hiyo ndivyo tz ilivyo. Hata ktk idara ya afya ukiangalia gap lililoko kati ya madaktari na hao watumishi wengine utaona huruma! Ila wangepandisha mishahara kwa idara nzima. Kama ni idara ya mahakama basi wapandishwe wote kuanzia mfagiaji hadi judge, kama ni idara ya afya vivyo hivyo, kama ni idara ya elimu basi wakiwaongeza walimu waongeze mpaka kwa wale wanaotunza mazingira ya shule na maabara. Kutofanya hivyo ni kuleta conflict/chuki baina ya watendaji walioko ktk sehemu/ofisi moja. Hakimu na karani wa mahakama wanafanya kazi mazingira hayo hayo(rushwa etc wanashawishika wote) kwanini uongeze mshahara wa hakimu peke yake? Kama kigezo ni elimu yake basi ongezeni kwa kufuata elimu hiyo(eg.degree) kwa watumishi wote wa serikali kwa kiwango sawa! Kwani mahakamu ndio wanaofanya kazi zaidi ya idara zingine zote? walimu,madaktari,maaskari,wahasibu, na wengine hawana mchango ktk maendeleo ya nchi hii au vipi?