Mahakama Kuu yamtambua Prof. Lipumba kama Mwenyekiti halali wa CUF

HIVI SISI CCM MBONA TUNAKUWA NA CONCERN KUBWA NA CHADEMA NA CUF? NA MBOWE NA MAALIM SEIF?

MBONA HATUNA CONCERN UENYEKITI/UONGOZI WA
1:FAHAM DOVUTWA
2:HASHIM RUNGWE
3:JAMES MBATIA NCCR
4:AUGUSTINE MREMA TLP

KUNA NINI KUHUSU MBOWE? CHADEMA? MAALIM SEIF?

TUSIFANYE KAMA MZAZI ALIYESHINDWA KULEA WATOTO KISHA ANAENDA KITUO CHA WATOTO YATIMA KUMCHUKUA MTOTO YATIMA AMLEE !

...
nenooooooo
 
Chama chako tu cha kijani ccm kimekaa madarakani miongo mingapi toka Uhuru ? kimewafanyia nini watanzania zaidi ya kuwafukarisha na kuwapa umaskini wa kutupa .
Kwahiyo unataka king'atuke? Hao unaosema kimewafukarisha wanakichagua maana hawajaona kinachoweza kuwatajirisha. Najua utakuja na hoja mfu kuwa mnaibiwa.
 
Mimi naona siasa ndio zinaanza sasa hivi! Mbadala ya CUF ni ZLO, Zanzibar Liberation Organisation. Kwa heri Tanzania, Karibuni Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar!
 
Leo ndio siku iliyopangwa kutolewa hukumu ya uhalali wa Uenyekiti wa Lipumba CUF.

Ninamtakia kila la heri Maalim Seif .


----Updates----

MAHAKAMA KUU YAMTAMBUA PROF LIPUMBA KAMA MWENYEKITI HALALI WA CUF

Uamuzi huu umetolewa leo baada ya kuwekwa pingamizi dhidi ya Uenyekiti wa Lipumba ndani ya chama hicho

Pingamizi lilifunguliwa baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kama ni Mwanyekiti halali wa Chama cha Wananchi(CUF)

Kesi hii ilifunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa chama hicho kwa upande unaomuunga mkono Maalim Seif

Wazanzibari wanasema lipumbafu anakaribishwa ila ajue kuwa amekabidhiwa tu zile herufi tatu CUF lakini wanachama hana.
 
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa hukumu inayotambua Profesa Ibrahim Haruna Lipumba kuwa Mwenyekiti halali wa Chama cha Wananchi (CUF) baada ya kushinda kesi iliyotokana na mvutano wa uongozi dhidi ya ‘CUF ya Maalim Seif Sharif Hammad’ leo Jumatatu, Machi 18, 2019.
Hukumu hiyo inatokana na kesi Namba 23/2016 iliyokuwa mbele ya Jaji Benhajj Masoud.



Kiini cha mgogoro huo ni mgawanyiko wa wanachama ambapo upande mmoja ulikuwa kwa upande Lipumba na mwingine kwa Maalim Seif ambaye alikuwa Katibu Mkuu.



Taarifa zinaonyesha mpaka kufikia lo, hukumu hiyo ilikuwa imeahirishwa mara nnne na mara ya kwanza, ilitakiwa kusomwa Oktoba 10, 2018, iliahirishwa hadi Novemba 30, 2018, ikaahirishwa tena hadi Januari 15, 2019, ikiaahirishwa tena hadi Februari 22, 2019 na sasa imeahirishwa hadi Machi 18, 2019 ambayo ni leo.

Profesa Lipumba alijiuzulu nafasi ya uenyekiti Agosti 6, 2015 wakati chama kinaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na rais na kutimkia nj ya nchi ambapo baada ya ya uchaguzi alireja nchini na kurudi knye chama chake.

Wiki iliyopita Profesa Lipumba alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa kupata kura 516, akiwashinda wapinzani wake, Zubeir Hamis aliyepata kura 36 na Diana aliyepata kura 16. Makamu Mwenyekiti Zanzibar, alichaguliwa Abbas Juma Mhunzi aliyepata kura 349, wakati Makamu Mwenyekiti Bara, alichaguliwa Maftah Nachuma kwa kura 231.

Juzi Baraza Kuu la Uongozi, lilimchagua Khalifa Suleiman Khalifa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho. Baada ya kupigiwa kura Khalifa alitangazwa mshindi kwa kupata kura 37, huku mpinzani wake Masoud Said Suleiman akijipatia kura 11.
Ukifanyika uchaguzi Chadema hivi leo mambo yatawaka moto
 
CUF Lipumba haina nguvu itaishia kufa na ingewezekana Maalim Seif akate rufaa kwani huyo Jaji kajitoa fahamu katoa hukumu kwa mujibu wa zidumu fikra za Mwenyekiti wa CCM na Bashite Maliyamungu Naibu Rais siyo kwa mujibu wa sheria na katiba ya Tanzania, Mahakama haipo Huru inafanya kazi kwa Amri toka juu
Kukata rufaa si lazima ushinde unawezapigwa chini vilevile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu mgogoro wa CUF chini ya supervision ya Msajiri na serikali ya ccm utakuja kusababisha uvunjifu wa Amani na wao bila kujua wana ccm wengi na hasa viongozi wao ndio wataathirika.
Wamesahau yaliyo kuwa yanajitokeza hapo jirani tuu kuelekea kule kusini?

Sent using Jamii Forums mobile app

Wenyewe huwa wanaimba kama noma na iwe noma, unadhani huwa wanamaanisha nini? That is what they want walishashindwa kote hii ni karats yao ya mwisho. Ingekuwa sivyo leo hii serif angekuwa rais Zanzibar


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom