Mtabiri
Senior Member
- Jun 23, 2009
- 152
- 4
ONGEZEKO la mishahara ya majaji na mahakimu, limeibua mgogoro unatokana na watumishi wa idara hiyo ambao si mahakimu, kuipa serikali muda wa siku 60, kurekebisha viwango vyao vya mishahara vinginevyo, wataendesha mgomo nchi nzima. Waraka huo unaonyesha kuwa kiwango cha mshahara wa hakimu wa mahakama ya mwanzo daraja la kwanza, umepanda kutoka Sh193,340 hadi kufikia Sh400,000 wakati mishahara ya majaji imepanda kutoka Sh2,160,000 hadi kufikia Sh3,645,000. Source: http://mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=14998