Mahakama ni Kikwazo katika vita ya ufisadi!

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Tumeshuhudia hukumu nyingi ambazo hata ukimpa mtoto anayesoma shule za msingi katika nchi yetu atawashangaa mahakimu wetu kwa hukumu zao.

masikini akiiba kuku huwa serikali haishindwi kuthibitisha hata siku moja wanahukumiwa miaka mingi sana. Lakini matatjiri au mafisadi wakishitakiwa hukumu zao huwa zinashangaza umma. mara zote serikali inashindwa kutoa ushahidi wa kuwatia hatiani mafisadi.

yapo mambo mengi ambayo serikali inafanya kwa sasa kurudisha nidhamu katika utendaji wa umma lakini mahakama imeonekana kwa mtizamo wangu kuwasafisha watuhumiwa.

mimi napendekeza Takukuru ianze kuchunguza mali za mahakimu na majaji wote kulinganisha na vipato vyao halali.

kuchunguza kuna nini nyuma ya hukumu za watu wenye mali kama kuna ushawishi wa mali hizo katika hukumu zinazotolewa utatusaidia katika vita dhidi ya ufisadi. ni vigumu kuona makabidhiano lakini sisi tufuatilie kule zinakoweza kuelekezwa baada ya makabidhiano tuone kama kuna dalili ya kuwepo fedha halamu.
 
serikali tunaona jitihada zao za kupamabana na ufisadi, bunge tunaona jinsi lilivyoanza kuunga serikali mkono.

lakini mahakama bado.

ila tukitafakari mfano ameletwa fisadi mahakami aliyekwapua mabilioni na akakutafuta wewe kama ungekuwa hakimu akaweka bilioni tano mezani ili umuondolee kadhia hii na uwezo unao kupitia kichaka cha ushahidi je ungefanya nini?

tunahitaji msukumo wa kuibadili mahakama lakini kwa dhamiri zao wenyewe ni vigumu.
 
Mwl Nyerere aliunda mahakama maalum kwaajili ya kupambana na walanguzi enzi za Marehemu Sokoine na Dr Magufuli lazima aunde mahakama maalum kwaajili ya kupamabana na ufisadi asipofanya hivyo hakika atajikuta anazunguka miaka 10 bila kutimiza malengo yoyote.
 
Lakini tambua hukumu hutolewa kutokana na shtaka alilishtakiwa nalo mtu. Mwizi wa mbuzi mmoja atapata kifungo kikubwa kuliko fisadi aliyetumia vibaya madaraka yake na kuisababishia serikali mabilion ya pesa. Kumbuka huyu fisaidi hashtakiwi kwa kosa la wizi. Hapa kosa ni la waendesha mashtaka, wala usiwatupie lawama mahakimu na majaji.
 
Tatizo liloko katika mhimili huu ni kutupiana lawama.

jaji anaposema ushahidi haukuwasilishwa wa kumtia hatiani mtuhumiwa, mpira unahamia kwa waleta mashitaka nao tunawasikia wakidai rushwa zimekithiri, hilo liko wazi wala halina mjadala, mara watengeneza sheria wanaangalia sheria zinawahusu wanalegeza adhabu mfano wakijua hawawezi kuiba kuku basi wanaweka adhabu kali lakini kwa yale makosa ambayo wanajiona wamo wanatania.

haya yote yanachangia lakini tukiyaruhusu yatupumbaze tutakaa siku zote tunamuangalia huyu anatuambia ni yule tunamuacha tunaenda kwa yule naye anatuelekeza kwingine tunabaki kuzunguka bila kupata jibu.

lazima tufanye maamuzi kwa kuangalia pa kuanzia ni wapi na tuondoe tatizo hilo na ni kwa kiongozi wa mhimili huu.

yeye tukisha tatua yaliyo kwake atasimama na anaweza kutoa hukumu za kuwaagiza watunga sheria kufanyia marekebisho ya sheria.

tuwabane hawa ndio tutaboresha sekita ya utoaji haki. tukiwabana hawa viongozi udhaifu wa hawa wengine utajionyesha wazi nao utashughulikiwa.

lakini hawa wengine wamekwisha onyesha nia ya kubadilika kwa maana ya serikali kama mtengeneza mashitaka na bunge kama mtunga sheria. huyu kinara wa huku ndiye bado anaonekana bado kutumia injini ya zamani hajafanyiwa overhaul ya nguvu.

Lakini tambua hukumu hutolewa kutokana na shtaka alilishtakiwa nalo mtu. Mwizi wa mbuzi mmoja atapata kifungo kikubwa kuliko fisadi aliyetumia vibaya madaraka yake na kuisababishia serikali mabilion ya pesa. Kumbuka huyu fisaidi hashtakiwi kwa kosa la wizi. Hapa kosa ni la waendesha mashtaka, wala usiwatupie lawama mahakimu na majaji.
 
Rais wetu ameliona hilo. Ndo maana Rais wetu ameahidi kuunda mahakama ya Majizi na Mafisadi
 
Kuunda mahakama maalumu ni kuhalalisha yanayotendeka katika mahakama zetu.

tunahitaji mabadiliko katika mahakama zetu sio kuunda nyingine. lazima tutafute kiini cha tatizo kiko wapi na tutibu.

haiwezekani mtu mmoja anapewa kufanya maamuzi ya hukumu then kwa sababu zake anazozijua yeye anadidimiza jitihada za watanzania za kujenga nidhamu katika utendaji wa umma tena kwa mambo yaliyo wazi.

lazima tuangalie tatizo liko wapi?

jamii nzima kukubaliana na uamuzi wa mtu mmoja ulioshawishiwa na rushwa sote tunakuwa walarushwa hata kama wengi hatujachukua chochote.

Mwl Nyerere aliunda mahakama maalum kwaajili ya kupambana na walanguzi enzi za Marehemu Sokoine na Dr Magufuli lazima aunde mahakama maalum kwaajili ya kupamabana na ufisadi asipofanya hivyo hakika atajikuta anazunguka miaka 10 bila kutimiza malengo yoyote.
 
Tumeshuhudia hukumu nyingi ambazo hata ukimpa mtoto anayesoma shule za msingi katika nchi yetu atawashangaa mahakimu wetu kwa hukumu zao.

masikini akiiba kuku huwa serikali haishindwi kuthibitisha hata siku moja wanahukumiwa miaka mingi sana. Lakini matatjiri au mafisadi wakishitakiwa hukumu zao huwa zinashangaza umma. mara zote serikali inashindwa kutoa ushahidi wa kuwatia hatiani mafisadi.

yapo mambo mengi ambayo serikali inafanya kwa sasa kurudisha nidhamu katika utendaji wa umma lakini mahakama imeonekana kwa mtizamo wangu kuwasafisha watuhumiwa.

mimi napendekeza Takukuru ianze kuchunguza mali za mahakimu na majaji wote kulinganisha na vipato vyao halali.

kuchunguza kuna nini nyuma ya hukumu za watu wenye mali kama kuna ushawishi wa mali hizo katika hukumu zinazotolewa utatusaidia katika vita dhidi ya ufisadi. ni vigumu kuona makabidhiano lakini sisi tufuatilie kule zinakoweza kuelekezwa baada ya makabidhiano tuone kama kuna dalili ya kuwepo fedha halamu.
Kasome sheria ndiyo uje hapa vinginevyo kakojoe ulale saa za kulala
 
Hivi wewe unajua maana ya sheria?

tunasoma kupata maarifa zaidi ya kukabiliana na nchangamoto za kimaisha lakini elimu hiyo hiyo inaweza kumgeuza aliyesoma kuwa mtumwa.

pale ulichokisoma kitazuia wewe kuwaza ukabaki kunukuu tu kile kilichoandikwa sehemu fulani herufi kwa herufi nukta kwa koma, huo ni utumwa.

sometimes mtu mwenye busara anaweza kuwa mjuzi wa sheria kuliko mwenye cheti cha sheria ambaye hawezi kutumia maarifa ya uanasheria kufanya maamuzi ya busara bali ni kunukuu vifungu ambavyo maamuzi yake hayaendani kimantiki na huku anazozitoa.

hatuhitaji wote kusoma sheria kuona kama haki imetendeka au sheria zimegeuzwa na anayedhani wananchi kuona yanayotendeka katika mifumo ya utoaji haki kama ni utoaji haki kweli au haki ni ngozi iliyofunika biashara nyingine kama ni mwanasheria basi huyo ni mtumwa wa sheria.

Kasome sheria ndiyo uje hapa vinginevyo kakojoe ulale saa za kulala
 
dawa ya ugonjwa si kuzaa wanadamu wengine zaidi ili kuchukua nafasi za wale wanaoumwa bali ni kutibu wale wanaoumwa.

hivyo hivyo kwa taasisi zetu tunahitaji taasisi kuzinduliwa kutoka katika usingizi na sio kuziacha ziendelee kusinzia tukianzisha nyingine bali tuziamshe. kama kuna wazembe wamulikwe, kama kuna wala rushwa wamulikwe, chochote kilicho nyuma ya pazia ya utendaji wa mahakama kimulikwe ili tiba ipatikane.

Rais wetu ameliona hilo. Ndo maana Rais wetu ameahidi kuunda mahakama ya Majizi na Mafisadi
 
Back
Top Bottom