi!!!!!
Nyani haoni kundule!!!!

jingalao YEHODAYA Wakudadavuwa stroke johnthebaptist mamayoyo1 MISULI ISIS MSAGA SUMU ndege JOHN USSR
Tundu Lisu ni spika wa bunge?Huyo spika alikuwa na kesi kisutu kama Lisu?
 
Watu wa humu vigeu geu aki. Juzi hakimu huyu huyu alitoa hukumu ya life imprisonment mkamtukana leo kaibania serikali mnammwagia sifa. I hope siku moja mtamjua kuwa ni the most humble and thoughtful magistrate I've ever seen in my career. Ila ma state attorney Mungu anawaona khaah.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijaelewa! Unataka akifanya vibaya asifiwe! Na akifanya vizuri atukanwe sio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tundu Lisu ni spika wa bunge?Huyo spika alikuwa na kesi kisutu kama Lisu?
Kwahiyo spika ana haki ya kutekeleza majukumu yake ila Lissu haruhusiwi kufanya hivyo?Akili zenu huwa mnaziacha wapi?
Ndio maana wadhamini waliitwa kisutu kwenda kueleza hali ya Lissu inaendeleaje,nadhani watakuwa wameieleza mahakama na ikaridhika na maelezo yao ndio maana hakimu akawaona mawakili wa serikali hawana hoja zaidi ya ukanjanja!
 
Huyo hakimu vipi? Anaposema hakuna asiyejua kuwa Lisu ni mgonjwa.Yeye kama hakimu kisheria taarifa za kujua mtu mgonjwa anazijulia magazetini,twitter,watsapp , Instagram,JamiiForums na media au ni report za madaktari? Huyo hakimu atueleze taarifa reliable za Lisu kuwa mgonjwa yeye reliable legal source kazipatia wapi kama hakimu?
Mh DC, Kisarawe kwema?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upande wa Jamhuri katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na wahariri wa gazeti wa la Mawio, wameomba Mahakama itoe hati ya kumkamata Lissu.

Wakili wa Serikali, Simon Wankyo amewasilisha maombi hayo leo Jumatatu Februari 25, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Wankyo amedai mshtakiwa anaonekana akizunguka nchi mbalimbali akitoa mihadhara na huko Ubelgiji anakodaiwa yuko Hospitali haijaelezwa yuko hospitali gani.

“Kama itafaa Mahakama iamuru mshtakiwa Lissu akamatwe maana hayupo hospitali kama inavyodaiwa hapa mahakamani,” amedai.

Mbali na Lissu, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.

Lissu na wenzake Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob, wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Inadaiwa kuwa Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, washtakiwa watatu, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

-Mtanzania
 
Back
Top Bottom