Mahakama Kuu: Sheria inayozuia watuhumiwa kupewa dhamana ni kinyume cha Katiba. Serikali yaazimia kukata rufaa

Hivi haiwezekani kubadili kifungu Cha Katiba ili kiendane na hicho kifungu Cha Sheria? Maana isije mkawazania kwenye kubadili kifungu Cha Sheria ili kiendane na katiba wanaweza fanya kinyume chake,
 
It is not over yet mpaka siku 30 zipite kama hawatakata rufaa

Pia bado kuna mkanganyiko wa nani kati ya bunge na mahakama mwenye jukumu la kutunga sheria ni nani , mahakama inatakiwa kuiamuru mahakama kurekebisha hivyo iwe jukumu la serikali, kamati au mtu kupeleka mabadiliko hayo

Safari ni ndefu
 
Hii kesi na ile ya Freeman Aikael Mbowe na Esther Matiko zitakuwa zimeweka mwanzo mzuri sana wa utoaji haki ya dhamana kwa mahakama zetu.

Haki ya dhamana ilikuwa inapotezwa na mambo mawili makuu.
1 sheria kuzuia dhamana kwa makosa fulani fulani

2 mahakama kuweka mashart magumu sana ya dhamana kiasi cha mtuhumiwa kushindwa kuyatimiza.

Hebu jiulize mtu kashitakiwa kwa kosa la dogo tu lakini anapewa Mashart ya kupeleka hati ya Mali isiyohamishika na wadhamini mmoja awe mtumishi wa umma watu wangapi wamekosa dhamana kwa mashart ya ajabu namna hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walio ziandika hizi sheria ni watumishi wa wizara ya sheria. Walio zipigia kura za ndiyooo ni wabunge wa Ccm wasio jua sheria. Wanao ziona zina makosa ni majaji wa serikali hii hii inauo ongozwa na Ccm. Hadi raha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii serikali haitambui hayo kwani yenyewe inajua iko juu ya sheria.
 
Walio ziandika hizi sheria ni watumishi wa wizara ya sheria. Walio zipigia kura za ndiyooo ni wabunge wa Ccm wasio jua sheria. Wanao ziona zina makosa ni majaji wa serikali hii hii inauo ongozwa na Ccm. Hadi raha

Sent using Jamii Forums mobile app
PC ni ya enzi ya chama kimoja licha ya marekebisho ya mwaka 1993 na 2002 bado yameacha matatizo hasa dhamana, arresting na upelelezi

Tume ya nyalali ilifunika mengi
 
Hii nayo ni kama ile ya Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi, nayo wataikatia rufaa na Serikali itashinda. Tusubiri tuone

Kama vile ilivyo tume ya uchaguzi kuwa ni silaha yao muhimu, hii pia ni moja ya silaha muhimu ambayo kamwe hawatokubali kuiachia iende. Haitakaa itokee hicho kitu never.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pumbavu sana hao Mahakama kwanini wasitoe siku moja ya kukutetea kwa serikali hasa ikizingatiwa serikali hii ya gangster inawatesa watu jela kwa sheria za kijingajinga hizi?
 
Mwanzo mzuri ila wanaonufaika na hizo sheria kandamizi hawatakubali kushindwa kirahisi (mfano kesi ya Marehemu Mtikila ya kuruhusu mgombea binafsi).
 
SERIKALI KUKATA RUFAA DHIDI YA HUKUMU YA SHERIA YA MAKOSA YA JINAI

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameazimia kukata Rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa leo na Mahakama Kuu ya Tanzania ya kutaka Serikali kufanyia marekebisho Kifungu 148(5) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai ndani ya miezi 18

Makosa yanayohesabiwa kwenye kwenye kifungu hicho ni pamoja na Utakatishaji fedha, uuzaji #DawaZaKulevya na uhujumu uchumi
 
H Huu muhimili mmoja leo umetambua kuwa nao una mizizi iliyokwenda chini kama ule muhimili wenye jeuri ya pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…