Mahakama Kuu yatupilia mbali pingamizi la CUF (upande wa Maalim Seif) kuhusu ruzuku

MOSHIFST

Senior Member
Jun 4, 2014
112
250
DAR: Mahakama Kuu imetupilia mbali pingamizi la CUF upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif kutaka Msajili wa Vyama vya Siasa asiipe CUF ruzuku.

=============
Nyongeza kutoka mahakama kuu:

Jaji Wilfred Dyansobera ameliondoa (Struck out) shauri la madai namba 21/2017 bila gharama. Shauri hilo linahusu Wizi wa fedha za ruzuku ya CUF milioni 369 kutokana na kifungu kilichotumika kufungulia shauri hilo haikipi Mahakama mamlaka ya kulisikiliza shauri hilo.

Mawakili wetu wanarekebisha kasoro hizo na Jumatatu wana-file upya shauri hilo.
 

MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
1,682
2,000
Kutoka Mahakamani.

Mahakama imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na CUF Maalim Seif ya kutaka CUF Lipumba wasipewe RUZUKU.

=====

Updates From High Court:

Jaji Wilfred Dyansobera ameliondoa (Struck out) shauri la madai namba 21/2017 bila gharama. Shauri hilo linahusu Wizi wa fedha za ruzuku ya CUF milioni 369 kutokana na kifungu kilichotumika kufungulia shauri hilo haikipi Mahakama mamlaka ya kulisikiliza shauri hilo.

Mawakili wetu wanarekebisha kasoro hizo na Jumatatu wana-file upya shauri hilo.


======


Mahakama Kuu imetupilia mbali pingamizi hilo leo tarehe 11 Agosti 2017, kufuatia Chama Cha CUF huko nyuma kufungua kesi ya msingi ya madai kuhusu wizi wa ruzuku na shauri dogo la kuweka zuio kutolewa kwa ruzuku ya chama kutokana na wizi wa shilingi milioni 369 ambazo zilidaiwa kuibwa na Lipumba na kundi lake kwa kushirikiana na Msajili wa Vyama Vya Siasa.

Pingamizi hilo limedumu kwa miezi minne kutoka Machi mwaka huu mpaka Agosti ambapo leo Mahakama Kuu imetupilia mbali zuio hilo lililowekwa na CUF upande wa Katibu Mkuu, hali ambayo inapelekea Msajili wa Vyama vya Siasa kuendelea kutoa ruzuku ya Chama hicho kwa Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Profesa. Ibrahi Lipumba na wananchama wake ambao wanamuunga mkono.

Toka mwezi wa Septemba 24, 2016 baada ya Profesa Lipumba kudaiwa kufanya uvamizi wa ofisi za chama cha CUF pale Buguruni kinyume na sheria na taratibu baada ya Kujiuzulu kwa hiari yake na kuiacha ofisi hiyo takribani kwa kipindi cha mwaka mzima ndipo ulipoanza mgogoro kati ya pande mbili, upande unaomuunga mkono Lipumba na upande unaomuunga mkono Maarim Seif jambo ambalo limesababisha madhara mengi ya moja kwa moja ndani ya chama hicho.
 

Ralph Tyler

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
2,489
2,000
Hata mimi nisiyekuwa mwanasheria nilijua Maalim na kundi lake wangepigwa. Lipumba na wenzie walishamzidi kimkakati mapema sana. Maalim alikosea jambo moja tu, kuchelewa kuridhia kujiuzulu kwa Lipumba. Kuna methali ya kiingereza "strike the iron when it is hot". Maalim alichelewa.
Hata kwenye boxing sisi wadau wa mchezo huo tunajua. Ukimpa mpinzani wako upper cut moja akapepesuka, usimsubiri aka-recover. Anaweza akaibuka akakutoa. Ukishaona amepepesuka unaongeza za mfululizo hapohapo hadi knock-out. Lipumba alipojiuzulu, wangejaza nafasi immediately kwa utaratibu rasmi wa kikatiba. Walikosea hapo, sasa wanapata malipo yake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom