Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 440
- 3,211
Leo Februari 16, 2026, Jopo la Majaji watatu Mheshimiwa Jaji Fahamu, J. Mheshimiwa Jaji Chuma, na Mheshimiwa Jaji Kamana, limeamua kuwa kifungu cha 194 cha sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act (CPA) ni kinyume cha Katiba kwa kuwa kinampa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai haki ya kipekee kuomba ulinzi wa shahidi bila kumpa mshtakiwa haki sawa, na pia kinaruhusu maombi ya kusikilizwa upande mmoja bila kuhakikisha haki ya kusikilizwa kwa upande mwingine.
Mahakama imetangaza kifungu hicho kuwa batili na imeipa Serikali muda wa miezi 12 kufanya marekebisho ya sheria. Itakumbukwa kwamba, Jamhuri walitumia kifungu hicho na kupeleka Maombi mahakama kuu mbele ya Jaji Mtembwa ambaye alikubali Maombi ya Jamhuri kuficha mashahidi wao wakiita ulinzi wa mashaidi.
Maombi hayo yanasajiliwa na Jamhuri peke yao, wanasikilizwa peke yao na Mahakama inatoa uamuzi. Angalau leo, Mahakama kuu imetamka kwamba Kifungu hicho ni kinyume na Katiba!
Pia soma>> Mawakili zaidi ya 13 wafungua kesi kupinga mashahidi wa siri, wakidai inaleta changamoto za haki na uwazi
Ni kupitia Petition NO. 22482 /2025, kati ya GODFREY MJUNI MARTIN BASASINGOHE dhidi ya ATTORNEY GENERAL & DIRECTOR OF PUBLIC PROSECUTIONS.
======================
Akizungumzia uamuzi huo, Mkurugenzi wa Sheria wa CHADEMA, Wakili Gaston Garubindi amesema, hauwezi kuathiri mwenendo wa kesi ya mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, kwani Mahakama imeipa Serikali miezi 12 kurekebisha sharia hiyo.
“Kwa sasa Serikali imepewa miezi 12 kurekebisha, kwa hiyo sharia inaendelea mpaka muda huo upite. Ukipita sharia hiyo inakuwa batili,” amesema.