Mahakama tuwe makini, tutafunga vichaa kila siku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama tuwe makini, tutafunga vichaa kila siku

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 26, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,483
  Likes Received: 5,718
  Trophy Points: 280
  Mbaroni kwa kudai ametumwa na Rais Kikwete kuchukua faili mahakamaniNa Sadick Mtulya

  MTU mmoja jana alikamatwa na maofisa usalama wa Ikulu baada ya udanganyifu Mahakamani kuwa ametumwa na Rais Jakaya Kikwete kuchukua jalada la kesi.

  Tukio hilo lilitokea jana saa 5:00 asubuhi katika Mahakama ya Ardhi wakati mtu huyo, ambaye jina lake halikuweza kutambulika na ambaye anakadiriwa kuwa kuwa na umri kati ya miaka 25 na 30, alipofika mahakamani hapo na kujitambulisha kuwa ametoka Ikulu na hivyo apewe jalada la kesi namba 182/2005 ili alifanyie uchunguzi.

  Baada ya kujieleza hivyo walinzi wa mahakama hiyo walimtaka aonyeshe kitambulisho chake na ndipo alipotoa kitambulisho ambacho kinamtambulisha kuwa ni afisa wa habari wa Rais Kikwete wakati alipokuwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  Hali hiyo iliwafanya askari wa mahakama hapo wazidi kumbana na ndipo mtu huyo alipoeleza kuwa “nimetumwa na Rais Kikwete, mimi ni ndugu wa rais Kikwete... ninaishi Ikulu”.

  Baada ya tukio hilo kuripotiwa, uongozi wa mahakama uliwasilina na Ikulu na muda baadaye maofisa hao walifika na kumchukua kijana huyo na kuondoka naye.

  Kijana huyo, ambaye alikuwa amevalia suruali ya kitambaa cha kijivu na shati jeupe lenye maua ya rangi ya bluu, aliingia mahakamani hapo na gari aina ya Toyota Landcruiser V8.

  Kwa mujibu wa uchunguzi wa Mwananchi, kijana huyo alikuwa amefuata jalada la kesi iliyofunguliwa Novemba 9, 2005 na Elizabeth Masandeko dhidi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kesi hiyo ilishamalizwa mahakamani hapo Mei 7, 2009 kwa NHC kushinda. Hadi Mwananchi inaondoka eneo la tukio, gari la kijana huyo lilikuwa bado kwenye maegesho ya mahakama hiyo.
   
Loading...