Mahakama Kuu yazuia ‘njama’ za Serikali

Mahakama Kuu yazuia ‘njama’ za Serikali

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2018
Posts
4,514
Reaction score
23,703
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), amegonga mwamba mahakamani. Ni baada ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, “kuzima” mkakati wake wa kuchelewesha kesi ya kupinga muswaada wa vyama vya siasa.
IMG-20190104-WA0041-620x308.jpg

Jopo la majaji watatu wa mahakama kuu, wanaosikiliza kesi hiyo ya kikatiba, linaloongozwa na Jaji Barke Sahe, wameeleza mahakamani hapo kuwa suala lililopo mbele yake, “lina maslahi mapana kwa umma.”

Maelezo ya mahakama yamefuatia upande wa mwanasheria mkuu wa serikali, kuwasilisha maombi ya kupewa muda wa miezi miwili, ili kuweza kujibu kwa ufasaha hoja za wadai.

Kesi ya kupinga kuwasilishwa bungeni muswaada wa vyama vya siasa, imefunguliwa mahakamani hapo na Zitto Zuberi Kabwe, kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo.

Wengine walioshirikiana na Zitto, ni Joran Bashange, naibu katibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Tanzania Bara na Salim Biman, mkurugenzi wa mawasiliano ya umma ya chama hicho.

Akisoma maamuzi madogo yaliyotokana na maombi ya mwanasheria mkuu na yale ya upande wa wadai, Jaji Sahe alisema, “kwanza kabisa, mahakama imeona hakuna sababu ya kuchukua muda mrefu kwa serikali kujibu hoja za walalamikaji.”

Amesema, “Mahakama inatoa siku saba (7) za kujibu hoja hizi. Hii ni kutokana na suala lililoletwa mahakamani, kuwasilishwa kwa hati ya dharura na kubeba maslahi mapana ya jamii.”

Pili, jopo hilo la majaji limesema, “mahakama imeona hakuna sababu kwa sasa ya kutoa zuio kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuwasilisha bungeni, muswaada huo. Maamuzi yetu haya yanatokana na ukweli kuwa kesi hii, itasikilizwa kabla ya tarehe 29 Januari.”

Shauri hilo la madai Na. 31/ 2018 lilikuja mahakamani kwa mara ya kwanza leo Ijumaa kwa ajili ya kutajwa na kupanga siku ya kusikilizwa.

Katika shauri hilo, wadai hao watatu – Zitto, Bashange na Bimani – wanawakilishwa mahakamani na mawikili, Mpoki Mpare, Daim Halfan na Frederick Kihwelo.

Kabla ya maamuzi hayo, mawakili hao wa wadai waliiomba mahamakama kutoa zuio la muda la kupelekwa bungeni muswada wa sheria ya vyama vya siasa.

Kufuatia maombi hayo, upande wa serikali uliomba mahakama hiyo kutoa muda wa miezi miwili kuweza kujibu hoja hizo.

Serikali italazimika sasa, kujibu hoja zote zilizowasilishwa na wadai, siyo zaidi ya tarehe 11 Januari mwaka huu. Muswaada wa sheria ya vyama vya siasa, tayari umesomwa kwa mara ya kwanza bungeni; kwa mujibu wa ratiba ya Bunge, unatarajiwa kujadiliwa katika mkutano ujao wa Bunge.

Mkutano ujao wa Bunge, umepangwa kuanza tarehe 29 Januari mwaka huu.

Tangu kuwasilishwa kwa muswada huo bungeni, kumeibuka madai kadhaa kutoka vyama vya siasa, asasi za kiraia, makundi ya kijamii, wakieleza kuwa kilichowasilishwa bungeni, “ni ukandamizaji wa haki za wananchi.”

Makundi hayo yamekuwa yakidai kuwa kilichowasilishwa bungeni kinakwenda kuuwa moja kwa moja demokrasia. Wanasema, ndani ya muswaada, kujazwa mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa, kuingilia uhuru wa vyama hivyo na kufuta hata uwanachama wa wanachama wake.

-Mwanahalisi
 
Tuombe Mungu huyo judge asipewe memo tu kutoka 'juu' au asibadilishwe.
Uzuri ukishakua JUDGE, huna cheo kingine cha kupigania. Majaji huwa hawapelekeshwi, ila mahakimu ndio wanaweza kupelekeshwa kwa kuangalia yasije majina yao yakapigwa X kuapishwa na kupanda vyeo kua "JUDGE".[emoji18]

Haki itapatikana tu.
 
Jaman wana CCM wenzangu. Achaneni na mambo ya miswada tuendelee kunyukana kwa hoja. Hizi sheria zitakwenda kuua siasa na pasipo na siasa, hakuna maendeleo.
Hawa team pinzani nimegundua ni watu wepesi sana. Wanakujaga na hoja mfu iliyojazwa hisia kali. Ila ukiwajibu kwa upole na kuwadadavulia mambo wanaelewa na kukaa kimya.
Msiwazibe watu na plasta mdomoni. Waachwe waongee tujue duku duku lao wanataka nini ili tuwatafutie majibu sahihi ya hoja zao... Maisha yaendelee mbele.
Tumewamudu kwa miaka mitatu, hatuwezi shindwa kuwamudu kwa miaka saba iliyobaki.
Kama CCM haikufa 2015, basi hakuna neno au tendo la mwanasiasa wa upinzani litakalo iua CCM.
Wapinzani ni kama nyoka wa Kibisa. Tunaweza kucheza nao tu bila kuwaogopa kutuuma kwa kuwa hawana sumu kali. Ni sawa tu na tembo kuumwa na mbu.
 
Mkuu hapa nimekuelewa vizuri sana.
Leo wanasifu ila kesho watasema mahakM hazitendi haki.
Refer issue ya promota mbowe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni ukweli lazima usemwe!!!! Sio favor ni haki!!! Kuna tatizo gani ndani ya vyama vya siasa mpaka nguvu kubwa apewe msajili ambae ni mteule wa mwenyekkiti wa chama kinachotawala ??? Power of reasoning!! Hakuna!!! Kuna sheria nyingi za hovyo za kushughulika nazo sio hiz za kudhoofisha vyama!!! Atafeli si rwanda hii!!! Tunamtazamaaaaaa!!!! Tunampimia tu!!!
 
Jaman wana CCM wenzangu. Achaneni na mambo ya miswada tuendelee kunyukana kwa hoja. Hizi sheria zitakwenda kuua siasa na pasipo na siasa, hakuna maendeleo.
Hawa team pinzani nimegundua ni watu wepesi sana. Wanakujaga na hoja mfu iliyojazwa hisia kali. Ila ukiwajibu kwa upole na kuwadadavulia mambo wanaelewa na kukaa kimya.
Msiwazibe watu na plasta mdomoni. Waachwe waongee tujue duku duku lao wanataka nini ili tuwatafutie majibu sahihi ya hoja zao... Maisha yaendelee mbele.
Tumewamudu kwa miaka mitatu, hatuwezi shindwa kuwamudu kwa miaka saba iliyobaki.
Kama CCM haikufa 2015, basi hakuna neno au tendo la mwanasiasa wa upinzani litakalo iua CCM.
Wapinzani ni kama nyoka wa Kibisa. Tunaweza kucheza nao tu bila kuwaogopa kutuuma kwa kuwa hawana sumu kali. Ni sawa tu na tembo kuumwa na mbu.
Uwezo wako wa kufikiri na kujenga hoja ni mdogo sana!!!! Umemmudu nani???
 
Mkuu wenu hajiamini kabisa, yaani ni bure, mtupuu! Vitisho tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), amegonga mwamba mahakamani. Ni baada ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, “kuzima” mkakati wake wa kuchelewesha kesi ya kupinga muswaada wa vyama vya siasa.View attachment 987319

Jopo la majaji watatu wa mahakama kuu, wanaosikiliza kesi hiyo ya kikatiba, linaloongozwa na Jaji Barke Sahe, wameeleza mahakamani hapo kuwa suala lililopo mbele yake, “lina maslahi mapana kwa umma.”

Maelezo ya mahakama yamefuatia upande wa mwanasheria mkuu wa serikali, kuwasilisha maombi ya kupewa muda wa miezi miwili, ili kuweza kujibu kwa ufasaha hoja za wadai.

Kesi ya kupinga kuwasilishwa bungeni muswaada wa vyama vya siasa, imefunguliwa mahakamani hapo na Zitto Zuberi Kabwe, kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo.

Wengine walioshirikiana na Zitto, ni Joran Bashange, naibu katibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Tanzania Bara na Salim Biman, mkurugenzi wa mawasiliano ya umma ya chama hicho.

Akisoma maamuzi madogo yaliyotokana na maombi ya mwanasheria mkuu na yale ya upande wa wadai, Jaji Sahe alisema, “kwanza kabisa, mahakama imeona hakuna sababu ya kuchukua muda mrefu kwa serikali kujibu hoja za walalamikaji.”

Amesema, “Mahakama inatoa siku saba (7) za kujibu hoja hizi. Hii ni kutokana na suala lililoletwa mahakamani, kuwasilishwa kwa hati ya dharura na kubeba maslahi mapana ya jamii.”

Pili, jopo hilo la majaji limesema, “mahakama imeona hakuna sababu kwa sasa ya kutoa zuio kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuwasilisha bungeni, muswaada huo. Maamuzi yetu haya yanatokana na ukweli kuwa kesi hii, itasikilizwa kabla ya tarehe 29 Januari.”

Shauri hilo la madai Na. 31/ 2018 lilikuja mahakamani kwa mara ya kwanza leo Ijumaa kwa ajili ya kutajwa na kupanga siku ya kusikilizwa.

Katika shauri hilo, wadai hao watatu – Zitto, Bashange na Bimani – wanawakilishwa mahakamani na mawikili, Mpoki Mpare, Daim Halfan na Frederick Kihwelo.

Kabla ya maamuzi hayo, mawakili hao wa wadai waliiomba mahamakama kutoa zuio la muda la kupelekwa bungeni muswada wa sheria ya vyama vya siasa.

Kufuatia maombi hayo, upande wa serikali uliomba mahakama hiyo kutoa muda wa miezi miwili kuweza kujibu hoja hizo.

Serikali italazimika sasa, kujibu hoja zote zilizowasilishwa na wadai, siyo zaidi ya tarehe 11 Januari mwaka huu. Muswaada wa sheria ya vyama vya siasa, tayari umesomwa kwa mara ya kwanza bungeni; kwa mujibu wa ratiba ya Bunge, unatarajiwa kujadiliwa katika mkutano ujao wa Bunge.

Mkutano ujao wa Bunge, umepangwa kuanza tarehe 29 Januari mwaka huu.

Tangu kuwasilishwa kwa muswada huo bungeni, kumeibuka madai kadhaa kutoka vyama vya siasa, asasi za kiraia, makundi ya kijamii, wakieleza kuwa kilichowasilishwa bungeni, “ni ukandamizaji wa haki za wananchi.”

Makundi hayo yamekuwa yakidai kuwa kilichowasilishwa bungeni kinakwenda kuuwa moja kwa moja demokrasia. Wanasema, ndani ya muswaada, kujazwa mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa, kuingilia uhuru wa vyama hivyo na kufuta hata uwanachama wa wanachama wake.

-Mwanahalisi
Kama walitayarisha mswaada wao wanashindwaje kuutetea kwa muda mfupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom